Mohamed Said ana siasa za kulialia

Mohamed Said ana siasa za kulialia

Kuna vitu kadhaa vinajirudia hapa tena na tena ambavyo pia vinaongeza mashaka zaidi:
Mosi
Ni kama harakati za kudai uhuru wa Tanganyika miongoni mwa waisilam zililenga sana kudai uhuru wa waisilam na uisilam. Ikimaanisha walikuwa wanapigania uhuru wa uisilam, bahati mbaya ikawa kumpa ukamanda Nyerere ambaye ajenda yake ilikuwa uhuru wa Tanganyika na watanganyika wote.
Kama hivyo ndivyo basi Mungu aliingilia Kati kuzuia hiyo hila ya watu kujifanya wanadai uhuru wa nchi kumbe wanadai uhuru wa uisilam na waisilam.
Pili
Kwa namna hoja zinavyojengwa kama hujui chochote kuhusu Nyerere unaweza kudhani lilikua Zoba fulani hivi ambalo waisilamu kwa huruma zao walimuwezesha na kumfanya apate quality za kuongoza.
Wakati ukweli ni kwamba uwezo wa mwalimu na maono yake viliwafanya hao wote waone Mungu kawaletea mtu waliye mngoja kwa muda mrefu sana.
 
Wazungu gani waliokuwa wanatawala ?? Take it easy , tutaelewana tu , wala mimi simjibii Mzee Mohammed ,usitie wasiwasi
Mbona mie nishakujibu, sasa na wewe rejea kwenye Cambrige paper press usome. Nilitoa mfano kama ilivyo waislam walisaidia kudai uhuru basi kuna wakristo nao walisaidia na nikaweka evidence. Na kuna na sie babu zetu walikuwa hawana dini ila walisaidia sana sana kwa kuwa mie nimetoka kwenye ukoo wa Mangi nakueleza. .

Kilimanjaro kulikuwa na mangi wengi sana zaidi ya 30 na walipigana sana vita. Na mzungu alikuwa mjanja sana aliwatumia baadhi ya mangi kwa kuwawezesha kiuchumi ili kupiga mangi wengine. Lakini hawa nao walidai uhuru wao, hawakuwa waislam. Wakati Mwl Nyerere anaenda umoja wa mataifa kudai uhuru alimkuta teyari Mangi Marealle keshafika kudai uhuru wa kaskazini. Je huyu alikuwa Muislam? Maana Mwl aliomba sana support kwake kwa kuwa alikuwa ana nguvu sana Kaskazini huyu Mangi.

Historia yake mzee Said ya kibaguzi wewe binafsi sikuzuii kumsupport. Ila Mwl alipita mkoa mpaka mkoa kwa sababu support ya wazee wa Dar haikuwa inatosha kudai uhuru. Dar ulikuwa teyari wana support je mkoani huko? Sasa si ushasema wazee wa Dar hapo. Nyerere alipita mkoa mpaka mkoa tena mikoa mingine ilikuwa na viongozi mpaka wanne, kuomba wote wamsupport. Hawa walikuwa wengine wakristo wengine wapagani wengine mchanganyiko, leo hii utasemaje tu hii ni historia ya Tanganyika wakati historia hii imetungwa kuwazungumzia sehemu moja tu ambayo ni waislam?. .
Nadhani nimekujibu
 
Mbona ulisema kuwa nawewe huzungumzii dini ?

Mimi sijasema kitu kuhusu Quran wala biblia , nimekuuliza dua ni kitu gani kwa mujibu wa imani uliyonayo ??

Usijizonge , take it easy
Nimekujibu kulingana na imani niliyokuwa nayo. Sijazungumzia dini. Mbona majibu yangu yako very simple aisee wewe tu unaelewa slowly

Hakuna dini yeyote Tanzania iwe mkristo, muilsm au dini yeyote za mshariki ya mbali inasupport matambiko ya asili popote pale uendapo

Imani yangu matambiko ya mizimu ni mizizi ya kichawi, haiwezi kukubalika kwenye vitabu vya dini. .
 
Mbona mie nishakujibu, sasa na wewe rejea kwenye Cambrige paper press usome. Nilitoa mfano kama ilivyo waislam walisaidia kudai uhuru basi kuna wakristo nao walisaidia na nikaweka evidence. Na kuna na sie babu zetu walikuwa hawana dini ila walisaidia sana sana kwa kuwa mie nimetoka kwenye ukoo wa Mangi nakueleza. .

Kilimanjaro kulikuwa na mangi wengi sana zaidi ya 30 na walipigana sana vita. Na mzungu alikuwa mjanja sana aliwatumia baadhi ya mangi kwa kuwawezesha kiuchumi ili kupiga mangi wengine. Lakini hawa nao walidai uhuru wao, hawakuwa waislam. Wakati Mwl Nyerere anaenda umoja wa mataifa kudai uhuru alimkuta teyari Mangi Marealle keshafika kudai uhuru wa kaskazini. Je huyu alikuwa Muislam? Maana Mwl aliomba sana support kwake kwa kuwa alikuwa ana nguvu sana Kaskazini huyu Mangi.

Historia yake mzee Said ya kibaguzi wewe binafsi sikuzuii kumsupport. Ila Mwl alipita mkoa mpaka mkoa kwa sababu support ya wazee wa Dar haikuwa inatosha kudai uhuru. Dar ulikuwa teyari wana support je mkoani huko? Sasa si ushasema wazee wa Dar hapo. Nyerere alipita mkoa mpaka mkoa tena mikoa mingine ilikuwa na viongozi mpaka wanne, kuomba wote wamsupport. Hawa walikuwa wengine wakristo wengine wapagani wengine mchanganyiko, leo hii utasemaje tu hii ni historia ya Tanganyika wakati historia hii imetungwa kuwazungumzia sehemu moja tu ambayo ni waislam?. .
Nadhani nimekujibu

Sasa umeshindwa kitu gani kusema tu ni Waingereza ? Unajua kuwa Uingereza ni nchi ya Kikristo rasmi ? na Anglican ni state church ?
 
Nimekujibu kulingana na imani niliyokuwa nayo. Sijazungumzia dini. Mbona majibu yangu yako very simple aisee wewe tu unaelewa slowly

Hakuna dini yeyote Tanzania iwe mkristo, muilsm au dini yeyote za mshariki ya mbali inasupport matambiko ya asili popote pale uendapo

Imani yangu matambiko ya mizimu ni mizizi ya kichawi, haiwezi kukubalika kwenye vitabu vya dini. .

Hayo maelezo yako ndiyo tuelewe ni maana ya dua kwa mujibu wa imani yako ?
 
Kuna vitu kadhaa vinajirudia hapa tena na tena ambavyo pia vinaongeza mashaka zaidi:
Mosi
Ni kama harakati za kudai uhuru wa Tanganyika miongoni mwa waisilam zililenga sana kudai uhuru wa waisilam na uisilam. Ikimaanisha walikuwa wanapigania uhuru wa uisilam, bahati mbaya ikawa kumpa ukamanda Nyerere ambaye ajenda yake ilikuwa uhuru wa Tanganyika na watanganyika wote.
Kama hivyo ndivyo basi Mungu aliingilia Kati kuzuia hiyo hila ya watu kujifanya wanadai uhuru wa nchi kumbe wanadai uhuru wa uisilam na waisilam.
Pili
Kwa namna hoja zinavyojengwa kama hujui chochote kuhusu Nyerere unaweza kudhani lilikua Zoba fulani hivi ambalo waisilamu kwa huruma zao walimuwezesha na kumfanya apate quality za kuongoza.
Wakati ukweli ni kwamba uwezo wa mwalimu na maono yake viliwafanya hao wote waone Mungu kawaletea mtu waliye mngoja kwa muda mrefu sana.
Tanganyika ilikuwa na viongozi wengi wa kikabila, ukienda Kilimanjaro kulikuwa na Mangi, Ukienda pwani kulikuwa na mamwinyi, Ukienda Tanga kulikuwa na Jumbe, Ukienda sehemu nyingi kulikuwa na machifu nk

Wazee wa Dar hawakuwa na mamlaka ya Tanganyika hivyo Nyerere alipita kwa kila himaya, kila kiongozi wa kimila kuomba support. Wakati Nyerere anaenda kudai uhuru kuna mangi Marealle alienda kuomba uhuru wa kaskazini na teyari alikuwa na baraka zote za viongozi wa kaskazini. Hapo inaashiria nini? Inaashiria kuwa aliwashawishi viongozi wengi wa kaskazini wamsupport ili adai uhuru na kaskazini ila Nyerere aliweza pata support ya nchi nzima ambapo alizunguka kwenda mkoa kwa mkoa ndio maana tunamuita Muasisi wa Taifa. Wazee wa Dar walikuwa na support ya Dar tu hata kama wangeenda wasingepata ndio maana kujua hili wakakubali kuwa chini ya mwalimu Nyerere kama viongozi wengine wengi Tanganyika. .

Hakuna Uhuru uliodaiwa kwa ajili ya waislam na hakuna uhuru uliodaiwa kwa ajili ya wakristo. Huyu mzee Said hakuwahi kumuhojo mwalim Nyerere wakati alikuwa teyari keshaandika vitabu vyake na Mwl yupo. Na rejea zake nyingi hazina ushahid zaid ya NIMESIMULIWA. Sasa aliyekusimulia kama alikudanganya je, maana yake kuna ngano za uongo. Vitabu vyake huyu mzee kwa jinsi alivyoviandika vitasomwa kama vitabu vya hadithi, wala si historia ya nchi ya Tanganyika. .

Uko huru kuamini ngano zake za kutunga ambazo hakutaka kuwahoji wahusika. Ila yote ni kukimbiza upepo tu. .
 
Sasa umeshindwa kitu gani kusema tu ni Waingereza ? Unajua kuwa Uingereza ni nchi ya Kikristo rasmi ? na Anglican ni state church ?
Anglican ina uongoz wake na England ina uongozi wake. Vivyo hivyo Anglican ni dini na Uingereza ni nchi, na haikutawala dini ilitawala nchi. Sijui kama unaelewa. Leo hii kuna nchi nyingi za kiislam lakini Uislam upo hata kabla ya hizi nchi. Huwezi kuzungumzia utawala wa kinchi na kidini usichanganye. .
 
Ajibu vipi tena ?? Inaelekea hivyo vyeti vyenu feki mlivyopewa kwenye shule za makanisa vinawapa shida. Hata kuingia kwenye blog mnashindwa kutafuta material
Janina,
Mimi ningekuwa wewe nisingejibu hivyo.
Ningemsomesha.

Kuna mtu anapenda dua iwe tambiko na sababu ni kuwa anataabishwa na kunasibisha dua na Qur'an.

Mimi kumuongezea uelewa nimemwambia kuwa Nyerere si wa kwanza kufanyiwa dua.

Mtu wa kwanza ni Rashid Ali Meli Bwana Fedha wa Dar-es-Salaam Municipal Council.

Akiwa ni mjuzi akiingia katika blog yangu na kufanya name search atamkuta Rashid Ali Meli na uhusiano wake na TANU na Nyerere na sababu ya yeye kufanyiwa kisomo.

Atasoma na kuelewa kuwa Rashid Ali Meli alihudhuria mkutano wa kwanza wa TANU ukumbi wa Arnautoglo August 1954.

Usijibu kwa ghadhabu.
Jambo lolote ukilitia upole litapendeza.
 
Kuna vitu kadhaa vinajirudia hapa tena na tena ambavyo pia vinaongeza mashaka zaidi:
Mosi
Ni kama harakati za kudai uhuru wa Tanganyika miongoni mwa waisilam zililenga sana kudai uhuru wa waisilam na uisilam. Ikimaanisha walikuwa wanapigania uhuru wa uisilam, bahati mbaya ikawa kumpa ukamanda Nyerere ambaye ajenda yake ilikuwa uhuru wa Tanganyika na watanganyika wote.
Kama hivyo ndivyo basi Mungu aliingilia Kati kuzuia hiyo hila ya watu kujifanya wanadai uhuru wa nchi kumbe wanadai uhuru wa uisilam na waisilam.
Pili
Kwa namna hoja zinavyojengwa kama hujui chochote kuhusu Nyerere unaweza kudhani lilikua Zoba fulani hivi ambalo waisilamu kwa huruma zao walimuwezesha na kumfanya apate quality za kuongoza.
Wakati ukweli ni kwamba uwezo wa mwalimu na maono yake viliwafanya hao wote waone Mungu kawaletea mtu waliye mngoja kwa muda mrefu sana.
The Phy,
Sehemu ya kwanza umekosea.
Waislam walitamani sana Wakristo wengi wajiunge na African Association ili ipatikane nguvu ya umoja wa wananchi wote.

Hii ndiyo sababu Kleist Sykes baada ya kuunda African Association 1929 akaunda Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) 1933.

Hakutaka agenda za Waislam zipitie African Association.

Historia hii unaweza ukaisoma kwenye kitabu na kwenye blog yangu: "Kleist Sykes Man of Ideas."

Unaweza pia kusoma historia hii katika Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam, East Africana: Kleist Sykes The Townsman (1968) seminar paper iliyoandikwa na Aisha Daisy Sykes.

Halikadhalika kwenye Dictionary of African Biography, Kleist Sykes, Oxford University Press New York 2011.

Uhodari wa Mwalimu nimeueleza kwa kirefu sana katika kitabu cha Abdul Sykes.

Abdul Sykes yeye alimtaka amwingize Chief David Kidaha Makwaia Hamza Mwapachu alitoa rai kuwa Nyerere ni aula zaidi.

Mazungumzo haya kati ya Sykes na Mwapachu yalifanyika nyumbani kwa Mwapachu Nansio, Ukerewe katika miezi mitatu ya mwanzoni 1953.

Mtu mwingine aliyekuwako katika mazungumzo haya alikuwa Ali Mwinyi Tambwe Secretary wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Ingia utasoma yote haya na mengi zaidi bure: mohamedsaidsalum.blogspot.com.

"Elimu Bila Khiyana."
 
Janina,
Mimi ningekuwa wewe nisingejibu hivyo.
Ningemsomesha.

Kuna mtu anapenda dua iwe tambiko na sababu ni kuwa anataabishwa na kunasibisha dua na Qur'an.

Mimi kumuongezea uelewa nimemwambia kuwa Nyerere si wa kwanza kufanyiwa dua.

Mtu wa kwanza ni Rashid Ali Meli Bwana Fedha wa Dar-es-Salaam Municipal Council.

Akiwa ni mjuzi akiingia katika blog yangu na kufanya name search atamkuta Rashid Ali Meli na uhusiano wake na TANU na Nyerere na sababu ya yeye kufanyiwa kisomo.

Atasoma na kuelewa kuwa Rashid Ali Meli alihudhuria mkutano wa kwanza wa TANU ukumbi wa Arnautoglo August 1954.

Usijibu kwa ghadhabu.
Jambo lolote ukilitia upole litapendeza.
Shukrani sana, Mzee wetu
 
Anglican ina uongoz wake na England ina uongozi wake. Vivyo hivyo Anglican ni dini na Uingereza ni nchi, na haikutawala dini ilitawala nchi. Sijui kama unaelewa. Leo hii kuna nchi nyingi za kiislam lakini Uislam upo hata kabla ya hizi nchi. Huwezi kuzungumzia utawala wa kinchi na kidini usichanganye. .

Mkuu wa Anglical church ni nani?
 
La
The Phy,
Sehemu ya kwanza umekosea.
Waislam walitamani sana Wakristo wengi wajiunge na African Association ili ipatikane nguvu ya umoja wa wananchi wote.

Hii ndiyo sababu Kleist Sykes baada ya kuunda African Association 1929 akaunda Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) 1933.

Hakutaka agenda za Waislam zipitie African Association.

Historia hii unaweza ukaisoma kwenye kitabu na kwenye blog yangu: "Kleist Sykes Man of Ideas."

Unaweza pia kusoma historia hii katika Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam, East Africana: Kleist Sykes The Townsman (1968) seminar paper iliyoandikwa na Aisha Daisy Sykes.

Halikadhalika kwenye Dictionary of African Biography, Kleist Sykes, Oxford University Press New York 2011.

Uhodari wa Mwalimu nimeueleza kwa kirefu sana katika kitabu cha Abdul Sykes.

Abdul Sykes yeye alimtaka amwingize Chief David Kidaha Makwaia Hamza Mwapachu alitoa rai kuwa Nyerere ni Allah zaidi.

Mazungumzo haya kati ya Sykes na Mwapachu yalifanyika nyumbani kwa Mwapachu Nansio, Ukerewe katika miezi mitatu ya mwanzoni 1953.

Mtu mwingine aliyekuwako katika mazungumzo haya alikuwa Ali Mwinyi Tambwe Secretary wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Ingia utasoma yote haya na mengi zaidi bure: mohamedsaidsalum.blogspot.com.

"Elimu Bila Khiyana."
Lakini dhana ya "amani" au ile aliyotumiridhwa mtu "rehemati lil Al amin" haikuwa kwa waislam pekee, ni kwa viumbe vyote hadi mimea kaka Mohamed wasomeshe hawa, wao wanachanganya madai yako ya kuenguliwa kwa makusudi kwa jitahidi za waislam kuupata uhuru wa Tanganyika na udini(ubaguzi wa waislam kwa wasio waislam) ule ubaguzi wa roho mbaya, laa Mohamed anachotaka ukweli uelezwe na ijulikane wazi makusudi ya kuondoshwa waislam katika historia yaani ifahamike nia ovu ya hawa waondoaji ambao kinara wake ni julius Nyerere (pamoja kwamba bwana julius Ana Mazuri yake)
 
Tanganyika ilikuwa na viongozi wengi wa kikabila, ukienda Kilimanjaro kulikuwa na Mangi, Ukienda pwani kulikuwa na mamwinyi, Ukienda Tanga kulikuwa na Jumbe, Ukienda sehemu nyingi kulikuwa na machifu nk

Wazee wa Dar hawakuwa na mamlaka ya Tanganyika hivyo Nyerere alipita kwa kila himaya, kila kiongozi wa kimila kuomba support. Wakati Nyerere anaenda kudai uhuru kuna mangi Marealle alienda kuomba uhuru wa kaskazini na teyari alikuwa na baraka zote za viongozi wa kaskazini. Hapo inaashiria nini? Inaashiria kuwa aliwashawishi viongozi wengi wa kaskazini wamsupport ili adai uhuru na kaskazini ila Nyerere aliweza pata support ya nchi nzima ambapo alizunguka kwenda mkoa kwa mkoa ndio maana tunamuita Muasisi wa Taifa. Wazee wa Dar walikuwa na support ya Dar tu hata kama wangeenda wasingepata ndio maana kujua hili wakakubali kuwa chini ya mwalimu Nyerere kama viongozi wengine wengi Tanganyika. .

Hakuna Uhuru uliodaiwa kwa ajili ya waislam na hakuna uhuru uliodaiwa kwa ajili ya wakristo. Huyu mzee Said hakuwahi kumuhojo mwalim Nyerere wakati alikuwa teyari keshaandika vitabu vyake na Mwl yupo. Na rejea zake nyingi hazina ushahid zaid ya NIMESIMULIWA. Sasa aliyekusimulia kama alikudanganya je, maana yake kuna ngano za uongo. Vitabu vyake huyu mzee kwa jinsi alivyoviandika vitasomwa kama vitabu vya hadithi, wala si historia ya nchi ya Tanganyika. .

Uko huru kuamini ngano zake za kutunga ambazo hakutaka kuwahoji wahusika. Ila yote ni kukimbiza upepo tu. .
Gily,
Umesema sikufanya mahojiano na Mwalimu Nyerere.
Kweli sikufanya mahojiano na Mwalimu.

Lakini kuna mtu mkubwa sana aliniahidi kumuona Mwalimu kuniwekea miadi.
Huyu bwana hadi leo yuko kimya hajanieleza kama alionana na Mwalimu au vipi.

Lakini mimi nilijua kabla vipi Mwalimu alivyokuwa ''uneasy,'' inapokuja kuandika historia ya TANU.

Nilijua hata kama atamuona Mwalimu hawezi kukubali kufanya mahojiano na mimi kuhusu historia ya TANU hata kama kitabu kile ni cha rafiki yake Abdulwahid Kleist Sykes.

Kitu gani kilinifanya mimi niwe na shaka hii?

Kwanza nilikuwa najua farka iliyotaka kuingia katika jaribio la kwanza la kuandika historia ya TANU Nyerere akihusika na kumchagua Dr. Wilbard Klerruu kushirikiana na Abdul Sykes kuandika historia ya TANU.

Kwa nini Abdul Sykes?

Sababu ni kuwa katika wale wote waasisi 17 ni waasisi wawili tu Abdul na Ally Sykes ambao wana nasaba na TAA kuanzia AA kwani ni chama alichoasisi baba yao mwaka wa 1929 na wao wakaja kuwa waasisi wa TANU achilia mbali kuwa walimpokea Nyerere nyumbani kwao 1952 na kumtia katika uongozi wa TAA kisha TANU.

Hii mosi.
Pili hawa akina Sykes walikuwa na nyaraka kuanzia AA, TAA hadi TANU.

Kubwa walikuwa na mswada wa kitabu alioacha baba yao baada ya kufa 1949.

Mswada huu unaeleza kila kitu kwanza kuhusu siasa za Dar es Salaam ya 1920s hadi kufikia 1940s siasa za mji ukiongozwa na TAA na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Abdul alijitoa katika mradi huu na sababu ni kuwa Nyerere hakuwa na raha na kile alichokuwa anakisoma kutoka kalamu ya Abdul Sykes.

Judith Listowel ameandika kitabu, ''The Making of Tanganyika,'' (1965).
Kuna barua Nyerere anamlalamikia kuhusu alivyomwandika.

Nyerere hakukipenda kitabu hiki.

Mwaka wa 1981 Chuo Cha CCM Kivukoni kilipokuwa kinaandika historia ya TANU kiongozi wa jopo Dr. Mayanja Kiwanuka alikataa kupokea ''notes,'' za Abdul Sykes kama rejea katika historia ya uasisi wa TANU.

Atakae historia hii anaweza kuingia katika blog yangu ataikuta akiweza na asome kitabu cha Abdul Sykes.

Hii ndiyo sababu kitabu kizima cha historia ya TANU kilichoandikwa na Kivukoni hukuti jina la Abdul Sykes na wengine wengi.

Kuhusu Mangi Mkuu Thomas Marealle kuwa alikwenda UNO kudai uhuru wa Kaskazini hii ni propaganda ya TANU hakuna ukweli katika hilo.

Nimesoma barua za Chief Marealle alizokuwa akiandikiana na Ally Sykes nimekuta mengi sana lakini sikuweza kuyaandika katika kitabu cha Abdul Sykes.

Ila hapa nitaeleza kitu kimoja tu kuwa Chief Marealle na Abdul Sykes walikuwa marafiki wakubwa.

Kwa kuhitimisha napenda kusema kitu kimoja kuwa nina mengi niliyosoma katika Nyaraka za Sykes mengi sijayatoa hadharani.

Hakuna aliyekuwamo katika siasa zile za 1950s ambae mimi sikumkuta na kumsoma katika Nyaraka za Sykes.

Tusimame hapa.
Inatosha.

Gily,
Chunga ulimi wako ndugu yangu.
Kweli mimi ni Mohamed Said Salum Abdallah Mswahili wa Kariakoo.

Wala wewe si wa kwanza kuonyesha dharua kwangu wengi wamefanya hivyo.
Unasema rejea zangu hazina ushahidi.

Unataka ushahidi gani zaidi ya Nyaraka za Sykes katika historia ya TANU?
Unazo wewe nyaraka zaidi ya hizi?

Nakusihi jitulize na soma ninayoandika hapa na iulize nafsi yako ya ndani itakupa jibu.
Angalia Nyaraka ya Sykes yenye majina ya viongozi wote wa TAA 1953:

1639759676870.png
 
Kuna vitu kadhaa vinajirudia hapa tena na tena ambavyo pia vinaongeza mashaka zaidi:
Mosi
Ni kama harakati za kudai uhuru wa Tanganyika miongoni mwa waisilam zililenga sana kudai uhuru wa waisilam na uisilam. Ikimaanisha walikuwa wanapigania uhuru wa uisilam, bahati mbaya ikawa kumpa ukamanda Nyerere ambaye ajenda yake ilikuwa uhuru wa Tanganyika na watanganyika wote.
Kama hivyo ndivyo basi Mungu aliingilia Kati kuzuia hiyo hila ya watu kujifanya wanadai uhuru wa nchi kumbe wanadai uhuru wa uisilam na waisilam.
Pili
Kwa namna hoja zinavyojengwa kama hujui chochote kuhusu Nyerere unaweza kudhani lilikua Zoba fulani hivi ambalo waisilamu kwa huruma zao walimuwezesha na kumfanya apate quality za kuongoza.
Wakati ukweli ni kwamba uwezo wa mwalimu na maono yake viliwafanya hao wote waone Mungu kawaletea mtu waliye mngoja kwa muda mrefu sana.
Kuna bandiko linalomuhusu Mzee Dossa Azizi Ally, sijajua bado limeandikwa na nani, japo kiuandishi linafanania na Mzee wetu huyu.

Mle ndani Muandishi anatuonesha ukaribu wa Nyerere na Dosa Azizi Ally, namna walivyopambana bega kwa bega kudai Uhuru.

Mwishoni baada ya Uhuru anataja kutokea kwa mipasuko baina ya Nyerere na Dossa.
Anasema Mpasuko ulitokea baada ya Nyerere alipotaka Baraza LA Wazee la TANU, ambalo wajumbe wengi walikuwa waislamu, liongozwe na Waislamu ambao ni Waafrika(Weusi).

Hilo kwa Mzee Dosa na wenzake walilitafsiri kama ni Hujuma dhidi ya Uislamu.

Sasa, kwa Mindset ya Mzee Mohammed Said kama wazee wake nao walikuwa alivyo yeye Leo, kuna uwezekano mkubwa walitaka Uislamu use sehemu ya sura ya Serikali. Kuna uwezekano ndio chuki kati ya Nyerere na kundi hili ilipozaliwa.

Mzee Mohamed Said, binafsi nikuhakikishie kuwa kilele cha mafanikio ya harakati zako hizi, ni siku watoto au wajukuu zako mwenyewe, watakapoona fahari kuchinjana hadharani na kujivunia.

Kaka na kaka wa ukoo wako watajivunia kumwagana damu kabla hawajawafikia majirani zao.

Na hayo ndio mafanikio ya wale uwaitao wa kimataifa wanaobariki maandiko yako, nawe ukajivika ufahari kusifiwa na adui za wajuukuu wako.

Binafsi nitakusihii Ujitafakari upya, Kwa Uzee wako kwetu vijana ni Fahari. Utumie vizuri.
 
Kitali,
Unaijua idadi ya dini asilia?

Walipata kuwapo na kuunda chama cha siasa kupigania uhuru wa Tanganyika?

Hii leo wapo na wana maslahi yeyote katika ujenzi wa taifa hili?

Unawajua viongozi wao?

Unadhani unaweza kupambanisha hoja ya upagani na historia ya Waislam wa Afrika ya Mashariki?

Jibidiishe kusoma.

we unajua uhuru tu ila hao waarabu walichowafanyia wenyeji ulishakiandika?
 
Back
Top Bottom