Mohamed Said ''Mzungu wa Unga,'' 2007 Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere

Mohamed Said ''Mzungu wa Unga,'' 2007 Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere

The 1967 census has not been able to show the reasons for the sudden decrease of Muslim population nor the growth of animists amidst believers in the span of the last ten years.
Mkuu Maalim Mohammed Said, kuna swali nataka kukuuliza, ila kabla sijauliza, kwanza naomba maana ya neno "animist" ulimanisha nini?. Na hao uliowaita "believes" unamaanisha nini ndipo swali langu lifuate.
Paskali
 
Ushauri wangu ni kwamba ni kazi ngumu na ashakum- ya kinafiki sana kuangalia na kushadidia kilichotokea miaka 70 iliyopita wakati una nafasi ya kuangalia, kupangilia na kutekeleza kitakachotokea miaka 70 ijayo. Wewe una influence, hamasisha taasisi zilizojikita Dar ziende mikoani zikanunue ardhi kwa ajili ya shughuli za ibada na huduma za jamii. Hii siri nakuibia kutoka kwa wakatoliki-wananunua ardhi kwa wanakijiji kwa bei chee, wanaisahau kwa miaka kadhaa halafu wanaipima na kuonekana prime land. Ardhi ipo ya bwerere leo, lakini kesho itatugombanisha kwa sababu tu wengine walilala wakati wengine wanakesha.
Sooth,
Kaka unanipeleka wapi huko?
 
Kuhusu "chokochoko" ukiisoma vizuri ile post amekuwekea alichomjibu Nanren, katika uzi mwengine.

Hiyo chokochoko ilielekezwa kwa Nanren. Kasome tena utaelewa kuwa ile post katuwekea alichomjibu Nanren.
Sawa bibi kifimbo cheza nimerudia kuusoma na nimeelewa nashukuru.

swali la kizushi.. inamaana kwenye hilo bandiko langu hujaona kabisa?
 
Laiti dini na madhehebu yetu yangekuwa na mikakati kama ya kanisa la Roman Catholic, tungepiga hatua sana kama taifa. Leo hii ardhi sehemu nyingi za Tanzania ni bei chee karibu na bure. Kuna sehemu unaweza ukaenda ukafyeka pori na likawa eneo lake lenye mamia ya hekari. Miaka 30 ijayo hayo maeneo ndio yatakuwa city center maana hata Sinza ilikuwa mashamba ya mpunga miaka ya 60-70.

Sasa jiulize taasisi za kiislamu zinamiliki eneo kiasi gani na RC ina miliki eneo kiasi gani. Hiyo ndiyo tofauti na mzizi wa fitna na chuki-long term planning. Umejichimbia kariakoo na sitashangaa huna hata ekari 100 za ardhi pamoja na nafasi adhimu ya kipato uliyonayo. Wewe ni mzee wa mjini, hupendi kwenda shamba.

Mzee mwenzio Njozi alipiga sana kelele na kitabu chake cha 'Mwembechai Killings', mwishowe akapata shavu la MUM na sasa ametulia maana huwezi ukaongea huku unakula. Tatizo la Njozi nae ni kwamba pamoja na elimu na uzoefu mkubwa alionao ameshindwa kukijenga chuo cha MUM kwa kukitawanya kikaenea kwa 'ndugu zake' aliokuwa anawatetea. MUM ilipaswa kuwepo Mtwara au Lindi, Tanga, Tabora au Kigoma. Kama vyuo vya juzi kama TEKU wameweza yeye anashindwa nini? SJUT ina tawi Mtwara, Njozi kafanya nini? Kuna watu wameumbwa ili kukosoa, sio kutenda.

Hiyo "dini na madhehebu" yako ni ipi?

Kumbe dini yako ni "inferior" kupita "Roman Catholic"? Yenye haya 10 secrets of the Vatican exposed ambayo dini na madhehebu yako inayaona bora na kutaka kuyaiga?

Unafikiri kuwa na ardhi kubwa ndiyo kuwa na dini na dhehebu bora?

Laiti ungaliujuwa Uislam japo kiduchu usingekuja na hoja muflis kama hiyo.

Nakuomba fungua uzi tuje tukupe darsa ni nini Uislam.

Unajitahidi sana kuutoa mjadala kutoka historia na kuupeleka kwenye dini, tunaelewa.
 
Siku zote kinachofanyaga utoe ile kauli yako ya maudhi ni nini eti?

= kinachofanya

Hata historia hii anayotupa Alama Mohamed Said inawaudhi wengi.

Seuse FF anaekupa ilm ya bure.

Ni vigumu sana mtu aliyesomea ujinga kumfundisha akakuelewa - kumbuka hilo.
 
Hiyo "dini na madhehebu" yako ni ipi?

Kumbe dini yako ni "inferior" kupita "Roman Catholic"? Yenye haya 10 secrets of the Vatican exposed ambayo dini na madhehebu yako inayaona bora na kutaka kuyaiga?

Unafikiri kuwa na ardhi kubwa ndiyo kuwa na dini na dhehebu bora?

Laiti ungaliujuwa Uislam japo kiduchu usingekuja na hoja muflis kama hiyo.

Nakuomba fungua uzi tuje tukupe darsa ni nini Uislam.

Unajitahidi sana kuutoa mjadala kutoka historia na kuupeleka kwenye dini, tunaelewa.
Dada Faizan mimi nakuonyesha MTO ulipo, kunywa maji ni hiari yako. Nimetekeleza wajibu wangu kama mtanzania.
 
= kinachofanya

Hata historia hii anayotupa Alama Mohamed Said inawaudhi wengi.

Seuse FF anaekupa ilm ya bure.

Ni vigumu sana mtu aliyesomea ujinga kumfundisha akakuelewa - kumbuka hilo.
seuse = seuze.

caught you at your own game, missus!!
 
Mohamed Said

Mimi ni mkiristo niliwahi kusimamishwa hapo airport na kusachiwa kwa madai kwamba nasafari Sana na wanadhani ninajihusisha na madawa.

Nilikalishwa hapo masaa matatu kuulizwa maswali ambayo hayana kichwa wala miguu.
Ndungu zangu waliokuja kunipokea na wenyewe
Wakapigwa maswali ambayo hayana mbele wala nyuma.

Wakaniambia yakwamba watakuwa wanafuatilia mwenendo wangu. sababu hawakupata kitu walichokiwa wanatafuta. mpaka nimeichukia airport ya Dar .

Hata siku moja sijawahi kuwaza wanafanya hivyo sababu mimi ni mkristu. Nilichokuwa nawaza ni kwamba hawa watu wanahitaji elimu kwa vile mtu unasafiri Sana haimaanishi unafanya biashara haramu.

Thread yako imekosa maana ulipoingiza udini .
 
I love you so much (mada zako kali na arguments zako zimekomaa, ttz lako udiiiiiiiini mpaka kufa)


Sasa huo udini tatizo langu au lako? Au tatizo lako ni Uislam? Funguka tu.

Maana mimi nikii quote biblia au Qur'an ni mdini? Wewe uki i quote biblia au Qur'an au useme huviamini vyote na u mpagani basi si mdini? Fikiri.
 
Dada Faizan mimi nakuonyesha MTO ulipo, kunywa maji ni hiari yako. Nimetekeleza wajibu wangu kama mtanzania.


Nnaona hoja imekuingia na unaanza kubwabwaja na kuhororoja bila mpango. Ulifikiri "yetu" ingekusaidia?

Unioneshe mto wakati nna kisima uani kwangu, si upunguani huo.
 
Kwa umri wa huyu mzee alipaswa kuwa na busara. Ni kwa nini kila linalomhusu au kumkuta maishani lazima analihusisha na dini?
 
Back
Top Bottom