Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,526
- 34,057
a4a...Kuna bandiko linalomuhusu Mzee Dossa Azizi Ally, sijajua bado limeandikwa na nani, japo kiuandishi linafanania na Mzee wetu huyu.
Mle ndani Muandishi anatuonesha ukaribu wa Nyerere na Dosa Azizi Ally, namna walivyopambana bega kwa bega kudai Uhuru.
Mwishoni baada ya Uhuru anataja kutokea kwa mipasuko baina ya Nyerere na Dossa.
Anasema Mpasuko ulitokea baada ya Nyerere alipotaka Baraza LA Wazee la TANU, ambalo wajumbe wengi walikuwa waislamu, liongozwe na Waislamu ambao ni Waafrika(Weusi).
Hilo kwa Mzee Dosa na wenzake walilitafsiri kama ni Hujuma dhidi ya Uislamu.
Sasa, kwa Mindset ya Mzee Mohammed Said kama wazee wake nao walikuwa alivyo yeye Leo, kuna uwezekano mkubwa walitaka Uislamu use sehemu ya sura ya Serikali. Kuna uwezekano ndio chuki kati ya Nyerere na kundi hili ilipozaliwa.
Mzee Mohamed Said, binafsi nikuhakikishie kuwa kilele cha mafanikio ya harakati zako hizi, ni siku watoto au wajukuu zako mwenyewe, watakapoona fahari kuchinjana hadharani na kujivunia.
Kaka na kaka wa ukoo wako watajivunia kumwagana damu kabla hawajawafikia majirani zao.
Na hayo ndio mafanikio ya wale uwaitao wa kimataifa wanaobariki maandiko yako, nawe ukajivika ufahari kusifiwa na adui za wajuukuu wako.
Binafsi nitakusihii Ujitafakari upya, Kwa Uzee wako kwetu vijana ni Fahari. Utumie vizuri.
Sijaelewa umekusudia nini kusema, ''kuchinjana.''
Nani atamuua nani na kwa sababu gani?