Daah... Nyie binadamu ni balaa tupu! Alipopotea mkailaumu serikali, kapatikana bado mnailaumu serikali. Naamini hata asingetekwa mgeilaumu serikali.
Nakuunga mkono asilimia mia moja.
Sisi tushukuru MO kapatikana inamaana waliomteka wanawapenda Watanzania kwa kuwasikia jinsi walivyoumizwa kwa kitendo chao hicho.
Kumbuka watekaji nao ni binadamu, wana moyo wa huruma pia. Wangemuuwa tungefanyeje ?
Binafsi Nawashukuru sana watekaji, kwa kitendo cha kusikiliza kilio cha sisi Watanzania.
MO usifadhaike mdogo wangu, mashujaa wote wamepitia majaribu mazito.
Sasa umekuwa shujaa zaidi, dunia yote imekutambua, hadi Uchina walikutangaza kwa a
Kichina.
Hadi visiwa vya Maldive wanakujua kwa sasa.
Tumia hii fulsa sasa kutangaza biashara zako.
Sisi Wanafilosofia tunaamini kwamba, katika kila jambo unaloona ni baya, basi lina faida kubwa kwa upande wa pili.
Sasa hivi Unapendwa sana kuliko kabla ya kutekwa.
Njoo mpirani uone kishindo chake.
Wamekutangaza sasa.
Usifadhaike wala kujutia wala kikata tamaa
Mimi sikupi pole,
Bali.
NAKUPONGEZA.