Hii santuri imechuja...kila baada ya muda watu wale wale, fikra zile zile, porojo zile zile, malalamishi yale yale, na ngano zile zile
starring wafia dini
Mohamed Said na
FaizaFoxy. Mwaka kesho bila shaka hadithi nyingine kama hii itatungwa na safari hii si ajabu ikapewa jina lingine kama;
Mwalimu Nyerere alifuta shule zote za Waislaam na kubakiza za Wakristo tu! Yaani hawa watu wawili wametia fora kwa kuwalisha vijana wa leo matango pori na wao huitikia tu hewala na kumeza tu kama misukule vile!
Kwa walioingia Jamii Forums majuzi tu naomba niwakumbushe uzuri wa JF nao ni kutunza kumbukumbu. Tumewahi kujadili sana hizi mada za kidini zinazoanzishwa na
Mohamed Said pamoja na
FaizaFoxy (utadhani ni mapacha wa kufikia). Uzushi katika hizo mada ni mwingi sana k.m.
Waislamu eti ndio walimfundisha Baba wa Taifa kuvaa suruali.
Ningekuwa mod hizi mada za chuki zinazoanzishwa na hawa wafia dini kwa lengo la kuwagawa Watanzania kidini
ningezipiga marufuku au kuzihamishia jukwaa la dini. Huko sisi wengine wala hatuingii kwani dini ni imani na kuchanganya dini na siasa ni kuleta mtafaruku usokuwa lazima. Kwa kuanzia mleta mada anafaa kupewa ban ya mwaka!
Kwa wageni hebu pitieni hizi thread mbili zilizowahi kujadiliwa humu...
Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa
Uchochezi wa Mohamedi Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar
Mag3,
Unaandika huku umeghadhibika na ukiwa na hamaki hata akili haiwezi
kufikiri vyema hadi umetulia.
Historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika ambayo ndiyo historia yake
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere iliandikwa na waandishi wengi
kabla yangu -
Kimambo, Kandoro, Barongo, Chuo Cha CCM Kivukoni na
watafiti wa nje halikadhalika.
Bahati mbaya historia hizo ilikuwa na upungufu mkubwa sana na ndipo mimi
nikaiandika historia hii kwa kutumia
Nyaraka za Sykes ambao historia yao
katika siasa za Waafrika wa Tanganyika zinaanza mwanzoni karne ya 20 na
ndiyo waliokuwa mstari wa mbele katika kuasisi TANU na harakati dhidi ya
ukoloni wa Muingereza.
Watafiti walionitangulia mimi hakuna aliyepata fursa ya kuzisoma nyaraka hizi
wala kuwahoji wenye nyaraka hizi.
Kitabu kilipotoka mwaka wa 1998 hakika kiliwashtua wengi kwa kule kutambua
kuwa historia waliyokuwa wakiiamini kuwa ndiyo historia ya kweli ya TANU na
uhuru wa Tanganyika ilikuwa na mashimo mengi yasiyo na hesabu.
Matokeo yake kitabu kilipata review tatu kutoka mabingwa wa African History
kwenye Cambridge Journal of African History waandishi wakiwa John Iliffe,
Jonathan Glassman na James Brennan.
The East African Magazine (Nairobi) ikatoa ''serialisation'' tatu za kitabu
Business Times nao pia wakaandika '' review,'' ya kitabu hiki.
Haya nishayaeleza huko nyuma lakini nayarudia kwa kuwa somo hili kila
siku linavutia wasomaji wapya.
Kubwa katika yale yanayoshughulisha akili za wengi ni mchango wa Waislam
katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Hiki ndicho kinachomuunguza
Mag3.
Kitabu kina kwenda toleo la nne Kiswahili na la tatu Kiingereza.
Mag3 historia hii si santuri inayochuja hii ni mfano wa picha ya ''Mona Lisa,'' au
ukipenda sawa na nyimbo, ''Besame Mucho.''
Kutokana na kitabu hiki nikatiwa katika mradi wa vitabu vya historia kwa mashule
chini ya Oxford University Press Nairobi na nikaandika kitabu kimoja: ''The Torch
on Kilimanjaro,'' na nikashirikishwa kwenye mradi mwingine, Dictionary of African
Biography (DAB) Oxford University Press, New York mradi chini ya Harvard.
Hawa wote hawakuona udini ila
Mag3.
Kutokana na kusahihisha historia ya uhuru wa Tanganyika nimealikwa kwingi duniani
kuzungumza pamoja na Northwestern University, Marekani wanaoongoza duniani
katika African History.
Hawa wote hawakuona udini ila
Mag3.
Mag3 anaita haya porojo na ngano na udini.
Mag3 anadhani yeye anajua kushinda hawa wote wanaonitandikia busati kwao nikae
nizungumze na wataalamu wao achilia mbali wachapaji vitabu (publishers) waliotoa
vitabu nilivyoandika.
Kuna mengine sikuyajibu kwani hayana maana na mimi siwezi kukosa adabu kuandika
matusi na kashfa.