Mohamed Said: TANU kilikuwa chama cha Kiislam, hili hakuna mtu anayeweza kulipinga

Status
Not open for further replies.
Ok tunakubali TANU ni ya Wislam, kuna jingine? Pia mnaweza mkachukua na CCM kama munaihitaji sababu imetufikisha mbali sana.
 
Hii santuri imechuja...kila baada ya muda watu wale wale, fikra zile zile, porojo zile zile, malalamishi yale yale, na ngano zile zile starring wafia dini Mohamed Said na FaizaFoxy. Mwaka kesho bila shaka hadithi nyingine kama hii itatungwa na safari hii si ajabu ikapewa jina lingine kama; Mwalimu Nyerere alifuta shule zote za Waislaam na kubakiza za Wakristo tu! Yaani hawa watu wawili wametia fora kwa kuwalisha vijana wa leo matango pori na wao huitikia tu hewala na kumeza tu kama misukule vile!

Kwa walioingia Jamii Forums majuzi tu naomba niwakumbushe uzuri wa JF nao ni kutunza kumbukumbu. Tumewahi kujadili sana hizi mada za kidini zinazoanzishwa na Mohamed Said pamoja na FaizaFoxy (utadhani ni mapacha wa kufikia). Uzushi katika hizo mada ni mwingi sana k.m. Waislamu eti ndio walimfundisha Baba wa Taifa kuvaa suruali.

Ningekuwa mod hizi mada za chuki zinazoanzishwa na hawa wafia dini kwa lengo la kuwagawa Watanzania kidini ningezipiga marufuku au kuzihamishia jukwaa la dini. Huko sisi wengine wala hatuingii kwani dini ni imani na kuchanganya dini na siasa ni kuleta mtafaruku usokuwa lazima. Kwa kuanzia mleta mada anafaa kupewa ban ya mwaka!

Kwa wageni hebu pitieni hizi thread mbili zilizowahi kujadiliwa humu...

Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa

Uchochezi wa Mohamedi Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar
 
Allah and yehova/jesus is nothing but foreign fraud
 
Hadi huko misikitini wanaburn CD's na kusambaza zinazohamasisha chuki na hizo habari za uongo mtupu.
 
KILIKUWA SO WHAT? NA KWA NINI MTU APINGE? SIONI SABABU HATA KIDOGO.SO PIA SIONI TOFAUTI YOYOTE.
 
TANU hakikuwa chama cha Kiislamu Bali kilikuwa na wafuasi wengi wa dini ya Kiislamu.
Usipotoshe Mzee.
 
Dada yangu nina share na wewe mambo mengi sana lakini hili la udini hapana. Waislam na wakristo wa tanganyika/Tanzania walisukumwa na kitu kimoja tu, uhuru wa kujiamria mambo yao ndani ya nchi yao waliyopewa na Mwenyezi. Waliokuwa na agenda ya dini hawakuwa watanganyika bali wakoloni pia. Waislam wa kweli na wakristo wa kweli walitaka uhuru na siyo uislam au ukristo. Ukristo na uislam sio utanganyika! Ni imani aliyonayo mtanganyika mmoja mmoja. Kwa maneno mengine hakuna muislam wala mkristo asiye mtanganyika ambaye aliguswa na swala la kuwa huru. Ukristo na uislam haukuwa hapa na unapatikana kokote duniani. Utanganyika unapatikana tanganyika pekee. Hata tukifuta uislamna ukiristo utanganyika unabaki. Acha kutuchanganya maana wanasiasa uchwara huficha ajenda zao kwenye udini na ukabila nothing else.




 
Mag3,
Unaandika huku umeghadhibika na ukiwa na hamaki hata akili haiwezi
kufikiri vyema hadi umetulia.

Historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika ambayo ndiyo historia yake
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere iliandikwa na waandishi wengi
kabla yangu - Kimambo, Kandoro, Barongo, Chuo Cha CCM Kivukoni na
watafiti wa nje halikadhalika.

Bahati mbaya historia hizo ilikuwa na upungufu mkubwa sana na ndipo mimi
nikaiandika historia hii kwa kutumia Nyaraka za Sykes ambao historia yao
katika siasa za Waafrika wa Tanganyika zinaanza mwanzoni karne ya 20 na
ndiyo waliokuwa mstari wa mbele katika kuasisi TANU na harakati dhidi ya
ukoloni wa Muingereza.

Watafiti walionitangulia mimi hakuna aliyepata fursa ya kuzisoma nyaraka hizi
wala kuwahoji wenye nyaraka hizi.

Kitabu kilipotoka mwaka wa 1998 hakika kiliwashtua wengi kwa kule kutambua
kuwa historia waliyokuwa wakiiamini kuwa ndiyo historia ya kweli ya TANU na
uhuru wa Tanganyika ilikuwa na mashimo mengi yasiyo na hesabu.

Matokeo yake kitabu kilipata review tatu kutoka mabingwa wa African History
kwenye Cambridge Journal of African History waandishi wakiwa John Iliffe,
Jonathan Glassman na James Brennan.

The East African Magazine (Nairobi) ikatoa ''serialisation'' tatu za kitabu
Business Times nao pia wakaandika '' review,'' ya kitabu hiki.

Haya nishayaeleza huko nyuma lakini nayarudia kwa kuwa somo hili kila
siku linavutia wasomaji wapya.

Kubwa katika yale yanayoshughulisha akili za wengi ni mchango wa Waislam
katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Hiki ndicho kinachomuunguza Mag3.

Kitabu kina kwenda toleo la nne Kiswahili na la tatu Kiingereza.

Mag3 historia hii si santuri inayochuja hii ni mfano wa picha ya ''Mona Lisa,'' au
ukipenda sawa na nyimbo, ''Besame Mucho.''

Kutokana na kitabu hiki nikatiwa katika mradi wa vitabu vya historia kwa mashule
chini ya Oxford University Press Nairobi na nikaandika kitabu kimoja: ''The Torch
on Kilimanjaro,'' na nikashirikishwa kwenye mradi mwingine, Dictionary of African
Biography (DAB) Oxford University Press, New York mradi chini ya Harvard.



Hawa wote hawakuona udini ila Mag3.

Kutokana na kusahihisha historia ya uhuru wa Tanganyika nimealikwa kwingi duniani
kuzungumza pamoja na Northwestern University, Marekani wanaoongoza duniani
katika African History.

Hawa wote hawakuona udini ila Mag3.
Mag3
anaita haya porojo na ngano na udini.

Mag3 anadhani yeye anajua kushinda hawa wote wanaonitandikia busati kwao nikae
nizungumze na wataalamu wao achilia mbali wachapaji vitabu (publishers) waliotoa
vitabu nilivyoandika.

Kuna mengine sikuyajibu kwani hayana maana na mimi siwezi kukosa adabu kuandika
matusi na kashfa.
 
Unaweza ukawadanganya wachache muda wote,
Unaweza ukawadanganya wengi mara moja moja,
Lakini huwezi ukawadanganya wote nyakati zote.
Bahati mbaya mimi hunidanganyi hata mara moja, alamsiki.
 
Waislam tafsirini kwanza Quran isomwe kwa Kiswahili, ili watu wengi waisome vizuri na kuielewa sio kukariri maneno ya kiarabu bila kujua kwa undani Zaidi, kwa nini miaka yote hata mmesoma vizuri na mmelimika bado mnatumia lugha ya kiarabu katika masomo yenu? tofauti na wakristo, ambapo hutumia lugha rahisi inayowazunguka kusoma kuelewa bible, na kuwa na uwezo wa kulogic hata kitu kilichoandikwa, sidhani kama kuiweka Quran kwa Kiswahili nayo ni dhambi.

Kuhusu mjadala huu umekaa kidini sana kukiwa na lengo la upande mmoja kulaumu upande mwingine, kumbukeni kuwa waksiku zote mafundisho yao ni ya kistaraabu Zaidi, ndio manaa mahali popote kwenye watu wengi wakristo Amani ni kubwa, mfano tu hapa Tanzania ukiangalia uwiano wa wakristo na waislam utajua, lakini wakristo hujishusha na kusihi vizuri na waislam, lakini kama waislam wangekuwa wengi nchi ingechimbika, dini ya kiislam hisia ni nyingi kuliko uhalisia, halafu mambo mengi ni ya zamani na ndoto nyingi hayo masomo ya kale ya kina musa ukiyafuatilia sana unaweza mkata panga hata mwanao, hata kwenye ukristo yako lakini yalibadilika baada ya yesu kuja, sisemi kuwa muyatupilie mbali lakini u have rights question, waislam hamuwezi kuuliza hilo ila wakristo wanaweza, ndio maana wakristo wengi hujua hili neo ni kweli au fake.
 
Sasa ilikuaje Chama cha Kiislam kiongozwe na Mkristu? tena mkamwachia aongoze na nchi..... Ni ajabu.

Inamaana ao babu zetu wa kiislam awakua na mtu wa kuongoza? Au awakua na Wasomi?

Siku tutaambia Nyerere Alislim Nyumban kwa Mtenvu.....!
Amulewek sijui mnaitaji nini? Kama ni swala la kupigania uhuru ata Babu zetu pia walipigania uhuru uko walipokua.
 
Unaweza ukawadanganya wachache muda wote,
Unaweza ukawadanganya wengi mara moja moja,
Lakini huwezi ukawadanganya wote nyakati zote.
Bahati mbaya mimi hunidanganyi hata mara moja, alamsiki.
Mag3,
Alamsiki bi nur.

Mimi nina uwezo wa kuidanganya Harvard, Northwestern University,
University of Iowa, Oxford University Press kutaja wachache?

Unachomwa kuona kama ulidhani Waislam hamna kitu unasoma
historia yao walivyokuwa bega kwa bega na Mwalimu Nyerere hadi
uhuru ukapatikama 1961.

Ulikuwa hujasikia historia ya Abdul Sykes wala baba yake.

Historia hii mbali ya kuwavutia wasomaji wengi duniani imewashangaza
Watanzania wote.
 
Hope you have some Undiagnosed mental illness my sister. Isn't it? Prove it with concrete examples.
 
Faiza Foxy yuko wapi ajibu hoja za wadau humu ndani?
 
unaona raha gani kudanganya kuhusu historia ya uhuru!?..unaweka fikra pembeni kisa imani!..kuhusu bunge mwaka 2000 baada ya waislam wengi kushinda kura za maoni ubunge,mchakato ukarudiwa kwa hoja zisizo na mashiko,makada wa msalaba walifurahi na kutamba kwamba tumewafyeka waislam,hebu tupe takwimu za dini bungeni
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…