Mohamed Said ana siasa za kulialia

Mohamed Said ana siasa za kulialia

Agenda yenu ya kulalamika ili muonekane mnaonewa na kuendelea kuiba rasilimali za nchi imeshafahamika.
Nssf mligeuza Msikiti,Udom mkataka geuza madina

Ndivyo ulivyoambiwa Na mchungaji wako?
Jibu swali please
 
Dira ...
Nimekujibu kwa kuwa umenitaja.
Ungenipuuza ungekuwa kimya mimi nisingekujibu.

Aliye pembeni haangukiwi na mnazi.
Umeusogelea mnazi ndiyo maana umekuangukia.
Wewe Mzee ni kweli ni msomi na una exposure ya kutosha ila elewa kwamba wewe ni reflection ya wazee wako wa Kariakoo. Jinsi ulivyojaa udini na malalamiko ni wazi kwamba wazee wako wa Kariakoo nao ni kama wewe ndo maana Mwalimu Nyerere akaona ni upumbavu kuwachekea watu kama hawa. Maandishi yako yanatupa majibu kwanini baba wa Taifa aliamua wazee wa Kariakoo wasizungumziwe. Sasa kama wewe msomi wa Chuo Kikuu una mawazo mgando kiasi hiki vipi hao wazee waliokuwa na elimu ndogo? Cha muhimu kwa sasa Mzee uza bitabu vyako ila jua kabisa serikali timamu ya CCM haina nafasi ya udini na mawazo potofu kama yako.
 
Kusema hawataki au hawakusoma huo ni uongo na propaganda zilizopitwa na wakati, ila kwa sasa
Jikite kwenye mada,
wapi wengi?
Hapo mada ni idadi ya upande fulani walio wengi ndio watawale walio wachache, sasa utawala hauwezi kuhusisha idadi peke yake ila maarifa na elimu na ndio maana hata wazungu walikuwa wanakuja wawili tu wanasomba babu zetu 100+.

Unapo zungumzia utawala huwezi kutenganisha na elimu
 
Ubaguzi uliopo bongo ni wa kisiasa tu. Upo waziwazi, Ila ubaguzi wa kidini haupo.
Ukiongoza nchi kwa kuwa unaangalia dini, utakuwa na ugumu sana wa kujenga nchi yenye dini nyingi kama Tanzania. Mohammed Saidi ana tatizo kubwa na Nyerere (mkristo) kwa vile aling'ara sana katika siasa za nchi hii kuliko akina Sykes (Waislamu). Kwa Mohammed, kila kitu kingekuwa sawa kabisa iwapo muislamu mmojawapo ndiye angekuwa rais, halafu Nyerere awe msaidizi tu. Pamoja na kuwa wasaidizi wakubwa wa Nyerere walikuwa ni waislamu, yeye hakuwahi kutosheka na hilo la Nyerere kuwa kiongozi juu ya waislamu. Hata hajawahi kukubali kuwa Nyerere alikuwa amesoma sana kuliko hao waislamu anaowazungumzia kila siku na wao wenyewe walimkubali kama kiongozi wao.
 
Nimesoma mwanzo hadi mwisho wa uzi huu. Haya nimebaini.

● Mzee Mohamed Said ni msomi mzuri na mtafiti juu ya historia ya waislamu katika kupigania uhuru wa Tanzania ambaye anasukumwa zaidi na uislamu wake katika kuchambua mambo kuliko uhalisia wake.

● Wasomaji wengi bila kujali imani zao wanapenda simulizi za mwandishi huyu ila hawaridhishwi na dhamira inayomuongoza mwandishi huyu katika makala zake.

● Mwandishi huyu ni mjanja wa kukwepa kujibu hoja ama maswali anayoulizwa ambayo kimsingi yanahitaji majibu mafupi ili kuleta mtiririko mzuri wa majadiliano, kinyume chake amekuwa akijibu hoja kwa ama kuweka links za machapisho yake ama makalu alizoziandika huko nyuma na hivyo majibu yake kuwa vague na kutokueleweka kwa wasomaji.

● Baadhi ya wachangia mada wanachangia kwa kufata mkumbo tu wa imani zao. Hata pale ambapo anaamini kabisa dini au imani yake imepelekea uwepo wa tatizo flani hata kubali bali atasapoti ti kwa sababu lina favour imani yake.

● Mzee Mohamed Said kupitia nakala zake amejitanabaisha kama mtu anayeutezwa utengano dhidi ya jamii iliyoungana. Kuna jambo analitaka juu ya utengano lakini ni muoga wa kulisema kinagaubaga hivyo kutumia maandishi yake kufikisha ujumbe kwa njiamficho!

● Mohamed Said ni tunu na hazina kwa taifa letu iwapo tu asingesukumwa na udini katika uandishi wake. Laiti kama angekuwa anaandika makala hizi za historia kama mtu HURU asiye na athiriwa na religious myopic disease hakuna nguli wala mwanahistoria katika nchi hii angefikia uwezo wake.

● Wachangiaji wengi pasi kujali imani zao HAWAFURAHISHWI na mijadala ya kidini inayolenga kuwagawa Watanzania. Wengi wanatamani kusoma namna gani historia ya nchi yetu ilivyo na kama iliandikwa isivyo irekebishwe lakini katika namna inayoweza kuwaunganisha watanzania wote na sio kuwabagua kwa misingi yeyote ile.

● Mwisho katika uzi huu nimegundua kwamba Mzee mwenzangu Mohamed (Kaka yangu Mkubwa) ni mtu Mstaarabu sana, si mtu wa jazba na mshika dini mno. Na katika maandishi yake anatamani watu wengi ama wasome maandishi yake kwa kujifunza ama kuamsha are ya "uislam tunaonewa" miongoni mwa wasomaji wake.
 
Nilikuwa nasikiliza kipindi cha maoni kinachorushwa na DW, ndipo nikamsikia huyu mtu anaitwa Mohamed Said akitoa maoni yake kuhusu miaka 60 ya uhuru, ingawa kabla nimewahi kusoma makala zake kadhaa, sikufikiri kwamba kwa ukubwa wa changamoto tulizonazo leo pamoja na mabadiliko makubwa ya kielimu na kimfumo bado atakuwa na mawazo kwamba waisilam wanabaguliwa.

Ninapata shida kumwelewa kwa sababu kwa taifa letu lilipofikia ningeweza kusema kama ni ubaguzi unaopaswa kupambana nao ni ule unaopendelea chama tawala.

Ubaguzi anaosema waisilam wanabaguliwa ni wa kufikirika sana. Sijui kama huyu ndugu amefanya utafiti kujua wakristo na waisilam wanaosota na kubaguliwa kwa sababu wao sio CCM!!.

Akiwa anasema hayo wapo viongozi wa kiisilam wengi tu wanaoshiriki uharamia wa kuwabagua ndugu zao ilimradi tu sio CCM.

Nashauri aache mambo ya kukaririshwa kwamba waisilam wanaonewa hizo hoja zilishapitwa na wakati. Isitosha zinafanya waisilam waonekane wanyonge na watu wa kuhurumiwahurumiwa tu.

Wewe Mzee ni kweli ni msomi na una exposure ya kutosha ila elewa kwamba wewe ni reflection ya wazee wako wa Kariakoo. Jinsi ulivyojaa udini na malalamiko ni wazi kwamba wazee wako wa Kariakoo nao ni kama wewe ndo maana Mwalimu Nyerere akaona ni upumbavu kuwachekea watu kama hawa. Maandishi yako yanatupa majibu kwanini baba wa Taifa aliamua wazee wa Kariakoo wasizungumziwe. Sasa kama wewe msomi wa Chuo Kikuu una mawazo mgando kiasi hiki vipi hao wazee waliokuwa na elimu ndogo? Cha muhimu kwa sasa Mzee uza bitabu vyako ila jua kabisa serikali timamu ya CCM haina nafasi ya udini na mawazo potofu kama yako.
Dira...
Unaandika umeghadhibika na hamaki zinapunguza uwezo wa kuwaza na kuandika maneno yenye busara.

Unaligeuza jambo zito la dhulma kuwa kejeli kwangu na kwa wazee wangu.

Lakini baya zaidi unazungumza historia usiyoijua kwa kusema kuwa Mwalimu Nyerere aliamua kufuta historia ya wazee wangu kwa kuwa walikuwa watu wabaya.

Unasema wazee wangu walikuwa na elimu ndogo nk.nk.

Labda nikufahamishe historia ya wazee wangu na kiwango chao cha elimu na nitakutajia wachache.

Katika TAA Political Subcommitee kulikuwa na Sheikh Hassan bin Ameir elimu yake ilikuwa kubwa sana na ndiyo alikuwa Mufti wa Tanganyika.

Sheikh Said Chaurembo alikuwa hakimu.

Hawa ni masheikh wakati ule walikuwa watu wazima.
Itapendeza kama utajifunza kwanza somo unalotaka kuchangia kabla ya kuandika.

Ninachouliza ni inakuwaje watu wa imani moja wanahodhi 80% ya serikali miaka 60 baada ya uhuru?

Labda hujui maana ya udini.
Udini tafsiri yake ni kukandamiza jamii moja na kuinua jamii yako kwa misingi ya imani.

Hiyo CCM unayoitaja asili yake ni TAA na TAA iliundwa na wazee wetu.
Kwa hakika hili tatizo wao wanalijua na ipo siku litazungumzwa.

Mimi sifanyi kazi ya kuuza vitabu wala siandiki kwa kutafuta fedha au umaarufu.

1639713185826.png
 
Nimesoma mwanzo hadi mwisho wa uzi huu. Haya nimebaini.

● Mzee Mohamed Said ni msomi mzuri na mtafiti juu ya historia ya waislamu katika kupigania uhuru wa Tanzania ambaye anasukumwa zaidi na uislamu wake katika kuchambua mambo kuliko uhalisia wake.

● Wasomaji wengi bila kujali imani zao wanapenda simulizi za mwandishi huyu ila hawaridhishwi na dhamira inayomuongoza mwandishi huyu katika makala zake.

● Mwandishi huyu ni mjanja wa kukwepa kujibu hoja ama maswali anayoulizwa ambayo kimsingi yanahitaji majibu mafupi ili kuleta mtiririko mzuri wa majadiliano, kinyume chake amekuwa akijibu hoja kwa ama kuweka links za machapisho yake ama makalu alizoziandika huko nyuma na hivyo majibu yake kuwa vague na kutokueleweka kwa wasomaji.

● Baadhi ya wachangia mada wanachangia kwa kufata mkumbo tu wa imani zao. Hata pale ambapo anaamini kabisa dini au imani yake imepelekea uwepo wa tatizo flani hata kubali bali atasapoti ti kwa sababu lina favour imani yake.

● Mzee Mohamed Said kupitia nakala zake amejitanabaisha kama mtu anayeutezwa utengano dhidi ya jamii iliyoungana. Kuna jambo analitaka juu ya utengano lakini ni muoga wa kulisema kinagaubaga hivyo kutumia maandishi yake kufikisha ujumbe kwa njiamficho!

● Mohamed Said ni tunu na hazina kwa taifa letu iwapo tu asingesukumwa na udini katika uandishi wake. Laiti kama angekuwa anaandika makala hizi za historia kama mtu HURU asiye na athiriwa na religious myopic disease hakuna nguli wala mwanahistoria katika nchi hii angefikia uwezo wake.

● Wachangiaji wengi pasi kujali imani zao HAWAFURAHISHWI na mijadala ya kidini inayolenga kuwagawa Watanzania. Wengi wanatamani kusoma namna gani historia ya nchi yetu ilivyo na kama iliandikwa isivyo irekebishwe lakini katika namna inayoweza kuwaunganisha watanzania wote na sio kuwabagua kwa misingi yeyote ile.

● Mwisho katika uzi huu nimegundua kwamba Mzee mwenzangu Mohamed (Kaka yangu Mkubwa) ni mtu Mstaarabu sana, si mtu wa jazba na mshika dini mno. Na katika maandishi yake anatamani watu wengi ama wasome maandishi yake kwa kujifunza ama kuamsha are ya "uislam tunaonewa" miongoni mwa wasomaji wake.
Mhad...
Ahsante kwa mchango wako.

Huna lolote la kuzungumza kwa hili la 20:80 miaka 60 baada ya uhuru?
 
Ukiongoza nchi kwa kuwa unaangalia dini, utakuwa na ugumu sana wa kujenga nchi yenye dini nyingi kama Tanzania. Mohammed Saidi ana tatizo kubwa na Nyerere (mkristo) kwa vile aling'ara sana katika siasa za nchi hii kuliko akina Sykes (Waislamu). Kwa Mohammed, kila kitu kingekuwa sawa kabisa iwapo muislamu mmojawapo ndiye angekuwa rais, halafu Nyerere awe msaidizi tu. Pamoja na kuwa wasaidizi wakubwa wa Nyerere walikuwa ni waislamu, yeye hakuwahi kutosheka na hilo la Nyerere kuwa kiongozi juu ya waislamu. Hata hajawahi kukubali kuwa Nyerere alikuwa amesoma sana kuliko hao waislamu anaowazungumzia kila siku na wao wenyewe walimkubali kama kiongozi wao.
Kichuguu,
Siwezi kuwa mjinga wa kiwango hicho unachonibebesha.

Dini ni muhimu katika utawala wa nchi yeyote ile.

Hii hali ya 20:80 miaka 60 baada ya uhuru kuwa waumini wa dini fulani ndiyo wanahodhi serikali ndilo tatizo.

Kutegemea watu wasiulize ni jambo lisilowezekana.
 
Hapo mada ni idadi ya upande fulani walio wengi ndio watawale walio wachache, sasa utawala hauwezi kuhusisha idadi peke yake ila maarifa na elimu na ndio maana hata wazungu walikuwa wanakuja wawili tu wanasomba babu zetu 100+.

Unapo zungumzia utawala huwezi kutenganisha na elimu
Mashine...
Katika hali kama hiyo ikiwa walioshika madaraka wanahujumu wengine wasipate elimu nini fikra yako?

Inawezekana hujui lakini ujenzi wa Chuo Kikuu kiichokuwa kinajengwa na EAMWS kilihujumiwa na ikavunjwa.

Hii ilikuwa 1968.
Nimeandika historia nzima ya mkasa huu, ''Islam and Politics in Tanzania,'' (1989).

Organisation of Africa Conference (OIC) walitaka kujenga Chuo Kikuu Tanzania serikali ikakataa kutoka kibali chuo hicho kikaenda kujengwa Mbale, Uganda.

Hii katika 1970s.

Nadhani unajua kuwa 2012 Waislam walifanya maandaman dhidi ya NECTA kwa kuituhumu kuhujumu shule za Kiislam.

Haya yote nimetafiti kwa kina na nimeandika.
Yapo mengi mengi sana na serikali yetu inataarifa zetu zote kwani hatunong'oni.

Unaona naandika hapa na jina langu naliweka ni kiasi cha mimi kuambiwa ni mzushi nasema uongo.

Lakini wahusika wanajua kuwa mimi si mpuuzi ni mjuzi na ninajua kweli ya hili tatizo.
Mimi naamini serikali iko siku itazungumza.
 
huyu mzee naona kuna kitu kama kisaikolojia kuna tatizo kabisa ?.
sawa na mtu aliyepotea au kutaka kulazimisha jambo ambalo si kweli .

ukiulizwa maswali jibu kwa nini unakuwa hivi!

majibu yako yote kama naona yanaishia wilaya ya ilala katika historia yako
 
Chiz...
Najibu maswali labda tatizo hupendi namna ninavyojibu.

Na kama kuna swali limenipita sijajibu tafadhali liulize.

Unajua unapoandika, ''Huyu mzee,'' ni kuwa umeghadhibika.

Sisi kwetu mtu akishakuwa mzee kama mimi anaheshimika huwezi kumwita ''We mzee,'' au ukasema, ''Huyu mzee.''

Kijana aliyefunzwa adabu angeniita mimi kama hivi, ''Mzee Mohamed kadha wa kadha...'' au, ''Mzee kadha wa kadha,'' ''Si huyu mzee.''

Mimi nakupima kwa mizani hii na nakuweka unapostahili.

Kuhusu Ilala kwani hairuhusiwi kuandika habari za Ilala?

Mjadala huu umependwa sana sasa tuko 6889 and counting.

Tusiuharibu kwa kejeli, kuvunjiana heshima na kukosa adabu.

Tujadiliane kiungwana.

Nina mengi ambayo wengi wenu hamjapata kuyasikia na ndiyo haya yanayovutia wasomaji.
 
Wewe Mzee ni kweli ni msomi na una exposure ya kutosha ila elewa kwamba wewe ni reflection ya wazee wako wa Kariakoo. Jinsi ulivyojaa udini na malalamiko ni wazi kwamba wazee wako wa Kariakoo nao ni kama wewe ndo maana Mwalimu Nyerere akaona ni upumbavu kuwachekea watu kama hawa. Maandishi yako yanatupa majibu kwanini baba wa Taifa aliamua wazee wa Kariakoo wasizungumziwe. Sasa kama wewe msomi wa Chuo Kikuu una mawazo mgando kiasi hiki vipi hao wazee waliokuwa na elimu ndogo? Cha muhimu kwa sasa Mzee uza bitabu vyako ila jua kabisa serikali timamu ya CCM haina nafasi ya udini na mawazo potofu kama yako.
Kwani udini ni nini?
 
Chiz...
Najibu maswali labda tatizo hupendi namna ninavyojibu.
Na kama kuna swali limenipita sijajibu tafadhali liulize.

Unajua unapoandika, ''Huyu mzee,'' ni kuwa umeghadhibika.

Sisi kwetu mtu akishakuwa mzee kama mimi huwezi kumwita ''We mzee,'' au ukasema, ''Huyu mzee.''

Kijana aliyefunzwa adabu angeniita mimi kama hivi, ''Mzee Mohamed kadha wa kadha...'' au, ''Mzee kadha wa kadha,'' ''Si huyu mzee.''

Mimi nakupima kwa mizani hii na nakuweka unapostahili.

Kwani udini ni nini?
Kitendo cha upendeloleo wa fursa kwa wafuasi wa imani yako dhidi ya wengine.
 
Mkuu hataa masimuliizi ya Nyerere alichokuwa anafanyiwa kule Bagamoyo na WazeewaKiaaslam' (kama anavyotaka Mzeee Mohamed Siadtuwatambue) yalikiwa no matambiko ya Dini Asili!
Anadai Nyerere alitafsiri vibaya Dua, akafananisha na Tambiko Asilia.

Ni kuukimbia tu ukweli, lakini yote tunajua chanzo in Ukoloni wa Fikra. Kwamba hata Tambiko zetu zinavishwa majina ya kigeni ili kupata uhalali.

Wazee wake hawakuwa huru kuishi Asili yao, wakaifanya kwa Kificho kuhofu Uislamu ama Ukristu wao.

Uhuru auishii kupandisha Bendera tu, ni hasa Uchumi na Tamaduni zenu.

Harakati za kudai Uhuru huo haukuanza na ujio wa Mjerumani au Mwingereza tu, ni Tangu Ustaarabu wa kigeni wa kwanza kuingia EA, wapo waliopinga. Ajabu, Mzee wetu hataki kujua nini kiliwakuta.

Mzee Mohamed Said , wazee wako licha Uislamu wao hawakuacha Tambiko Asilia, Si kwa bahati mbaya ila ni kwa kujua hasa Nguvu ya Asili hiyo.
Kinachotuumiza wengi Leo ni Aibu/Usiri wa Kuishi Kweli ya wazee wetu kwa hofu ya Uislamu au Ukristu, ati wameita Shiriki.

Uhuru tunaoutaka ni Wakuishi Maisha yetu katikavUkamilifu wake, so kwa kificho. Hivyo Tambua kuwa bado Unapigania kuhalalisha Ubatili katika Ubatili.

Amka!
 
Hapo mada ni idadi ya upande fulani walio wengi ndio watawale walio wachache, sasa utawala hauwezi kuhusisha idadi peke yake ila maarifa na elimu na ndio maana hata wazungu walikuwa wanakuja wawili tu wanasomba babu zetu 100+.

Unapo zungumzia utawala huwezi kutenganisha na elimu
Nje ya mada
 
Phy...
Tunaweza hapa tukafanya mjadala wa adabu na heshima na jamii ikanufaika na hoja.
Bahati mbaya umeanza mjadala na lugha za kejeli.

Umekuja na neno, ''kulialia.''

Ikiwa unataka kujadili na mimi njoo za lugha za kiungwana kwani inawezekama kabisa ukasema hayo uliyosema katika njia ya staha na kuheshimi
Naomba nikutake radhi kwa lugha iliyokukwaza hata hivyo nashukuru kwamba umekuja na kueleza mengi sana nashukuru kwa hilo hata hivyo

Niliona nitulie kwanza ili nipate
utetezi wako, lakini kwa bahati mbaya, kwa kadri unavyozidi kujieleza ni kama unazidi kuniongezea mashaka ya hii misimamo yako.

Mosi, maelezo na machapisho yako mengi yanalenga kututazamisha kwamba jamii ya waisilam nchini tanzania ni dhalili wanyonge duni na watu ambao hawana la kujivunia kwa maneno mengine ni kama unasema ni watu hohe hahe!!.

Kwa maoni yangu huku ni kuudhalilisha umma wa mtume. Waisilam wa Tanzania wa leo hawastahili hiyo status, kwani wanayo mengi ya kujivunia katika taifa lao.

Pili, Facts na tafiti nyingi unazozitumia kujenga hoja zako zimepitwa na wakati, kuna mengi sana yamebadilika kiasi kwamba ili utuaminishe kwamba haya mambo yapo lazima utumie nguvu nyingi sana! Maana kwa namna unayoeleza mtu asiyejua chochote kuhusu tanzania anaweza kudhani waisilam hawapo wala hawahitajiki au wamepigwa marufuku kupata nafasi serikalini. Ninachojua mimi ni kwamba tumekuwa na ushindani mkubwa wa ajira kwa kiwango ambacho kuna miaka katika baadhi ya sekta upatikanaji wa ajira uliamriwa na rushwa, ukabila, kujuana/refa, ukanda, uchama nk.

Kwa maoni yangu kuliko kuwahamisha watu kwamba waisilam wanabaguliwa ni heri ukamulika upya aina za ubaguzi zinazolitesa taifa.

Tatu, sijajua kigezo unachotumia kujua dini ya mtu unapoweka uwiano wa kidini wa idadi ya watu walioajiriwa na kuteuliwa serikalini. Naomba leo unisaidie, nijuavyo mimi kwa Tanzania ni jambo gumu kudertamine dini ya mtu, maana dini sio kama kabila ukizaliwa mndengeleko we ni mndengeleko tu hakuna namna itatokea ubadili kabila. Mtu anaweza akatumia jina la Ashura, Ramadhan Khadija Mfaume, Mohamed na asiwe muisilam, lakini pia mtu anaweza akaitwa Petro, Joni ,Salome ,Julius na akawa sio mkristo.
Labda kama mwenzetu umejaliwa kama mitume kutambua dini za watu unithibitishie hapa!
Mbali ya hilo kama nilivoeleza kwenye mazingira ya changamoto za ajira, kuna mtu kaingia kazini ni kweli jina ni Zahra ila Katoa rushwa ya ngono ndo kaajiriwa huyu naye utajivunia!?

Nne, ni uhalisia wa taasisi za kielimu ambayo ndiyo huandaa watumishi wa kada zote katika taifa letu. Kuna pengo kubwa sana la umiliki wa taasisi za kielimu Kati ya taasisi za kiisilam na zile za kikristo.
Mf. Kanisa katoliki peke yake linamiliki taasisi nyingi za kielimu kuliko zinazomilikiwa na taasisi zote za kiisilam kwa ujumla wao, kwa msingi huo lazima litoe wataalamu wengi kuliko wengine.

Kwa maoni yangu ndugu mzee Mohamed badala ya kuendelea mijadala mingi mara kuandika vitabu machapisho, na kulalamika tumia muda mwingi kutafuta taasisi zenye mrengo wa kuongeza wasomi ili ushindani uwe sawia na si kutafuta huruma.
 
Back
Top Bottom