Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #401
Nanren,Kwa usomi wako nafikiri utakuwa unajua McCarthyism.
Unatumia similar techniques kukwepa hoja ili kushinda.
Unalazimisha eti kifua "kinanifukuta" . Huko ni kupoteza hoja. Kifua kinifukute kwa lipi?
Au unafikiri sijawahi kusikia muslim heroes?
Mbona wako wengi tu dunia nzima?
Tatizo lako ni kupenda ku-exaggerate stories ili zionekane "sensational" kwa wasomaji wako. Ili baadhi ya waislam wajisikie kweli kuwa wameonewa, na kuwa tusio waislam hatupendi wajikomboe na hatupendi maendeleo yao, something which is untrue!
Hapo ndipo penye maajabu ya kitabu cha Sykes na yale niliyoeleza.
Huwa hayamwachi mtu salama.
Historia hiyo itamtaabisha sana.
Kuamini anataka na kuikataa Othman anataka.
Prof. Haroub Othman juu ya kukisoma kitabu na kufanya mazungumzo
na mimi hakutosheka.
Akamuuliza Ahmed Rashad Ally kama kweli Abdul Sykes ndiye aliyeasisi
TANU.
Mzee Rashad akamwambia,''Prof. kwani kipi cha ajabu? Baba yake Abdul
Mzee Kleist kaasisi African Association cha kushangaza nini mwanae kuasisi
TANU?''
Prof. Haroub hakutosheka akaenda kwa Nyerere mwenyewe apate ukweli.
Mimi sishangai ninavyokuona unaungua na kutaabika.
Wewe si wa kwanza.
Hebu staladhi na hii hapo chini:
Mohamed Said, hakika kuna mambo yanatia maudhi si kwasababu nyingine bali pale yanapotoka.
Wewe ni mzee na hutakiwi kuwa tricky za mjidala za kitoto kiasi hiki.
Wapi nimeandika kuishi na watu si muhimu?
Onyesha hapa jamvi lione, kama hutaonyesha basi tambua unaukejeli umri wako na heshimaWewe jnayeweza kumkashfu Nyerere unasababu za kunisitiri mi
.Hapa ndipo panaonyesha jinsi usivyoweza mjadala na usivyoelewa.
Hivi mtu anaweza kuomba document tu bila kusema document gani na wewe ukatoa tu bila kujua ameombwa nini!!!
Hakuna mahali nimeomba document , nilichokiomba ni katiba ya kuandika au ya kukopi ya Abdul Sykes au Baba yake au ukoo mzima kama wanayo.
Hadi sasa hukuweza kuleta na kusingizia zimeibiwa Dodoma.
Ukweli, hakuna mahali Abdul aliandika katiba tukujia elimu yake ya darsa la 10. Ni fact
Kitu kinachoitwa katiba Abdul Sykes amekiona kutoka kwa Nyerere.
Sasaunasema Nyerere alikopi, well, iwe hivyo au la bado alikuwa anajua nini kinatakiwa.
Ingalikuwa rahisi,Abdul Sykes angekopi ziku nyingi. Hawakuweza kwasababu hawakujua namna ya ku transform chama kuwa institution, yeye na baba yake.
Waiendesha chama kwa umaarufu na hilo si jambo baya.
Ukweli upo pale pale hawakuwahi kuandika katiba asilani hadi anfariki Husemi nimeomba document gani, na kwa jinsi usivyoweza au usivyojua unaleta documents,yaani ukiombwa unatoa tu bila kujua umeombwa nini, real mzee!
Kwamba mtu anaweza kusema MS naomba document nawe ukaingia kabatini na kuleta document usiyojua ni ipi! it doesbn't make sense at all rather than telling us more
Mohamed kilichotakiwa si document ni katiba au rasimu aliyoandika Abdul Sykes!
Micro film imeibiwa Dodoma haijibu hoja na ni njia za mkato za kukwepa ukweli, tunataka ushahidi kuwa Abdul Sykes aliwahi kuandika katiba ya chama kabla ya Julius Nyerere! period Mwiba upi umekwama? Mwiba umekwama kwako ndiyo maana unaleta document yoyote na kusema ni katiba ya TAA! Pathetic
Sasa wanajmvi someni katiba ya TAA aliyoandika Abdul Sykes probably kwa msaada wa nyaraka za baba yake Kleist Sykes.
Someni katiba ya chama hapa chini kaa ilivyoletwa na Alama Mohamed Saidi
Katiba ya Abdul Sykes- Mohamed Said
Halafu katiba ya Abdu Sykes inaendelea hapa kama ilivyoletwa na Mwapachu katika kuongeza nguvu umuhimu wa katiba ya Abdul Sykes Hapa mnaweza kuona 'katiba' aliyoandika Abdul Sykes kama ilivyoletwa na Mohamed Said. Please MS usimdhalilishe Abdul kiasi hicho.
Tafadhali sana uwezo wako usilete adha na fadhaa kwa familia nzima.
Kama huna hoja , kukaa kimya ni busara kuliko kuendelea kumdhalilisha Abdul.
Mtu akisoma hiyo kama ndiyo katiba ya kuunga unga vipande vigine kutoka kwa mwapachu na maongezi kuwa katiba ni dhalili ya juu sana. Kwamba hiyo ndiyo katiba aliyoandika Abdul Sykes ni aibu ! si kwa aliyeandika bali wewe uliyeileta hapa bila kujali dhalili yake!
Nguruvi3,
Umezungumza mengi ambayo hayana maana kwa hiyo sitajibu ila
hili la kumdhalilisha Abdul Sykes.
Mimi ndiye niliyemfufua Abdul Sykes kwa kuandika maisha yake na
ndiyo leo uko hapa unatokwa na povu na jasho.
Kitabu kimechapwa miaka 18 iliyopita lakini hadi leo kinavuma kila mtu
anakisoma tunakwenda sasa toleo la 4 katika miaka 18.
Kushoto ni Brendon Grimshaw
Unakijua kisa cha Brendon Grimshaw aliyekuwa Mhariri Mkuu wa gazeti,
Tanganyika Standard?
Unaijua taazia aliyomwandika Abdul Sykes baada ya kuona kuwa magazeti
ya TANU Nationalist, na Uhuru, yamemdhalilisha kwa kukataa kuandika
ukweli wa mchango wake kwa Nyerere na TANU yenyewe?
Mimi nimdhalilishe Abdul Sykes?
Nitaanzia wapi?
Huna moja ulijualo katika historia hii.
Wanamajlis,
Ikiwa mnataka kujua Grimshaw alisema nini kuhusu Abdul Sykes mwaka
wa 1968 katika Tanganyika Standard semeni nitoe darsa In Shaallah.
Grimshaw akijuana na Abdul toka 1950s.