Nime notice ukiwa Nairobi, Kariakoo and Hausa country unavaa vibaraghashia na kanzu za Mtume, ukiingia DC, Chicago, Geneva unavua haraka sanaaaa...
Nimeomba details za elimu yako ya msingi na sekondari. Wanapohakiki vyeti hawajali shahada, tunataka STANDARD 7, FORM IV, FORM VI. Huwezi kutaja, elimu yako ya awali ni suspect!
By the way, ulipokuwa Hausa country umetudanganya walikwambia Nigeria hakuna na hawawezi kuwa na anti-Terrorism laws. Nigeria inaongoza Afrika kwa uhanga wa ugaidi, haiwezi kuwa haina anti terror laws. The Terrorism Prevention Act, 2011 as amended in 2013 zipo.
Wale watu wa airport ambao mwisho wa siku ulikuja gundua walikuwa hawana mpango wa kukuwekea madawa ulirudi kuwaomba msamaha? Manake walikuwa kazini in good faith wakifuatilia suspicions and instructions za USA juu yako, a firebrand islamist zealot...
Kuruani Takatifu inakataza dhana, Al Isra, sura ya 17 pamoja na Al Hujurat, sura ya 49. Ukidhani nduguyo ana nia ovu ukaja gundua ulimhisi kimakosa kaombe radhi. Muislam unapigania nafasi ya dini yako wakati we mwenyewe huna high moral ground?
Kwameh,
Sijui kwa nini huniamini.
Nimekwambia kuwa mie mtupu sina elimu ndugu yangu.
Kuhusu mavazi itabidi nikufahamishe hulka yangu na jinsi nilivyofunzwa
kuhusu mavazi.
Mimi nimewaona wazee wangu wakienda kazini wanavaa shati suruali kama
kawaida lakini wakirudi nyumbani baada ya kazi jioni huwa wanavaa kanzu
na ndani wanavaa seluni.
Hizi ni nguo nyepesi na zinamfanya mvaaji kuwa ''relaxed.''
Mimi nikialikwa nje ya nchi na inategemea na mazingira na nyakati hupenda
kuvaa kanzu, kofia na hutupia kashda kuonyesha utambulisho wangu kama
Muislam.
Nikiwa kwenye miji mikubwa ya dunia kama Paris, London, New York wakati
niko shughulini kuvaa kanzu itanizuia ''movement,'' hivyo navaa mavazi muafaka
na hali iliyopo.
New York Grand Central hapo juu nitachekesha kama nitakuwa nimevaa kanzu na makbadhi
nadandia treni kwenda kwangu Manhattan.
Tambua pia kuwa mavazi yanakwenda na umri.
Angalia picha hii hapo chini nilipokuwa kijana hapo nipo London wakati wa Kiangazi
kiasi cha miaka 30 iliyopita:
Na hii chini niko kijana Paris 1993 na navaa kama vijana wanavyovaa kwa umri
wao unavyoruhusu tena nipo Paris Central Mosque 1993 nimekuja kusali.
Angalia sasa mtu mzima 2011 niko Paris nimevaa vipi:
Hapo chini niko Cape Town:
Hapo chini nipo Hamburg Train Station nitachekesha kama nitakuwa
ndani ya suti ya Yves Saint Laurent (YSL) au Gucci.
Tungeweza kuzungumza mengi katika mavazi lakini naamini kwa mifano
hii utakuwa umeelewa.
Kuhusu sheria ya ugaidi Nigeria mimi sikusema uongo.
Wakati nazungumza Chuo Kikuu Cha Ibadan mwaka 2006 sheria hii ilikuwa
bado kupitishwa.
Hayo mengine nitakuwa kimya maana naona ndugu yangu sijui niite hasad au
kitu gani naona unapandwa na mori na chuki dhidi yangu pasi na sababu na
unanishambulia.
Umebeba joto kali katika kifua chako.
Huu ni mjadala ndugu yangu usikuathiri kwa kiwango hicho.
Niko Makka:
Nilikotoka: