Mohamed Dewji (MO) aliyepotea, apatikana. Amerudi nyumbani akiwa salama

Mohamed Dewji (MO) aliyepotea, apatikana. Amerudi nyumbani akiwa salama

Kwa yote tunayojua Mo na kila mtu alijua kupatika kwa MO polisi walipaswa kujulishwa kwanza. Ninashangaa kwa nini polisi walipewa umuhimu wa mwisho pamoja na juhudi kubwa walizokuwa wamefanya?
 
Watanzania wenzangu kuna mahali sijaelewa, hivi inawezekanaje gari litoke kawe hadi jimkana barabara yenye ulinzi mzito tena kwa kutumia gari iliyokwisha kuonyeshwa hadharani kuwa ndo ilotumika kumteka?
Hii kitu inaniumiza sana kichwa🙂😉🙂😉
 
Hii muvi imechezwa kienyeji Sana walicho weza wao n kumwacha MO na midev tu lkn huko mafichon kungekuwa na salon angenyolewa hata hizo ndevu lkn ndo hivyo! Kweli nchi isha waona watanzania n mazuzu Sana! Kisa tajir katangaza kufunga viwanda vyake hapo lazima ugwae mwenyewe make nchi haina kiwanda hata cha tooth stick
 
Ulinzi mkali huwa uko sehemu gani mkuu?
Barabara ya old hasan mwinyi pembezoni wanaishi watu wakubwa na viongozi, yupo mwinyi,mama maria ndo makao makuu ya JKT na barabara nzima nyumba nyingi zina kamera, syo rahisi gari lililokwisha tajwa ni hatari na linalosakwa lipite, ni muujiza tu kuamini
 
Majibu ya hilo swali lako yatakuwa bado maswali. Kupata jibu la moja kwa moja bado ni ngumu sana, kwa hili tukio.
 
Barabara ya old hasan mwinyi pembezoni wanaishi watu wakubwa na viongozi, yupo mwinyi,mama maria ndo makao makuu ya JKT na barabara nzima nyumba nyingi zina kamera, syo rahisi gari lililokwisha tajwa ni hatari na linalosakwa lipite, ni muujiza tu kuamini
mbona kuna alternative nyingi sio lazima lipite Njia hiyo tu
 
mbona kuna alternative nyingi sio lazima lipite Njia hiyo tu
Hivi unachotetea ni kitu gani hasa? Una maslahi gani kwenye kutetea kila kitu kibaya kinachofanywa na baadhi ya mamlaka za serikali?
1. Kuuwawa kwa Mwangosi mlitete
2. Kuuwawa kwa AKwilina mlitetea
3. Watu kufia mikononi mwa polisi mkafananisha na wanaokufa wakiwa gesti ...
4. Kuuwawa kwa Kombe baada ya kufananishwa na jambazi
5. Kupotea kwa akina Saanane, mwandishi wa gazeti la mwananchi
6. kupotea kwa yule kiongozi wa Kigoma
7. Kuuwawa kwa Mawazo
etc etc

Hivi mnateteaga kwa maslahi gani?
 
Watanzania wa mtandaoni ni tofauti na waliopo kwenye field/ground. Refer to maandamano ya Mange.


Hii ya Muhindi ni funga kazi haijawahi kutokea, hata Nyerere hakuwahi kupata sapoti kubwa ya negros kama aliyopewa Muhindi!
 
Aisee wewe umeona mbaali sana! Yaani jumuiya ya wahindi wote kimya! Lakini wale jamaa ni wazuri sana kwa upande wa filam hivyo waliona ile ni filamu ya kiwango cha chini sana ambayo kule kwao huchezwa na watoto wa chekechea wakaona haina haja hata ya kuiangalia. Ila sisi kama ambavyo huwa unaona bongo movies zetu jambazi anavamia lakini kabla hajaingia ndani anavua viatu ili asichafue kapeti ndio tukashobokea na kupiga kelele kuliko "wafiwa wenyewe" Ni ushamba wetu ndio uliotuponza. Ndio maana kuna mwenzetu mmoja wa suti 6 za bendera ya taifa akaona tunapoteza muda bure akapiga marufuku kujadili kuhusu filam ya kitoto kama hiyo
 
Katika nchi zote kweli hii ni kiboko ya zote kwa vyote,Mungu anatuona lakini,haya ndiyo yangu machache
 
Back
Top Bottom