Mohamed Said ana siasa za kulialia

Mohamed Said ana siasa za kulialia

Kwa Wazanzibar ni afadhali kutunyonya kuliko kutuuwa kwani kila mtaa mumeweka kambi za kijeshi mnasubiri Uchaguzi mtutwange marisasi
Kwahiyo hapa nchini wanauwawa?
 
Yaani wazanzibari mtuuwe, mtuibie , mtuletee majeshi mpaka ya Burundi halafu tukae kimya kwa vile hatuna silaha za kujinginga na uvamizi wenu , TUAENDELEA KUSEMA WALIO NA MIOYO YA KIBINAADAMU WATAFAHAMU NA WALE WENYE MIOYO MIGUMU KAMA WEWE DAWA YENU IKO JIKONI
Mmeuliwa na Nani nyie wezi wa kulalamika mnatumia rasilimali zetu bure mnatuibia haki zetu...siku zenu zinahesabika hii sio tanganyika ya Mwalimu Nyerere majambazi nyie
 
Ishu ya wabunge wengi ni wakristo kwasababu ratio inaonyesha wakristo ni wengi zaidi Tanzania. Mikoa mingi majimbo mengi wanaishi wakristo ya waislamu ni mikoa ya pwani Kwa kiasi kanda ya Kati na kigoma kiasi chake. Ni ngumu kuona muislam ni mbunge wilaya za Mwanza , Njombe, katavi , Mbeya , Mara, Songwe , Arusha, Kilimanjaro, n.k. kwasababu wanaochagua hao wabunge ni watu waishio pale kwahiyo ishu ya wabunge uiache tuu. Population haijawahi kudanganya . Hao wabunge hawajichagui wenyewe wanachaguliwa.
Kwani walienda shule wakafukuzwa hao Waislamu?
Shuleni wanaandikishwa kwa dini?
Kiufupi ni waongo wanaotaka kuonewa huruma ili agenda Yao ya kunyonya watu wasio dini yao itamalaki vema
 
Lambo,
Hapana hali ilibaki kama ilivyokuwa kabla ya kutaifishwa.

Kuna utafiti ulifanywa na Warsha mwaka wa 1981 na matokeo yake kusambazwa kwa Waislam nchi nzima.

Hii ilileta matatizo makubwa sana.

Nina paper niliandika "Islam and Politics in Tanzania," (1989) na niliwasilisha kwenye mkutano Nairobi.

Hii paper iko kwenye journal sikumbuki jina la hii journal.
Ukitaka kujua yaliyotokea nifahamishe nikuwekee link.
Naomba hiyo link
 
Kitu kirahisi angalia ukubwa wa Tanzania na mikoa ipi ina waislamu wengi na wakristo wengi. Jibu utalipata
Yanini kubahatisha?
Mwakani si kuna sensa?
Tuhesabiane tu
Shughuli iishe, halafu baada ya hesabu walio wengi wawatawale wachache
 
Ukiona watu wanatumia muda wao kukujadili ujue kuwa wewe unathamani.
Ata kisicho na thamani hujadiliwa nd maana kuna muda watu hujadili dhahabu na kuna muda hujadili kokoto au mchanga,, na ndivyo ilivyo hata shetani, wezi nao hujadiliwa kwahiyo nao n wa thamani?
 
Mzee Muongo huyo ila bishi balaa.... TBC pale kuna tape za Nyerere za kitambo akiadithia kuhusu uhuru ulivyopatikana na watu walikuwa kwenye mikakati halisi yaani story kutoka kwa mhusika yeye anakuja na watu wake wengine wale waliokuwa wanakaa vijiweni kama sijui wazee wake au lah ndio anaowaita waislam waliokuwa kwenye kupigania uhuru??? sasa kama nchi ilikuwa na raia wake walikuweko kabla ya uhuru hata kama walikwa hawana ushawishi na siasa nao anawaita wapigania uhuru kisa tu walikuwa waislam. walichofanya hakuna, michango yao hakuna yeye anawapigania tu kisa nyumba zao nje zilikuwa vijiwe vya soga
 
Una uhakika ule msikiti alijenga JPM? OK turudi kwenye mada je waislam wanabaguliwa? Nikiwaza masuala ya UDOM na NSSF nabaki kimya
Hakuna anayewabagua, ni wao wenyewe wanajishtukia tu. Rais Samia kafuata utamaduni wa waliomtangulia. Kaweka waislam wengi tu serikalini lakini wakristo ni kama wanapuuzia tu.
 
Mzee Muongo huyo ila bishi balaa.... TBC pale kuna tape za Nyerere za kitambo akiadithia kuhusu uhuru ulivyopatikana na watu walikuwa kwenye mikakati halisi yaani story kutoka kwa mhusika yeye anakuja na watu wake wengine wale waliokuwa wanakaa vijiweni kama sijui wazee wake au lah ndio anaowaita waislam waliokuwa kwenye kupigania uhuru??? sasa kama nchi ilikuwa na raia wake walikuweko kabla ya uhuru hata kama walikwa hawana ushawishi na siasa nao anawaita wapigania uhuru kisa tu walikuwa waislam. walichofanya hakuna, michango yao hakuna yeye anawapigania tu kisa nyumba zao nje zilikuwa vijiwe vya soga
Mlaleo,
Ungeweza kusema hayo yote uliyosema kistaarabu bila ya kuonyesha utovu wa adabu na kuniita muongo.

Ungeweza ukasema mathalan, ''kuna tape TBC zinasema kadha wa kadha...''

Hapakuwa na haja ya matusi ''bishi balaa nk. nk.''

Hao unaowaita wakaa ''vijiweni,'' mimi ni baba zangu na najua walichofanya na nimeandika yote na yanafahamika na kitabu kinasomeshwa katika vyuo vikuu Ulaya, Marekani na kwengineko na vyuo hivi wamenialika kuzungumza.

Soma hapa chini Mwalimu Nyerere anasema nini kuhusu wazee wangu:

"Mimi nimeanza siasa na wazee wa Dar es Salaam; na wazee wa Tanzania.

Nimeanza nao mapema sana; mapema kweli.

Nilirudi kutoka masomoni, Uingereza Oktoba 1952 – miaka 33 nyuma.

Wakati huo nikiwa kijana mdogo wa miaka thelathini na kidogo hivi.

Niliporudi nikakubaliana na wamisionari hapo Pugu (sekondari), nifundishe shuleni kwao. Lakini nikiwa shuleni – Chuo Kikuu – nilijua.

Niliishaamua kwamba maisha yangu yatakuwa ya siasa. Niliamua hivyo: Nitafundisha kwa muda wa miaka mitatu, nione hali inavyokwenda na kuzoeana na wenzangu kabla ya kuanza maisha ya siasa.

Niliporejea nchini hapo Oktoba, nikaenda Butiama. Januari nikarudi Dar es Salaam. Nikaanza kazi.

Nikataka kujua habari za African Association.

Mzee Mwangosi anakumbuka.

Yeye ndiye aliniambia habari za African Association. Aliisha niambia habari hizo tangu nikiwa Makerere – Chuo Kikuu – nikiwa mwanafunzi.

Pale, mimi na wanafunzi wenzangu tulikuwa tumeanzisha chama kinachoitwa Tanganyika African Welfare Association (TAWA) cha wanafunzi wa Tanganyika; mimi nikiwa katibu wao.

Hapa tukaona mambo yanakwenda vizuri kidogo.

Tukaona kwanini TAWA iwe ya wanafunzi peke yao na siyo Tanganyika nzima.

Kwa hiyo nikawaandikia baadhi ya watu Tanganyika.

Nikasema, jamani ee, tumeanzisha chama, kwanini msianzishe huko matawi ya chama hicho?

Ndugu Mwangosi akapata barua hiyo.

Alikuwa miongoni mwa waliopata barua hiyo.

Akaniandikia – nikiwa Makerere – akasema: wewe kwanini unataka kuanzisha chama kipya?

Kipo chama.

Kipo chama cha TAA (Tanganyika African Association).

Kwa hiyo la maana siyo kuanzisha matawi, maana chama kipo na matawi yameenea; la maana ni kwamba hicho chama chenu mfute, na muanzishe tawi la Tanganyika African Association.

Hivyo ndivyo tulivyofanya.

Kwa hiyo mimi nikawa katibu wa katawi ka TAA hapo Makerere.

Niliporudi Tabora na kuanza kufundisha pale St. Marys (sasa inaitwa Sekondari ya Milambo), nikachaguliwa katibu wa TAA wa jimbo ambalo makao yake makuu yalikuwa Tabora.

Ulipofanyika mkutano wa TAA mjini Dar es Salaam, nilihudhuria nikiwa mjumbe kutoka Tabora.

Kwa hiyo nilikuwa naijua Tanganyika African Association.

Nilipokuwa ninaondoka kwenda Ulaya kusoma, nilikuwa nimeishaonja shughuli za TAA.

Sasa niliporudi, baada ya kukaa Pugu siku chache, nikaja mjini Dar es Salaam.

Nikauliza nani wanaongoza TAA?Nikaambiwa kuna jamaa mmoja anaitwa Abdul Sykes.
Sasa ni marehemu.

Abdul ndiye alikuwa katibu wakati huo.

Nilipelekwa na Kasela Bantu - ambaye naye aliteleza-teleza na hatunaye hapa (kwenye mkutano).

Kasela Bantu alikuwa mwalimu mwenzangu.

Tulifundisha pamoja Milambo.

Nilipokuja Dar es Salaam, nikakuta anafanya kazi Redio (Tanganyika Broadcasting Corporation). Ni Kasela Bantu aliyenipeleka kwa Sykes.

Wakati huo mambo yalikuwa yanasinzia kidogo.

Kwa muda mfupi mwaka ule, tukafufua-fufua, hasa kutoka Januari.

Kufika Aprili, TAA ikafufuka.

Tukafanya mkutano hapo Anautouglou.

Kwenye mkutano huu wakanichagua kuwa Rais wao – wa TAA.

Ninasema yote haya kwa shukrani kwa wazee.

Jamaa hawa walikuwa watu wazima wa Dar es Salaam, na mimi kijana mdogo Mzanaki, na Kiswahili changu si kizuri sana – cha matatizo.

Nimekuja, natoka Ulaya, tena masomoni.

Muda mfupi tu jamaa hawa wakaniamini haraka sana – katika muda wa miezi mitatu.

Wakanichagua Rais wa TAA.

Hapo ndipo nilianza shughuli mpya ya kuandika katiba ya TAA na kuipa madhumuni hasa ya shabaha ya kuleta uhuru.

Baada ya miezi 13, hapo 1954, tukaanzisha TANU.

Jina hili lilipendekezwa na akina Abdul Sykes.

Walikuwa wamelifikiria tangu zamani, walipokuwa askari vitani huko Burma (Vita vya Pili).

Miezi minne baada ya kuanza kazi Pugu nikawa ninakuja Dar es Salaam, kwa mguu; kila Jumamosi.

Baadaye wazee wakanipa baiskeli nikawa ninakuja mjini kukutana na wenzangu; kufanya mikutano.

Hivyo ndivyo tulivyofanya. Wazee wakaniamini upesi sana.

Tukawa na uhusiano mkubwa sana.

Wadogo wenzangu wengine walikuwa Abdul Sykes, Abass Sykes (mdogo wake), Dosa Aziz – waliokuwa wengi ni wazee.

Katika kuhutubia mikutano yangu, nilikuwa nikisema: Wazee na Ndugu zangu! Wazee hasa ndio walikuwa na mikutano ya awali ya TAA na TANU.

Walikuwa na msimamo wa hali ya juu kabisa!

Hawakuyumba hata kidogo! Vijana walikuwa na mashaka.

walikuwa na vikazi vyao, waliogopa kuvipoteza.

Nalo jambo lenyewe ni la hatari – la kuzungumzia uhuru!

Unaweza ukakosa kazi; na wapo waliopoteza kazi; wengine wakaacha kazi.

Akina Rashid (Kawawa) waliona watoke kwenye shughuli hizo tuje tuungane katika chama.

Wazee wa Dar es Salaam, na baadaye wa nchi nzima, wakatuunga mkono, na kila nilipokwenda, watu wa kwanza walionielewa, walikuwa wazee.

Nilikwenda Songea mwaka 1955 mara baada ya kujiuzulu.

Huko wazee walinipokea na kunielewa.

Nilianza safari za kuitembelea Tanganyika nzima.

Nilikwenda Mbeya.

Mkutano wangu niliufanya na wazee; kikundi kidogo cha wazee, ndani ya nyumba ya mtu.

Kwa mkutano huu wa Mbeya, wazee wakauliza: Unatafuta nini?
Nikawaambia natafuta uhuru.

Wale wazee, kwa sababu ya vita vya Maji Maji, na wanakumbuka, kabisa, wakaona mimi ninatafuta jambo la hatari.

Tulifanya mkutano wa makini kweli. Wakauliza: Wewe unawezaje kuleta uhuru?

Wewe una njia gani kudai uhuru na usitiwe kitanzi na Waingereza?

Tulielezana.

Nikawaambia ninyi wazee, Waingereza wanawadanganya, Waingereza wametumwa na ule Umoja wa Mataifa uliokufa (League of Nations), waje kuishika Tanganyika kwa muda tu; watusaidie, na wakati tutakapokuwa tayari, watuachie tukajitawale.

Waingereza wanafanya ujanja; hawasemi.

Vita vimekwisha (vya Pili) na Umoja wa Mataifa mwingine – mpya (United Nations Organisation – UNO) umewakabidhi Tanganyika kwa shabaha ileile.

Sisi siyo koloni lao.
Wamepewa dhamana tu.

Kwa hiyo nikawaambia wazee, hakuna haja ya kumwaga damu.

Tuwaseme tu!

Tuwashitaki kwa waliowaleta hapa kwamba hawafanyi kazi yao; wamesahau kabisa!

Wazee wakauliza: Eh, inawezekana?
Nikasema inawezekana.

Kazi yetu ya kwanza ilikuwa kuwaambia watu kwamba uwezekano wa kujitawala upo.

Hilo lilikuwa la kwanza. Wazee walijua maana ya kujitawala.

Walitamani kujitawala, lakini hawakujua waanzie wapi.

Vijana hawakuwa na habari kwamba kujitawala kunawezekana. Kwa hiyo kwa wazee sikuwa na matatizo.

Wao hawakuwa na kazi; hawakumwogopa Mwingereza.
Hawakuogopa kufukuzwa kazi.

Baadhi walikuwa wafanyabiashara.

Mzee John Rupia (marehemu) alikua mfanyabiashara na kaidi kidogo.

Aliwahi kutishwa na kunyang’anywa leseni yake ya biashara.

Akaambiwa akiendelea kushirikiana na kijana mwenda wazimu (Julius Nyerere), atanyang’anywa leseni moja kwa moja.

Rupia aliwajibu: Potelea mbali!

Nasema yote haya ikiwa njia ya kutoa shukrani kwa wazee na imani yao kwa vijana wakati huo.
Imani hujenga imani.

Na mambo haya makubwa ya nchi, kama hayana baraka za wazee hayaendi.

Magumu sana.

Wanasema ngoma ya watoto haikeshi!

Mimi nilipata baraka za wazee tangu zamani.

Tangu awali kabisa.

Siku moja, Dossa akanifuata Magomeni (Dar es Salaam).
Akasema: Leo wazee wanakutaka.

Wapi?
Kwa Mzee Jumbe Tambaza.

Wanakutaka usiku.
Nikasema haya, nitakuja.

Nikaenda.

Nikakuta wazee wameshakaa; wameniita kijana wao kuniombea dua.

Mimi Mkristo, wao Waislamu watupu.

Wakaniombea dua za ubani.
Tukamaliza.

Tulipomaliza wakasema kuna dua pia za wazee wao.

Basi wakanitoa nje.
Tukatoka.

Zilipomalizika zilikuwa za Korani; sasa zikaja dua za wazee – za jadi.

Walikuwa na beberu la mbuzi. Wamechimba shimo.

Wakaniambia simama.

Nikasimama.

Beberu akachinjwa, huku anaambiwa, “Twining (Twainingi) umekwisha!”

(Edward Twining alikuwa Gavana wakati huo).

Ndipo nikaambiwa: Tambuka!

Nikavuka lile shimo.

Hapo nikaambiwa na wazee: Basi nenda zako; tangu leo Twainingi amekwisha!

Sasa mimi Mkristo; hao Waislamu.
Na mimi mkorofi-korofi katika mambo haya (ya kutambika).

Lakini tulikuwa tunaelewana na wazee wangu hao.

Kwa hiyo nilitambuka pale na kuambiwa: Nenda nyumbani salama.

Twaining hawezi tena!
Wazee wangu wengine wanakumbuka tulikuwa tunakwenda Bagamoyo.

Kwenye makaburi kule!

Tunapiga dua huko kwenye makaburi na wazee wangu.

Baadhi yetu mtakumbuka safari moja jamaa wa Kenya, hawa akina Tom Mboya (marehemu) walishitakiwa.

Tukasema tuwasaidie.
Tuwasaidie vipi?

Tukasema tufunge.

Tukaomba nchi nzima kufunga siku hiyo.

Tufunge!
Tukafunga.

Hakuna kula.

Na siku ya kufunga tulikuwa na mkutano Bagamoyo.

Tukaenda huko.

Tukafanya mkutano hadi saa 12 jioni.

Baada ya mkutano tukaenda nyumbani kwa Mzee Mohamed Ramia (marehemu).

Hapa ndipo tulikuwa tumefikia.

Mimi nikamuuliza mzee: Sheikh, una Aspro?

Akajibu: Kwa nini unataka Aspro?

Nikajibu kuwa kichwa kinaniuma kwelikweli.

Akasema subiri.

Tulisubiri hadi saa ya kufuturu.
Tukafuturu vizuri.

Mzee Ramia akaniuliza: bado unataka Aspro?

Nikajibu kichwa sasa hakiumi.
Kumbe ilikuwa njaa.

Nawaelezeni haya kwa sababu huko tulikotoka, tulishikamana sana.

Tulishirikiana sana na wazee.''

Mlaleo,
Huyo ndiye Mwalimu Nyerere anavyowahadithia wazee wangu.

Waswahili tuna msemo, ''Akutukanae hakuchagulii tusi.''

1639682175089.png

Kulia Nangwanda Lawi Sijaona, Abdulwahid Kleist Sykes, Julius Kambarage Nyerere na Waziri Dossa Aziz hafla ya kumuaga Nyerere Ukumbi wa Arnautoglo safari ya pili UNO 1957.
 
Hakuna anayewabagua, ni wao wenyewe wanajishtukia tu. Rais Samia kafuata utamaduni wa waliomtangulia. Kaweka waislam wengi tu serikalini lakini wakristo ni kama wanapuuzia tu.
Thubutu! Vita vyenu ni kimya kimya. Mbona hamkuinyamazia NSSF ya Dau na UDOM ya Kikula?
 
Mmeuliwa na Nani nyie wezi wa kulalamika mnatumia rasilimali zetu bure mnatuibia haki zetu...siku zenu zinahesabika hii sio tanganyika ya Mwalimu Nyerere majambazi nyie

Msikilize babu yako Laanatullahi Nyerere

 
Back
Top Bottom