Mohamed Mwameja: Siwezi kumsamehe Muhidin Ndolanga

Mohamed Mwameja: Siwezi kumsamehe Muhidin Ndolanga

Hayo ya mwameja, ukisikia ya yusuf macho jinsi alivofanyiwa na hawa jamaa unaweza toka machozi japo hayakuhusu
Mwaga nondo mkuu. Ya Yusuf Macho ilikuwaje?
 
Anaitwa ALHAJ MUHIDIN NDOLANGA. Kuna wkt ktk utawala wake safu ya juu ya FAT wote walienda Makka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
POLE SANA...Tanzania One wetu wa jana...

Mpira wa bongo una wachawi wengi, roho za kwanini, unaidai timu, unachukua hela ya mchezaji, kisha unambania kupata riziki..

Duuh sasa hao ndiyo viongozi, wa chama cha mpira nchi, ukienda vyama vya mikoa nako ni balaa, fitina, unafiki, viherehere n.k.

Na manabii wote wapakwa mafuta tulionao na upepo wa kisulisuli umeshindwa kuzitoa hizo tabia...mbaya SANA

Everyday is Saturday..................😎
 
" Mwaka 96 nikiwa South Africa kuna mdau wa Jomo Cosmos aliniona akanifuata hotelini kwangu akaniuliza kama Nina wakala nikamwambia sina.

Akaniambia Mimi Nina Shida ya Goal Keeper kwenye timu yangu Lakini Uingereza Kuna timu pia inahitaji kipa ( Reading FC wakiwa daraja la TATU ) Kwa hiyo ninafanya mpango baada ya wiki moja nitakutumia pesa uje South u sign Jomo Cosmos then nikupeleke Reading UK ukiwa kama mchezaji wa Jomo Cosmos.

Mwameja aliomba Dola elfu kumi Jamaa akawambia atamtumia Kwanza Dola elfu sita halafu dola.elfu nne itakayo Baki atapewa Akisha fika Sauz.

Hiyo dola.elfu sita ilitumwa kwangu kupitia Fat, Fat wakaizuia hiyo pesa wakisema wanaidai Simba Kwa hiyo wamekata Deni Lao.

Nili mind Sana suala Hilo na nilipishana kauli na Ndolanga na baadhi ya viongozi WA Simba ambao walionekana kusapoti ujinga Huo.

Nilienda Sauz kinyonge sana Kwa kulazimika kutafuta pesa yangu mwenyewe kumlipia tiketi ya ndege, nikifika Sauz nikiwa nimechelewa so Jamaa WA Jomo akasema inabidi niende Kwanza UK nikafanye training na Reading Kwa sababu walikua Wana nihitaji Kwa wakati Huo na nilikuwa nje ya muda..

Kufika UK nikafanya training na kweli nikafaulu so ikabaki kusign mkataba.

Reading walihitaji nipate kitu kinaitwa ITC ( International Training Certificate) kupiga simu Tz Ndolanga na Rage wakabana.

Nilikuwa stressed sana nikarudi bongo na kwenda Hadi office za Fat. Tulipishana maneno na Ndolanga, Rage akapiga simu polisi waje wanichukue Lakini polisi walivyo fika na kugundua NI Mimi na baada ya Mimi kuwaeleza chanzo cha Ndolanga kunifanyia fitna wali amua tumalizane wenyewe kwenye vikao vyetu

Rage aliwahi kuniita wakati Fulani akaniomba msamaha but Ndolanga sintoweza kumsamehe daima.

Nikisema nimemsamehe nitakuwa mnafiki. Siwezi kumsamehe Kwa sababu ameniharibia maisha.

# Mungu' ampe subra Kaka yetu Mohamed Mwameja.
Hata mie nisingesamehe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata mimi nina mchongo wa kwenda mambele, ila kila nikiwaza ofisi ninazotakiwa kwenda ili wanicertify napata stress sana.

Wabongo wakishaona unaenda kuyakamata maisha wanakuingizia figisu sijui kwa nini!

Unforgetable
 
ndolanga na rage ni viongozi wa ovyo waliowahi kuongoza mpira Tanzania
Mnakumbuka mwaka 1998, Yanga waliingia makundi klabu bingwa wa Afrika,Caf waliwapa Yanga takribani million Mia mbili na ushee,Ndolanga na Rage waliupiga juu kwa juu mkwanja wa Yanga,na kutoka madai mbalimbali ya kuwa wao(FAT)wanawadai pesa nyingi wana wa jangwani,kwa hiyo hawastahili kudai chochote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baba ako amepata hasara sana kuzaa Toto km Wew

Sent using Jamii Forums mobile app
Umepaniki kumlaumu harakaharaka labda hukumuelewa. Anamaanisha siku alipodhulumiwa ilitakiwa asitukanane nao kwa sababu bado watu haohao akifuzu ndo ilitakiwa wamtayarishie hiyo ITC.

Ndo maana katolea mfano wa kuvunja daraja baada ya kuvuka ilihali unaweza kulihitaji baadaye. Kuna somo amenipa kwa ujumla.
 
Kingekuwa ni kitambulisho cha NIDA angekipata kwa nguvu!

Hiki ni kitu kinachotoka kwa hiari, kwa magumashi, ambacho Mwameja alitaka FAT wamchongee wamtumie, wakati washatukanana, wakampiga chini!

South Afrika hawakutaka mifarakano na FAT wala Simba, wamenunua mchezaji wakatuma hela FAT na ujumbe hii hela pelekeni Simba. FAT kabla ya kuwaambia tuna hela yenu mkononi wakakumbusha deni lao, Simba wakazingua, FAT wakakaza hukumu!

Mwameja kawatukana, kaondoka kibaharia. Yakamkuta mbele. Anakuja kulia leo.
Mwameja alikuwa kama mtoto at that mean time. Kwa nini mkamtreat kwa kumkomoa wakati nyie pale ni kama wazazi?

Pale mlipochukua dola 6000 alipanic lakini aliporudi kwa ajili ya ITC at least mngemsamehe kama wazazi na kutambua jitihada zake binafsi mkamsaidia.
 
" Mwaka 96 nikiwa South Africa kuna mdau wa Jomo Cosmos aliniona akanifuata hotelini kwangu akaniuliza kama Nina wakala nikamwambia sina.

Akaniambia Mimi Nina Shida ya Goal Keeper kwenye timu yangu Lakini Uingereza Kuna timu pia inahitaji kipa ( Reading FC wakiwa daraja la TATU ) Kwa hiyo ninafanya mpango baada ya wiki moja nitakutumia pesa uje South u sign Jomo Cosmos then nikupeleke Reading UK ukiwa kama mchezaji wa Jomo Cosmos.

Mwameja aliomba Dola elfu kumi Jamaa akawambia atamtumia Kwanza Dola elfu sita halafu dola.elfu nne itakayo Baki atapewa Akisha fika Sauz.

Hiyo dola.elfu sita ilitumwa kwangu kupitia Fat, Fat wakaizuia hiyo pesa wakisema wanaidai Simba Kwa hiyo wamekata Deni Lao.

Nili mind Sana suala Hilo na nilipishana kauli na Ndolanga na baadhi ya viongozi WA Simba ambao walionekana kusapoti ujinga Huo.

Nilienda Sauz kinyonge sana Kwa kulazimika kutafuta pesa yangu mwenyewe kumlipia tiketi ya ndege, nikifika Sauz nikiwa nimechelewa so Jamaa WA Jomo akasema inabidi niende Kwanza UK nikafanye training na Reading Kwa sababu walikua Wana nihitaji Kwa wakati Huo na nilikuwa nje ya muda..

Kufika UK nikafanya training na kweli nikafaulu so ikabaki kusign mkataba.

Reading walihitaji nipate kitu kinaitwa ITC ( International Training Certificate) kupiga simu Tz Ndolanga na Rage wakabana.

Nilikuwa stressed sana nikarudi bongo na kwenda Hadi office za Fat. Tulipishana maneno na Ndolanga, Rage akapiga simu polisi waje wanichukue Lakini polisi walivyo fika na kugundua NI Mimi na baada ya Mimi kuwaeleza chanzo cha Ndolanga kunifanyia fitna wali amua tumalizane wenyewe kwenye vikao vyetu

Rage aliwahi kuniita wakati Fulani akaniomba msamaha but Ndolanga sintoweza kumsamehe daima.

Nikisema nimemsamehe nitakuwa mnafiki. Siwezi kumsamehe Kwa sababu ameniharibia maisha.

# Mungu' ampe subra Kaka yetu Mohamed Mwameja.
Ndolanga na Rage nadhani pia walikuwa wachawi .
 
Training × = transfer✓

Sent using Jamii Forums mobile app

Transfer Certificate unasema wewe!

Ye mwenyewe kasema Training Certificate

Na hata kama ni Transfer Certificate, Mwameja alikuwa anatokea South Africa, anakwenda UK, FAT inahusika vipi na transfer yake?

Mwameja angekuwa kweli anatakiwa huko UK ni wenyewe English Premier League wangemwombea documents! Na kama ni haki yake zingekwenda!

Alitaka favor wakati keshatukanana na watu!
 
Back
Top Bottom