Mohamed Dewji (MO) aliyepotea, apatikana. Amerudi nyumbani akiwa salama

Mohamed Dewji (MO) aliyepotea, apatikana. Amerudi nyumbani akiwa salama

Yaani kelele za Lema ziwe msingi wa kupatikana Dewji lakini kelele hizo hizo zisiweze kumleta Ben Saanane? You must be joking!

Nani mwenye uhusiano wa karibu kikazi na kimaisha kati ya Lema na Ben Saanene au Dewji?

Kumbuka Ben Saanane alikuwa mfanyakazi wa CHADEMA

Ulichofanya ni kutoa shukrani ambazo hazina hata ukweli kifikra!
Hujitambui
 
Baada ya press ya Ziro ku-backfire wameamua wamuachie..
Ila sidhani kama ataweza kusema yaliyomkuta, yatakuwa kama yale ya Roma.
Hahahaaaaa lazima awe bubu aisee, ila sijawahi kuona watu wajinga kama watu wasiojulikana maana michezo yao niya kijinga na yakitoto ila ipo siku tutawatoa ujinga wao ili tuheshimiane!.
 
Wanasema gari lile lile na plate namba zile zile ndiyo limepatikana kwenye eneo la tukio..Gymkhana .
Kwa mujibu wa itv gar linaonekana limepachikwa namba nyingine ila za tz....
 
Wamebana wameachia, Jiwe siyo Mtu!.

Namshauri Mo asepe atulie zake huko Brunei au Kisiwa chochote cha Pasifiki ale bata miaka saba ipite kisha arudi tujenge nchi!, yeye bado kijana, kupumzika miaka saba siyo ishu!
Wewe mwenyewe utaenda kupumzika wapi hiyo miaka 7, au tandale kwa mtogole haha..
 
Kama Ni hivyo Lema si apige Press release nyingine kina Kubenea na Anthony Komu nao wamuachie Ben Sanane
 
Na gari lilitumika kumtekea, limepatikana likiwa limebadilishwa namba...Mambosasa ndio ametoa habari hiyo
IMG_20181020_062543.jpg
IMG_20181020_062548.jpg
 
Hii inaonyesha familia wamelipa ransom!

Moja ya masharti ya ransom ni kutozungumza kuhusu tukio lote!

Kama atazungumza kuhusu yaliyomsibu mpaka akarudi basi hiyo itaonyesha kuwa hakulipa ransom na hakuna makubaliano.

Hoja iliyopo mbele yetu kwa sasa, Je, kama amelipa ransom, nini kwa sasa nafasi ya matajiri nchini kuhusiana na usalama wao kwa sababu kulipa ransom ni kufungua mlango wa biashara ya kidnapping and ransom nchini kwa matajiri.

Kosa la kulipa ransom baada ya kutekwa ambalo nchi za kusini mwa Afrika kama Afrika Kusini na Msumbiji walilianza kwa matajiri ndilo kwa sasa linazidi kuwatafuta kwa kasi zaidi.

Je, kuna uwezekano na Tanzania tukaelekea ambako nchi za kusini mwa Afrika ziliko kwenye biashara ya kidnapping and ransom?
Hapana mkuu, hii ni UNITED REPUBLIC OF GANGSTER .
 
Kelele za wanajamiii Forum namini pia zimesaidia Sana maana watu tulikuwa hatuamini amini kirahisi tarifa Fulani Fulani
 
SERIKALI NA CCM NDIO WAMETUINGIZA KATIKA UCHAFU! VITU VILIUZWA LEO UNAANZA KUDAI NI UHUJUMU UCHUMI AU MTU KUJITAJIRISH KWA MALI ZA UMMA?? NYUMBA ZA SERIKALI ZILIZOUZWA KWA M3, NYUMBA YA KIGAE AMBAYO THAMANI YAKE NI ZAIDI YA MILIONI 80 ILIWEZEKANA VIPI??

Mtu kapiga halaf hashtakiki na hata akishtakika hashindwi kesi. Sasa unamfanyaje. Mtihani kwa kweli. Pole zao wenye kuchukua hatua za lawama
 
Back
Top Bottom