Mohamed Said ''Mzungu wa Unga,'' 2007 Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere


Acha kupiga chenga.
Nirudi kusoma kisa kizima ili iweje?
Nimeijibu post yako kwa kui-quote. Tuendelee kuanzia hapo.
Isitoshe, si mara ya kwanza wewe kusimulia kisa hicho nimekisoma mara kadhaa.

Kama mwandishi aliyechoka, nafikiri kwa sasa umeishiwa cha kuandika. Unaandika yale yale kwenye threads tofauti. Utaongelea Habari za ibadan, na kukamatwa uwanja wa ndege, au utaanzisha thread ya Mwapachu au Kunambi au jina lolote lile, lakini hatimaye lengo ni ku-promote kitabu chako cha Sykes et al., na ku-promote chuki za kidini.

Nahisi hata wafuasi wako watakuwa wamekustukia, hawaji kwa kasi na matusi kama zamani au unaonaje kaka Moh'd?
 
Kama waislam wa Nigeria walisema ingekuwa sawa na kutangaza vita kwanini waislamu wa Tanzania msitangaze vita?
Tangazeni vita muuwe maadui zenu kwa Sababu hata uislamu unaruhusu kuua adui na ukiua adui unapata pepo.
Kuua adui wa waislamu ndio njia rahisi ya kupata pepo kwa mujibu wa uislamu.
 
MrOnline225,
Huijui historia ya Tanganyika.
Lakini nitakusaidia.

Msome Bergen (1981), Sivalon (1992) na
Njozi (2002).

Ukipenda msome Said (1998).

Ila kitabu cha Njozi kimepigwa marufuku
lakini kinapatikana mtandaoni.
 

Nanren,
Ikiwa hutaki kurudia kusoma sikulazimishi.

Kisa hiki kipo kwenye blog yangu toka 2008 na inapobidi huwa nakieleza kufatana na matokeo ya nyakati.

Labda huenda hujui.

Historia haina ukomo wa kusomwa kwani kila
siku wanakuja wasomaji wapya.

Kitabu changu kila aliyekisoma atamweleza mwenzake yale mapya aliyojifunza.

Kitabu cha Sykes hakina upungufu wa wasomaji wapya kwa hiyo hakinitaabishi.

Angalia uzi huu wamekuja watu gani?
Ninapoandika hata wewe unashindwa kujizuia.

Kama ni suala la mtu kusoma na kuchangia ni "ufuasi," hata wewe hujasalimika.
 
MrOnline225,
Huijui historia ya Tanganyika.
Lakini nitakusaidia.

Msome Bergen (1981), Sivalon (1992) na
Njozi (2002).

Ukipenda msome Said (1998).

Ila kitabu cha Njozi kimepigwa marufuku
lakini kinapatikana mtandaoni.
Mkuu samahani naweza kupata link ya hicho kitabu cha "Njozi"?
 
Kitulo,
Unaandika huku umekasirika.
Ghadhabu humfanya mtu akasema maneno akitulia anajuta.

Tufanye mjadala wa kisomi ili jamii inufaike na haya tunayoandika
kiasi miaka 100 baadae wakija watu kutosoma watasema hakika
wazee wale waliotangulia walikuwa watu makini.
 

Kwa neno ufuasi, najua unaelewa nilichomaanisha, ila unajitoa ufahamu kijanja. Wafuasi unao, wale wanaokuona wewe ni "infalliable" na wanakutetea unapopotosha umma.
 
Labda kwann unahangaika na historia ni kama mambo yalopita pia kizazi cha sasa hawana mda wa kushugulika na historia wao wanaangalia maisha yanakwenda vipi kwa nyakati hizi,wanaoshughulika na history labda waliozaliwa kabla ya Uhuru ambao hawazidi hata 20% ya watanzania wote.
 
MrOnline225,
Huijui historia ya Tanganyika.
Lakini nitakusaidia.

Msome Bergen (1981), Sivalon (1992) na
Njozi (2002).

Ukipenda msome Said (1998).

Ila kitabu cha Njozi kimepigwa marufuku
lakini kinapatikana mtandaoni.


bro nimesoma historia tangu darasa la 3 ila sijawahi ambiwa popote uhuru ulipiganiwa na wakristu au waislam

ila wewe ndio unataka kuleta udini kutaka iwe confrmd kua waislam walipigania uhuru

fikiria kwanza madhara yake kabla hujaleta izo propaganda zako za udini
 
Kenstar,
Hapana sihangaiki mimi nastarehe sana ninapokuwa hapa ''ofsini,''
kwangu natoa hizi darsa.

Mimi ni mpenzi wa jazz basi ninapofungua hiki kijiofisi changu
hufungua na muziki nikiwasikiliza wapigaji wangu ninaowapenda.
dala
Yawezekana kuna watu hawapendi historia lakini wako wanaopenda
na ndiyo kama hivi wewe unachangia hapa.

Pia nina blog www.mohammed.com inasomwa dunia nzima.
Ukiingia hapo umenaswa kwani kuna mengi ambayo yatakustaajabisha.

Nimeanzisha sehemu makhsusi nimeipa jina, ''Kutoka JF,'' hapa utakutana
na zile mada ambazo mjadala ulikuwa mkali sana.

Wanangu wananishauri nihamie Macintosh wanasema ndiyo itanifaa zaidi
kwa kazi zangu.

Nawajibu kuwa siwezi kujifunza upya wao wanasema watanifundisha.
Mambo ni kama hivi.

Huwa naalikwa katika TV na radio na vipindi vyangu Alhamdulilah vinapendwa.
Hivi vipindi viko katika ''gallery,'' kwenye blog.

Niko vilevile kwenye Yuo Tube.

Tembea hii blog naamini utafaidika na elimu iliyopo mle.
Chembelecho Maalim Faiza: ''Elimu Bila Khiyana.''
 
MrOnline255,
Nitakupa darsa In Shaa Allah kuhusu historia ya Tanganyika na kwa nini
historia ilichakachuliwa.

Natoka kidogo.
Waalike na jamaa waje darsani wasome.

Nimerejea.

Hebu tuanze darsa na historia ya TANU tukianza na historia ya mtangulizi
wake African Association iliyoasisiwa mwaka wa 1929:
Saturday, 24 January 2015
KLEIST SYKES (1894 - 1949) KATIKA DICTIONARY OF AFRICAN BIOGRAPHY (DAB) OXFORD UNIVERSITY PRESS, NEW YORK





Jengo Hili la African Asociation Lilijengwa kwa Kujitolea Kiongozi Akiwa Kleist Sykes
Hapa Ndipo Palipokuja Kuzaliwa TANU Mwaka 1954



Msomaji nakuwekea hapa vipande kutoka Dictionary of African Biography (DAB) ambao ni mkusanyo kwa njia ya maandishi historia ya Waafrika walioacha alama katika maendeleo ya bara hili.

Huu ulikuwa mradi wa Oxford University Press (OUP) na Chuo Cha Harvard na ulichukua miaka kadhaa kukamilika.

Nilikuwa mmoja wa waandishi waliotakiwa kuwaandika baadhi ya Watanzania na Watanganyika waliofanya makubwa katika historia ya nchi yao. Mradi huu ulikuwa chini ya Prof. Emmanuel K. Akyeampong wa Harvard na ulikusanya wanahistoria 500 kutoka Afrika na kwengineko.

Nilimshauri Prof. Akyeampong akate baadhi ya majina aliyoniletea ya Watanzania kwa kuwa kwa hakika hawakuwa na mchango wowote wa maana isipokuwa labda baadhi walipata kuwa na vyeo katika serikali uhuru ulipopatikana mwaka wa 1961. Nilifanya hivi kwa makusudi kabisa kwa kujua kuwa waliokuwa madarakani hawakutaka hata kidogo historia ya kweli ya waliopogania uhuru wa Tanganyika ifahamike na kuthaminiwa. Hii sasa ikawa nafasi yangu ambayo lau kwa uchache ningeliweza kuiweka sawa historia ya kweli ya Tanganyika.

Mimi nilisahau kabisa kuhusu kazi hii na hata ilipochapwa mwaka 2011 ilinichukua miaka minne kuja kukumbuka na kuanza kufuatilia nini ilikuwa hatima ya ule mradi na hapo ndipo nilipoona hii Dictionary of African Biography katika mtandao.
OUP wametoa volume sita za kazi hii mwaka 2011.

Volume hizi sita zinauzwa USD 1300 na vilevile zinapatikana kwenye mtandao kwa ''subscribers.'' Nimeletewa kutoka School of African Studies, London ukurasa ulio na makala niliyoandika kuhusu maisha ya Kleist Sykes (1894 - 1949) nami nimeona itakuwa vyema kama nitaweka hapa vipande vipande ili wasomaji wasome kwa faida ya kuhifadhi kumbukumbu za wazee wetu.

Labda msomaji utataka kujua kwa nini nilichagua kuandika maisha ya Kleist Sykes katika Dictionary of African Biography.

Nimemchagua Kleist Sykes kwa sababu hizi kubwa:
  1. Kwanza alikuwa ndiye katibu muasisi wa African Asociation mwaka 1929 na muasisi wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika 1933 akiwa katibu vilevile na kwa jinsi siasa za kiloloni zilivyokuwa wakati ule za ''wagawe uwatawale,'' yeye aliunganisha vyama hivi katika uongozi mmoja lau kama Al Jamiatul Islamiyya kilikuwa chama cha Waislam na wakati huo huo akaweza kuweka misingi ya kuwashirikisha Wakristo katika kupigania haki za Mwafrika wa Tanganyika katika African Association.
  2. Pili Kleist alifungua mlango wa Waislam wawe na shule zao wenyewe ili kukabiliana na shule za Wamishionari ambazo zilikuwa zikiwabatiza watoto wa Kiislam katika shule zao na hili liliwafanya wazazi wa Kiiislam kusita kuwapeleka watoto wao shule.
  3. Tatu katika kutimiza hili alianzisha shule ya Kiislam - Al Jamiatul Islamiyya Muslim School ambayo ilisomesha masomo ya kisekula na Qur'an. Inasemekana ilikuwa ndoto ya Kleist kuona Qur'an inasomeshwa kwanye madarasa juu ya madawati na wanafunzi wamekaa katika viti kama shule badala ya zile madras za asili ambazo watoto wanakaa chini katika majamvi. Nia yake ikiwa kuwa katika shule mtoto atapata yote mawili - elimu ya dini yake na masomo ya kisekula. Ndoto hii ya Kleist sasa si ndoto tena kwani shule za Kiislam nyingi zimeanzishwa nchini pote miaka mingi baada ya yeye kutangulia mbele ya haki zikisomesha Qur'an na masomo ya kisekula kwenye darasa moja na mwalimu akiwa kasimama mbele ya ubao.
  4. Jambo la nne ni lile la kuuweka wazi mlango wa TANU kwa Wakristo ambao wakati wa vuguvugu la kuanzisha African Association mwaka 1929 serikali iliwatisha wasijiunge na chama hicho. Hii inatokana na yeye kuwa na akina Cecil Matola, Raikes Kusi na Rawson Watts katika uongozi wa African Association na kwa njia hii kujenga msingi wa umoja na ushirikiano kwa Waafrika wote bila kujali dini zao. TANU ilipokuja asisiwa na wanae Abdulwahid na Ally wazalendo wengine mwaka 1954 hali ilikuwa haijabadilika lakini uongozi wa Waislam ndani ya TANU uliweka mkakati maalum wa kuhakikisha kuwa TANU haivurugwi na hisia za Uislam kiasi cha kuwaweka pembeni ndugu zao Wakristo.
Hii ndiyo sababu ikawezekana Nyerere kuchaguliwa kuongoza TAA mwaka 1953 na TANU ilipokuja asisiwa mwaka 1954 watoto wake wawili Abdulwahid na Ally wakiwa kati ya waasisi 17 kutoka sehemu mbalimbali za Tanganyika haikuwa tabu kwake yeye kukabidhiwa jukumu la kuwaunganisha Waafrika chini ya bendera moja ya kudai uhuru. Itoshe tu safari ya kwanza ya TANU kujitangaza nje ya Dar es Salaam Nyerere aliifanya 1954 Morogoro akifuatana na Zuberi Mtemvu na nyingine ilikuwa 1955 Lindi akifuatana na Rajab Diwani na Ali Mwinyi Tambwe Katibu wa Al Jamiatul Islamiyya.

Hizi ndizo sababu nne zilizonipelekea kuandika maisha ya Klesit Sykes katika Dictionary of African Biography.


Zuberi Mtemvu kama alivyokuwa 1962;
Picha hii ilipigwa nyumbani kwa Abbas Sykes
Shaaban Robert Street



Kushoto Abbas Kleist Sykes na Abbas Zuberi Mtemvu
Abbas Mtemvu alipewa iina hili kwa heshima ya Abbas Sykes



Abbas Sykes Wakati Akiwa Balozi Kulia ni Balozi Salim Ahmed Salim na
kushoto ni
Bhoke Munanka


 
Mohamed Said,
Kwa hotuba hiyo ambayo umetubandikia na kwa wanaoelewa hali ya mambo nchini Tanzania nachelea kusema ulikuwa unamwaga sumu labda bado unaendelea kumwaga sumu kwa umma wa watanzania (waislam na wasio waislam). Tupe ushahidi kanisa kutaka kuua uislam, tupe ushahidi kwamba Waisalam nchini Tanzania ni wengi kuliko makundi mengine, tupe ushahidi pia kwamba vita vya majimaji vilipiganishwa na waislam pekee, tupe ushahidi kwamba uhuru wa Tanzania ulipiganiwa na waislam pekee na kuukabidhi kwa wakristo. Mohamed, kwa uongo huo ulistahili kubanwa na hata hivo nashangaa ni kwa nini uliachiwa huru hufai kukaa ndani ya jamii.

Nikuunge mkono kwa hili, Amerika ni mchonganishi na anachokiangalia ni maslahi yake tu. Amerika amefanikiwa kukuaminisha wewe kuwa nchini Tanzania kanisa ni adui wa uislam (you're very wrong). Kwa hali hiyo, ndio maana unapita na unataka kupita dunia nzima kutangaza uongo kwamba waislam wa Tanzania wanadhulumiwa haki zao na ni daraja la pili katika nchi ambayo wao wameiletea uhuru. Wahausa wa Nigeria walipigwa na butwaa baada ya kusikia mada yako hata mimi ningeshangaa yaani kundi Fulani limwage damu kasha matunda ya damu zao yakabidhiwe kwa kundi linguine kasha kundi kabidhiwa lianze dhuluma dhidi yao hii inasikitisha sana na kama ni sumu kweli ulimwaga. Boko Haramu kule Nigeria ilipata nguvu kupitia wamwaga sumu kama wewe. Na mashaka kama wewe haufungamani na wale magaidi wa Mkuranga na Amboni Tanga.

Nakushauri, tangaza ukweli bila kushawishiwa na makundi yaliyo nje ya mipaka ya Tanzania na uwe mwakilishi mzuri kwa nchi yako. Wanaofahamu ukweli hotuba yako haikuwa kitu kingine bali kueneza chuki kati ya makundi mawili kama ulivyosema (waislam na wakristo)
 
sasa naanza amini jamaa liposema religion is opium of the people...... ni kama mzee wetu umepoteza imani na nchi yako kabisa unaanza elekea radicalism..unanikumbusha jamaa yangu tulisoma naye shule ya msingi aliishia mpiga vibao raisi mstahafu sasa hivi amekua kama amerukwa hivi...angalizo www.mohammed.com sio website na wala hakuna kitu..na swala la kusachiwa mbona hata raisi mstahafu alishawahi sema watanzania walikua wanabeba sana madawa hadi naye alisimamishwa kiwanja cha ndege ughaibuni..nadhani swala hapo ni eneo ulilotokea kipindi hicho kama tehran ndipo madawa ya kulevya yalikua yanasambazwa sana na haina haja kuituhumu serikali..nisamehe mzee wangu kama nimekukosea heshima..ni mawazi =o ya upeo wangu mdogo tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…