Mohamed Said ''Mzungu wa Unga,'' 2007 Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere

Tatizo ninaloliona hapa ni kutaka tuamini takwimu za wakati wa majimaji na sensa ya mwaka 1957. Kuna mabadiliko makubwa ya kidemografia yametokea baada ya wakati huo. Leo hii watu wengi wanaamini katika dini mbalimbali kuliko ilivyokuwa awali. Inawezekana kabisa kutokana na utamadumi wa mikoa ya pwani waislamu walikuwa wengi kuliko wakristo mwaka 1957, lakini haimaanishi waislamu walikuwa wengi kuliko wapagani(wenye imani za kijadi) na baada ya hapo mabadiliko makubwa yametokea ikiwemo kupungua sana kwa wanaoamini imani za jadi.

Walakini mwingine ni imani yako kwamba vita vya majimaji vilipiganwa na waislamu. Yawezekana viongozi wengi walikuwa waislam, lakini haina maana wapiganaji wote walikuwa waislamu. Tena siamini kama kulikuwa na msukumo wa kidini katika kupigana, la sivyo wasingetumia uganga kuwaaminisha watu kuwa kuna dawa ya kubadilisha risasi kuwa maji.

Mwisho, mzee wetu una maisha mazuri na unasafiri sana sababu ya misimamo yako. Unakula na kuishi kwa kutumia misimamo yako. Binafsi sishangai wamarekani kukufadhili katika mihadhara yako pamoja na misimamo yako kutowapendeza. Wazungu wana akili sana kiasi cha kuwaweka 'maadui' wao karibu. Haina maana wanakubaliana na unachokisimamia. Pia, unajinasibu kama 'wa kariakoo', wasiwasi wangu upo ndani ya yai la Dar es Salaam na haujui uhalisia wa mambo nje ya Dar es Salaam. Kwa fikra zako, Kariakoo ndiyo Tanzania. Naamini una safari nyingi za nje kuliko za Nkasi kule Rukwa.
 
Hivi Tito okelo ni muislam? Acha udini acha kabisa huko Libya walikouwawa Si walikuwa Waisalam kwa Waisalam?
 
Laiti dini na madhehebu yetu yangekuwa na mikakati kama ya kanisa la Roman Catholic, tungepiga hatua sana kama taifa. Leo hii ardhi sehemu nyingi za Tanzania ni bei chee karibu na bure. Kuna sehemu unaweza ukaenda ukafyeka pori na likawa eneo lake lenye mamia ya hekari. Miaka 30 ijayo hayo maeneo ndio yatakuwa city center maana hata Sinza ilikuwa mashamba ya mpunga miaka ya 60-70.

Sasa jiulize taasisi za kiislamu zinamiliki eneo kiasi gani na RC ina miliki eneo kiasi gani. Hiyo ndiyo tofauti na mzizi wa fitna na chuki-long term planning. Umejichimbia kariakoo na sitashangaa huna hata ekari 100 za ardhi pamoja na nafasi adhimu ya kipato uliyonayo. Wewe ni mzee wa mjini, hupendi kwenda shamba.

Mzee mwenzio Njozi alipiga sana kelele na kitabu chake cha 'Mwembechai Killings', mwishowe akapata shavu la MUM na sasa ametulia maana huwezi ukaongea huku unakula. Tatizo la Njozi nae ni kwamba pamoja na elimu na uzoefu mkubwa alionao ameshindwa kukijenga chuo cha MUM kwa kukitawanya kikaenea kwa 'ndugu zake' aliokuwa anawatetea. MUM ilipaswa kuwepo Mtwara au Lindi, Tanga, Tabora au Kigoma. Kama vyuo vya juzi kama TEKU wameweza yeye anashindwa nini? SJUT ina tawi Mtwara, Njozi kafanya nini? Kuna watu wameumbwa ili kukosoa, sio kutenda.
 

Kuhusu "chokochoko" ukiisoma vizuri ile post amekuwekea alichomjibu Nanren, katika uzi mwengine.

Hiyo chokochoko ilielekezwa kwa Nanren. Kasome tena utaelewa kuwa ile post katuwekea alichomjibu Nanren.
 
Sooth,
Kwanza napenda kukufahamisha ''kuwa siendeshi maisha yangu kwa kuhadhiri
wala kwa, ''royalities.'' za vitabu nilivyoandika ingawa ni moja ya vyanzo la pato
langu.

Kuhusu mabadiliko nakubaliana na wewe kuwa yapo mabadilko mengi ya, ''demography.''
Ila lazima utambue kuwa hiyo ni barabara ya njia mbili.

Kuhusu uongozi katika uhuru wa Tanganyika kuanzia 1929 hadi uhuru ulipopatika 1961
nimetafiti na nimeandika kitabu cha Sykes ambacho ndicho kinachosomeshwa katika vyuo vingi
Afrika, Ulaya na Marekani.

Kitabu hiki ndiyo kisa cha mimi kualikwa kwingi.

Hakuna popote niliposema kuwa Wamarekani wanakubaliana na mimi lakini kitu kimoja
ni wazi kuwa wamenufaika na utafiti wangu kwa kauli zao wenyewe hili wamelisema.

Hili la Kariakoo katika harakati za uhuru wa Tanganyika halina shaka.

Vita vyote vilianza hapo na hadi leo hizo nyumba mipango ya kupambana na ukoloni
ilipokuwa ikipangwa zipo na nikizijua vyema.

Sasa ikiwa na wewe unayo historia kama hii ya Kariakoo kutoka kwenu Nkasi, Rukwa
wengi naamini wangependa kusoma.

Napenda kukufahamisha kuwa katika utafiti na kuandika niko karibu zaidi na Waingereza
kuliko Wamarekani.

Dictionary of Africa Biography (DAB) ambayo naamini umesoma katika post zangu za nyuma ingawa
ulikuwa mradi wa Harvard lakini kitabu kimechapwa na Oxford University Press, New York.
 
Sooth,
Ukitaka kuzungumza chochote kuhusu historia ya Waislam na kama ulivyojinasibu na hiyo ''yetu,''
na kusema, ''dini na madhehebu,'' ushajiweka peupe kila mtu keshakujua.

Hebu kwanza soma historia ya Sheikh Hassan bin Amir, Tewa Said Tewa, EAMWS na historia ya
Muslim Congress 1962 na 1963 ndiyo ulete hiyo hoja ya kutaka kufananisha mipango ya Kanisa
Katoliki.

Kwani ungeliyajua yaliyotokea wala usingekuwa na sauti ya siyo tu kumkejeli Njozi bali hata hii
mada usingetia neno lako.

Haipendezi kuzungumza jambo usilolijua.
 
Mzee wangu kwa umri na elimu yako wayajua mengi kuliko mimi, lakini haina maana unajua kila kitu. Pokea ushauri ninaokupa wewe na Prof. Njozi.
 
Mzee wangu nimekupata na nitakujibu kama ifuatavyo: Mapambano hayana mwisho maana udhalimu ni sehemu ya maisha ya binadamu. Mfano mzuri wa mapambano yasiyoisha ni South Africa na USA. Katika nchi hizo watu weusi wamepitia harakati na mapambano ambayo yamewafanya wawe tofauti sana na raia wa nchi nyingine kwa sababu harakati zinaishi kizazi kimoja mpaka kingine.

Sasa mbona nyie wanaharakati wa 'Kariakoo' harakati zenu zimefikia ukingoni? Kuna mambo serikali yetu inayafanya ndivyo sivyo, mbona mko kimya? Wewe ni mfano mzuri wa watu wanaolalamika bila kuchukua hatua katika sanduku la kura. Amini nakuambia, nguvu hizo ungezielekeza katika kubadilisha mfumo wa kisiasa au ungezielekeza kwa wanasiasa, ungefanikiwa sana. Tatizo harakati zako wazielekeza kwa maskini na walalahoi walio wengi. Zikitokea fujo za kidini, wanaoumia ni maskini. Wewe mwenye kipato kizuri utapanda ndege kwenda Nigeria kwa rafiki zako maana una pasipoti kitu ambacho kwa 90% hawana. Nakuomba uelekeze nguvu zako sehemu sahihi. Vyovyote mnavyotendewa, vinatendeka chini ya serikali ya CCM ambayo wewe hauthubutu kuikosoa.
 
Freya,
Hujafikia makamo ya kufanya mjadala wa aina hii.
 
Mmm
 
Sooth,
Mimi silalamiki wala sipambani na yoyote kwa hiyo ndugu yangu hujanijui
toka mwanzo na hivyo yote uliyosema hayawezi kuwa yananihusu mimi au
ndugu yangu yoyote wa Kariakoo.

Mimi nimeandika historia ya uhuru wa Tanganyika historia ambayo ilikuwa
karibu ipotee kabisa.
 
Mzee wangu kwa umri na elimu yako wayajua mengi kuliko mimi, lakini haina maana unajua kila kitu. Pokea ushauri ninaokupa wewe na Prof. Njozi.
Sooth,
Kwani umenipa ushauri gani?
Wala sijasema mie najua kila kitu.

Usikose kusoma rejea nilizokuwekea unaweza ku-search:
www.mohammedsaid.com
 

Kweli kabisa mzee Mohamed
 
= halikadhalika

Wapi Yesu amesema kuweni Wakristo?

Fungua uzi tuwekane sawa kuhusu Uislam na Ukristo, hapa si mahala pake.
Muislamu anayeamini anafanya vema, maaa anaamini bila kuona, mkristo nae anayeamini, anafanya vyema maana anaamini bila kuona.

Nyote mnaamini, hakuna ushahidi wala kigezo, mmepokea imani kutoka kwa waliotutangulia kuishi, na waliokuwa na upeo kuliko sisi, kwa hiyo, msidozoane, wala asiwepo wa kuona yeye ni bora wakati anamini kwa imani kama mwingine, kwa sababu hana kigezo anachotumia kumponda mwenzie, bali ni imani iliingia moyoni mwako kwa sababu ya kusikia tu, wala siyo kuona, kama na yeye anavyoamini kwa kusikia.
 

Fungua uzi.
 
Mimi nawatambua watu kwa matendo, sio maneno wala sura.
 
Sooth,
Kwani umenipa ushauri gani?

Wala sijasema mie najua kila kitu.

Usikose kusoma rejea nilizokuwekea unaweza ku-search:
www.mohammedsaid.com
Ushauri wangu ni kwamba ni kazi ngumu na ashakum- ya kinafiki sana kuangalia na kushadidia kilichotokea miaka 70 iliyopita wakati una nafasi ya kuangalia, kupangilia na kutekeleza kitakachotokea miaka 70 ijayo. Wewe una influence, hamasisha taasisi zilizojikita Dar ziende mikoani zikanunue ardhi kwa ajili ya shughuli za ibada na huduma za jamii. Hii siri nakuibia kutoka kwa wakatoliki-wananunua ardhi kwa wanakijiji kwa bei chee, wanaisahau kwa miaka kadhaa halafu wanaipima na kuonekana prime land. Ardhi ipo ya bwerere leo, lakini kesho itatugombanisha kwa sababu tu wengine walilala wakati wengine wanakesha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…