Mohamed Said ana siasa za kulialia

a4a...
Huna la kusema kuhusu 20:80?

Huna la kusema kuhusu kuhujumiwa kwa miradi ya elimu mfano chuo kikuu kilichokuwa kinajengwa na EAMWS na chuo kilichotaka kujengwa na OIC?

Huna la kuchangia kuhusu kuhujumiwa kwa shule ya ufundi Kibaha iliyokuwa inataka kujengwa na Darul Iman ya Saudi Arabia?

Au NECTA na kuhujumu shule za Kiislam?
Au huamini haya kama kweli yamefanyika?

Vipi kuhusu barua ya Waziri wa Elimu Prof. Kighoma Malima kwa Rais Mwinyi akitahadharisha aliyoshuhudia katika wizara hiyo?

Au haya huyajui?

Hayo ya dua na tambiko si ya kutuhangaisha sisi amini unavyopenda.

Nimeeleza ha kuhusu dua na visomo wakati wa kudai uhuru na nimeeleza kuwa Mwalimu hakuwa wa kwanza kufanyiwa kisomo.

Mtu wa kwanza alikuwa Rashid Ally Meli kisha Abdul Sykes na Mwalimu alifanyiwa dua nyingine Lindi na Sheikh Yusuf Badi 1956 na nyingine Mnyanjani Tanga 1958.

Hii ndiyo historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Hii ndiyo historia mpya inayosomeshwa sasa hivi si ile ya Chuo Cha CCM Kivukoni.

Mjadala umependwa sana tunakimbilia wasomaji 7000.
 
Your browser is not able to display this video.
 
Walio shika madaraka wanahujumu kwa namna gani mzee wangu?

Kuhusu watu kuandamana haiwezi kuhalalisha kwamba wanacho kililia kipo kweli, kwa hiyo mzee wangu kama utanijibu hilo swali hapo juu au kama una link ya sehemu yoyote ulio elezea hilo swali naomba ili nikajisomee hoja zako
 
Phy...
Hizo hoja unazoleta sina tatizo kuzielewa kwa kuwa zinatoka kwako na wewe siyo unaetuhumiwa kwa hii dhulma.

Serikali iko kimya.

Rais Mkapa aliomba ushahidi wa Kisayansi kama kweli Waislam wanadhulumiwa.

Prof. Mustafa Hamza Njozi akatoa ushahidi kupitia kitabu chake, "Mwembechai Killings..." (2002).

Kitabu kikapigwa marufuku.
Kuwa na kitabu hiki ni kosa la jinai.

Mimi niko ndani ya darasa hili kusomesha yale ambayo hayakuwa yakifahamika.

Ndiyo maana unaona nikinyanyua kalamu najaza watu kwenye uzi wanakuja kusikiliza nini ninasema.

Ndiyo maana hata mtu akinitukana sijibu matusi yake.

Mtu akinikejeli sijibu kejeli zake.

Nafarajika na kuwa huyu anaenitukana kasoma niliyoandika na kasikia kile alichokuwa hakijui.

Wazee wangu walikuwa wakimsomea dua Nyerere kwa kuwa walikuwa pamoja na yeye kutafuta haki.

Mimi leo nasomewa dua kila siku.
Haniandikii mtu ila atahitimisha kwa dua.

Tuendelee na mjadala.

Mkizungumza haulipuki moto itafika mahali mtaelewana.

Allah ametufunza Waislam katika Qur'an anatuambia tusidhulumu wala tusikubali kudhulumiwa.
 
Mashine...
Ahsante sana.

Ukiwa hujui unauliza.

Ndiyo mwanzo naingia katika uzi huu nikawatahadharisha wasomaji kuwa wasiingie katika mjadala huu kama hawaijui historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Soma kitabu cha Abdul Sykes (1998) na soma kitabu cha Njozi(2002).

Kitabu cha Njozi soft copy iko mtandaoni.

Ingia: mohamedsaidsalum.blogspot.com.
 
fursa anazopewa muislam ni hizo hizo wanazopewa wakristo, kama ni elimu ipo bure, usipopeleka mtoto wako shule usije lalamika, tuna matatizo makubwa ya kitaifa ya kufanyia kazi sio ujinga wa wakristo au waislam wanabaguana.
 
Kuna mchangiaji ameuliza kuwa unawezaje kujua dini ya mtu?

Je kama mtu amezaliwa katika dini ya kiislamu then akabadili dini na kuwa mkristo lakini majina yake yakabaki kuwa hussein, shabaan, zulfa n.k au mtu amezaliwa katika dini ya ukristo na akabadili dini lakini majina yake katika vyeti yakabaki kuwa baraka, josefu daudi n.k.

Hii research ulioifanya ulitumia nyenzo gani kuwajua wote hao na biography zao?

Vipi kwa wale ambao wamezaliwa katika familia ambazo hazipo kati ya dini hizi mbili (tuwaite wapagani au waabudu mizimu) na kwa bahati nzuri au mbaya wakafanikiwa kupewa majina ambayo kwa mtazamo yameonekana kuwa upande wa ukristo au uislam?

Naomba majibu mzee wangu
 
Mzee wangu hapo unakuwa unaleta utata sana kwa sababu mi naamini kama mtunzi wa kitabu lazima utakuwa na soft copy na hivyo kuwarahisishia watu kwa kucopy paragraph uliyo elezea jibu langu.

Hivi kwa mfano mimi ni mkristo nitakuwa sahihi kwenye mjadala wa namna hii nikasema kafungue kitabu alicho andika mwakasege au kasikilize alivyo sema gwajima kuhusu waislamu? tuokoe muda na kama unavyo sema upo katika kutuelimisha watu tulio wengi basi fanya hivyo mzee wangu[emoji120]

Utanisamehe kama kuna sehemu nilipo kosea maana ki umri wewe ni sawa na baba yangu
 
Wewe mzee ungetupia link ya huo utafiti wako wa 20:80 .... jinsi unavyoendelea kujibu ndo unavyozidi kupoteza heshima yako na kuonekana mtu mpumbavu unayeaibisha uislamu. Serikali haiendeshwi kwa kufuata imani za watu.. elimu ndo msingi mkuu wa kupata ajira serikalini na sio dini. Wewe mzee ni mpumbavu sana.
 

 
Shikamoo mzee Said

Kabla sijakuuliza swali lolote lile Je unawafahamu WAZEE WA MIKOANI? Kwenye hoja zako umewazungumzia hawa wazee katika harakati za kudai uhuru?

Mie binafsi naufatilia huu mjadala toka mwanzo mpaka hapa ulipofikia. Sikutaka kabisa kuchangia ila kuna vitu naviona vinaendelea na nimesukumwa kutoa mawazo yangu binafsi. Kuna maswali mengi ya msingi ambayo mzee wetu anaulizwa ila anaakwepa akiwa na ufahamu mzuri kabisa na hajibu maswali kama anavyoulizwa. Mfano:

  • Mzee saidi hajui kuwa yaliyofanywa na wazee wa Dar bagamoyo ni matambiko ya asili na wala sio Dua. Au anajitoa ufahamu? Matambiko yaliyofanywa Tabora, Lindi na Bagamoyo yalikikuwa matambiko ya kiasili. Dini ya Kiislam wala Kikristo haisapoti matambiko ya aina haya, usitete hili jambo ukweli unajulikana
  • Mzee Said anadai aliyeongoza vita ya maji maji ni muislam, sawa ila anataka kutuaminisha waliopigana vita ile ni waislamu. Je vita ile ilipigwa na waislam? Na usilam unasupport fikra za kichawi kuwa risasi itageuka maji? Binafsi sidhani
  • Mzee Said anadai mangi sina alikuwa muislam, sawa sibishi ila Kilimanjaro kulikuwa na mangi wengi mno mfano mangi Marealle, Mangi George, Mangi Meli, Mangi Horombo nk. Ila yeye binafsi kamuona Mangi Sina na anadai alikuwa muislam, Mbona katika historia yako unaona yeye muislam peke yake huandiki kuhusu mangi wengine waliotaka kumtoa mzungu, kwani hujui Marealle alienda kudai uhuru na Mwl Nyerere?
  • Mzee Said, hata wazee wako walikuwa wasomi kama unavyodai na sibishi, sasa basi kama wazee hawa wa Dar kwa nini hawakumsimamisha Abdulwahid Sykes na chama chake alichokianzisha kwenda kutaka uhuru wa waislam? Huyu mzee alianzisha TANU (kwa madai yako na jina alitoa yeye akiwa vitani BURMA), sasa basi ilikuwa na ulazima gani kumshirikisha Mwl Nyerere?
  • Mzee Said anajua kabisa kuwa harakati za uhuru hazikuanza na wazee wa Dar, kuna vita nyingi zilipigwa na kuna viongozi wengi walikufa katika kudai uhuru. Je Mkwawa alikuwa muislam? Je vita ya maji maji ilipigwa na waislam? Mtemi isike alipigana vita kujikomboa alikuwa muislam? BABU ZAKO WALIPIGANA NA NANI (UKIACHANA KWENDA BURMA HUKU) TANGANYIKA KUDAI HUO UHURU?
  • Mzee Said anajua wazee wake walikuwa ni wazee wa Dar basi, kwa kuwa walikuwa wazee wa Dar je Tanganyika ilikuwa mali yao? Tanganyika inakaliwa na waislam tu? Mwl Nyerere alipita kila kona kuwashawishi kila himaya kila mkoa kuwashawishi machifu kuwaunga mkono kwenye harakati ya kudai Uhuru. MZEE SAID HUJUI MWL NYERERE ALIWASHAWISHI VIONGOZI MBALI MBALI TANGANYIKA NYOTE KUWAUNGA KUDAI UHURU.
  • Maji yakishawagiza hayazoleki na leo hii tunaishi dunia yenye dini mbali mbali kitu ambacho hakiwezi badilika. Nilitegemea kwa hekima zako utasema, Je unataka nchi yetu ya Tanzania iwe katika uongozi wa aina gani kuzingatia usawa haki na heshima kwa imani zote zilizopo Tanzania? Kila swali unaloulizwa unajikuta tu unawataja akina Sykes. Je leo hii historia mzee Sykes na familia yako inatukomboa vipi watanzania kwenye umasikini, uchumi, kiteknologia, kisiasa na kijamii? Hizi hoja zinamsaidia nini Muislam wa leo? Dunia haiwezi kuzunguka familia ya mtu mmoja kila kukicha. .
Mzee Said anajiita msomi, mie siwezi kukataa. Ila vitabu vyake vimelenga kuonyesha waislam na uhuru, sawa ila asitake kuuaminisha umma wa watanzania kuwa historia ya waislam na uhuru ndio historia ya Tanganyika. Sisi wengine tunatoka familia zenye mchanganyiko wa waislam na wakristo, mzee wangu CHUKI mbaya sana. Tunaona kuna nchi nyingi sana zenye waislam kwa 90% na kila kukicha tunaona vita kila siku mfano Syria, Afrighanstan nk. Kitu ambacho hujui mzee wangu leo hii Tanganyika au hata Zanzibar ikitawaliwa na waislam, kutatokea vita kubwa. Mimi nimeishi karibu na msikiti wa mtambani, yani kuna mgogoro mkubwa madhehebu mawili yanagombania msikiti mmoja. Jambo ambalo ukiangalia wote wanamuabudu Allah. Upendo uko wapi?

Mzee wangu mpaka Allah atakapokuchukua kwa mapenzi yake nakuhakikishia lengo lango halitotimia unajua kwa nini? Kwa sababu UKWELI haubadiliki. Kwa sababu Tanganyika tuna misingi ya umoja na sasa tunaoleana matabaka ya ukabila yamekufa kabisa na kamwe hatuwezi kugawanywa kwa misingi ya kidini, kwa sababu baba yangu Mkristo na Mama yangu Musilam, nikimbagua Muislam manake nimembagua mama na nikimbagua mkristo maana yake nimembagua baba. Hatuweki raisi kwa sababu ya dini yake, la hasha. Hili swala linaonekana linakunyika usingizi sana, haitokuja kutokea historia ya wazee wa Dar ikawa ndo historia ya Tanganyika. NYERERE ALIZUNGUKA NCHI NZIMA KUOMBA NGUVU, UMOJA NA MSAADA KWA MAKABILA YOTE ILI KUWAUNGANISHA TANGANYIKA KUWA KITU KIMOJA KATIKA UHURU. Hawa wazee wa mikoani wasingempa Mwl Nyerere nguvu hata angekuwa ametumwa na wazee wa Dar Tanganyika isingepata uhuru. .
 
Mashine...
Ikiwa unaona shida kusoma kitabu ingia kwenye hii blog na fanya name search:
mohamedsaidsalum.blogspot.com.
 

 

 
Sio nje ya mada isipokuwa umeogop kujibu ila mtu kama mohamed said amejibu na tunaendelea kuelimishana. HUWEZI KUTENGANISHA UTAWALA NA ELIMU.
Niogope kwani tunashindana?
Mada ni nani wengi?
Waislamu wanaonewa au hawaonewi.
Kwenye utawala waislamu wako vizuri kuliko wengine,
Ukipinga mdini,
Coz wenzio wa dini yako pia walilikubali hilo
 
Gill,
Marhaba.
Umeniuliza mengi lakini niatajibu kidogo tu ila hili neno "kujitoa fahamu," si neno zuri kumwambia mtu lakini naamini huenda hujui.

Ndiyo nilisema toka mwanzo usijadili mjadala huu ikiwa hujasoma kitabu cha Abdul Sykes.

Hivi sasa historia iliyoeleza ukweli wa harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika ipo kitabu hiki.

Laiti ungekuwa umekisoma usingekuja hapa ukauliza wazalendo waliopigania uhuru kutoka majimboni.

Ungesoma kitabu ungekutana na Ali Migeyo, Sued Kagasheki, Abdillah Rutabanzibwa (Bukoba), Dharura bint Abdulrahman na Nyange bint Chande (Tabora), Haruna Taratibu na Omar Suleiman (Dodoma), Salum Mpunga, Yusuf Chembera na mwalimu wao Sheikh Yusuf Badi (Lindi), Halima Selengia, Lucy Lameck, Mama bint Maalim na Amina Kinabo (Moshi), Sheikh Abdallah Rashid Sembe, Hamisi Kheri (Tanga) nk. nk.

Hayo mengine uliyoandika utayaelewa vyema kama kweli unajitambua kuwa hujui na sasa unataka kujua.

Ukisoma kitabu cha Abdul Sykes utaongeza maarifa.

Kwa ajili hii nimeamua kuyakalia kimya.
 
Mashine...
Ikiwa unaona shida kusoma kitabu ingia kwenye hii blog na fanya name search:
mohamedsaidsalum.blogspot.com.
Unacho kifanya bado si sawa mzee wangu samahani sana, umenipa link ya blog yako yenye article zaidi ya 100 huku ukisema umenipa unafuu wa kusoma kitabu.

Si sawa kujibu swali kwa mtindo huu na kama lengo ni kuelimisha watu basi hakika hawawezi kukuelewa.

Ili kurahisisha basi nipe link ya article husika ili nichukue hayo majibu yangu.

Napenda kujifunza.
 
Duh

Kuhusu mahakama ya kadhi, raisi mstaafu mzee Kikwete yeye mwenyewe alikataa jambo hili akiwa msikitini. Sasa kwa sababu ya chuki tu kila jambo litazungumzia ukristo. Nakumbuka mzee Kikwete aliwaambia kama mtahitaji sawa mnaweza fata sheria mkafungua mahamama za kadhi ila sharti ni

  • Misikiti igharamie kuwalipa wafanyakazi wake wote na yafunguliwe na misikiti. Serikali itawaweka kisheria ila tu lazima hawa mahakimu na wafanyakazi wake walipwe na misikiti. Swala la kadhi sio swala la watanzania ila ni swala la waislam wa Tanzania. Hivyo basi ikitokea mnataka kufungua mahakama hizi basi wafanyakazi wake walipwe na hel kutoka mfuko wa misikiti
  • La pili zikifunguliwa basi kusiwe na ulazima wa mtu kupelekwa mahakama hizi. Mtu binafsi anaweza kuchagua kesi yake isikilizwe mahakama ipi. Lakin mpaka leo nadhani kuna chombo huwa kinasikiliza mirathi ya waislam na mabaraza yake yanaamua, ila jambo hili linahusika vipi na kanisa?
Hayo mambo ya pengo kapiga simu mara pengo kasema ni maneno tu mtu anayatoa kinywani mwake. Nipe ushahidi wa pengo kumuita Bernard Membe. Tusifikie huko ndungu zangu, mambo mengi yanasemwa hivyo tu ila kibusara huwezi fanya jambo la mtu mmoja au dini moja kuwa jambo la taifa. Nchi yetu ina makundi mengi ya dini na viongozi wengi wapo na hata wasiokuwa na dini wapo. Hakuna mwenye haki zaidi ya mwingine. Dini zifanyike sehemu za dini tu ila serikali isimamie mambo ya msingi ambayo wananchi wanahitaji. Sasa kama ushahidi wako unazungumziwa kwenye msikitini, hapo unakosa mashiko. .

Makonda kusema serikali iko mikononi mwa kanisa hayo ni maneno tu ya mtu binafsi. Siyatilii maana ni kwa sababu huyo makonda mwenyewe sio serikali. Serikali ni bunger, mahakama na mhimili wa uongozi. Mawazo ya mtu binafsi hayawezi kuw mawazo ya nchi nzima tena azungumzie kwenye mikutano ya kanisa huko. .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…