Mimi nina maswali ambayo ningemuuliza , ambayo haya maswali nahisi kama hakuwa na majibu mazuri, hakuna taahira yeyote angeweza kumuachia huru, hata kama hana hatia.
1) Kutoka Lugalo kwenda Manzese inabidi upite Mwenge kwanza ambako ni nyumbani kwake, kwanini hakuacha mizigo yake hapo Mwenge ndio aende Manzese akapate starehe?
2) Kwa akili za kawaida za kibinadamu, unaweza ukaacha begi la silaha za kijeshi na vitambulisho vyako juu ya meza ya bar na kwenda msalani bila kukabidhi hata kaunta? Ukizingatia bar wanaingia watu wa kila aina?
3) Muda wa kupoteza begi lake hadi ripoti ya ujambazi kufika polisi ilikuwa ni masaa mangapi? Yaani mtu ambae hajui ndani ya begi lako kuna nini aibe begi, awe anajua jinsi ya kutumia hiyo silaha, awe alishapanga tukio la ujambazi, maana tukio kama hilo hukurupuki tu, inatakiwa angalau siku 1 kabla uwe umepanga, aweze kutekeleza wizi na mauaji, polisi wafike wachukue ushahidi , hayo yote wamewezaje kutokea ndani ya muda mfupi hivyo? Halafu baadae wewe ndio unaenda kuripoti? How?