Mohammed Dewji ajiuzulu Uenyekiti wa Bodi ya simba, amteua Salim Abdallah (Try Again) kuchukua nafasi yake

Mohammed Dewji ajiuzulu Uenyekiti wa Bodi ya simba, amteua Salim Abdallah (Try Again) kuchukua nafasi yake

Uko sahihi mwanaume anasusa Susa nini, mara mabifu ya wachezaji anawauza Hadi kuathiri team, Bora aondoke tu ikiwezekana Simba ilikuwepo kabla yake na itaendelea kuwepo aanzishe tu team yake mpya bana, mambo yake ya ajabu yanaathiri team
Kwa sasa bado tunamuhitaji mihemko tuweke pembeni. Hakuna mwekezaji kw sasa la sivyo tutapoteana kama ma utopolo kipindi kile Manji alivyosepa
 
Mohammed Dewji amesema kikao walichokaa Septemba 21, 2021 kuwa asiendelee kuwa Mwenyekiti wa Simba Sc kutokana na safari zake za kibiashara kuwa nyingi

Hata hivyo amesema anaendelea kuwa mwekezaji katika klabu ya SImba huku akiahidi kushirikiana vizuri na viongozi watakaoendelea kuwepo

Kwa sasa Kaimu Mwenyekiti ni Said Abdallah Muhene A.K.A Try Again ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Simba
Sijawahi sikia popote anayejiuzulu akiteua wa kumwachia nafasi yake.
Sijui kwanini Wana Simba wenzangu tumekuwa wapumbavu kiasi hiki.
[emoji51][emoji51][emoji51][emoji51][emoji51]
 
Aibu ipi?!!..Kwani kachukua fedha zake?!!..Yeye ni Mwekezaji na Mwanachama!!..
Nimegundua hata humu JF kuna watu upeo wa kufikiri na kuchambua mambo ni mdg sana. Wengi wanaongea kwa kufata mkumbo but not Facts. Yani wasichoelewa hapo ni nini? Mo ni mwekezaji na bado ni mwanachama. Leo hii Rais akihudumu miaka 30 wanasema dictator akijiuzulu wamasema dhaifu.
 
Hahaha
Screenshot_20210929-142058.jpg
 
Mohammed Dewji amesema kikao walichokaa Septemba 21, 2021 kuwa asiendelee kuwa Mwenyekiti wa Simba Sc kutokana na safari zake za kibiashara kuwa nyingi
Yaani tangu Rage aseme mashabiki wa Simba mbumbumbu, basi Braza Mudi anapenda sana kutembelea hiyo kauli....

Ina maana anataka kutuambia yeye ana safari nyingi sana za kibiashara kumzidi Khaldoon Al Mubarak wa Man City?!

Ukisikia chupli chupli anayoisema Manara, ndo hii sasa!!
 
Luc ni kocha alifundisha yanga hapa karibuni.

Wakati anaondoka alisema mashabiki wa yanga ni kama mbwa au Nyani, wanabweka bweka tu na kuzomea.....hawana uelewa wowote juu ya mpira.
Sawa asante mkuu ndo nimeelewa
 
Kigwangala alijaribu kusanua usanii wa mwamedi mapema, mbumbumbu wakasimama na mwamedi na kumchamba Hamisi mapikipiki badala ya kuchambua hoja na kutafuta ukweli ni upi...........haya ponjoro amelala mbele atakuwa anawacheki mnavyotafutana.
 
We jamaa unajiskia unachoongea kweli??
Simba ya miaka hiyo ilikua inajulikana kvp kimataifa kama sasa!!?
Unafananisha jina la simba kimataifa kwasasa na zamani!?
Kwaheri πŸ™ŒπŸ™Œ
Aisee kwa hii comment sijui una umri gani! Simba imetambulika kimataifa zaidi wakati wa mwamedi!! My ribs....
 
Sio kwamba anawekeza simba bila kuwa na maslahi. Kabla ya MO simba ilikuwepo na baada yake itakuepo.

Hakuna anayemchukia hata kwa anayoyafanya ila na yeye atambue simba ina mashabiki na wapenzi ambao hawezi kuwakwepa.

Kama hataki maneno aanzishe team mpya kabisaaaaa iwe mali yake binafsi

Maana kama anakereka atashindwa kuistawisha team na zaidi ataididimiza.... Angondoka kabisa ili wenye nia waingie na kufanya kazi na Simba
Mm Ni Simba lkn Simba walifanya makosa hisa zote 49 kumpa Mo pekee, wangekuwa km wawekezaji wawili au watatu
 
Mohammed Dewji amesema kikao walichokaa Septemba 21, 2021 kuwa asiendelee kuwa Mwenyekiti wa Simba Sc kutokana na safari zake za kibiashara kuwa nyingi

Hata hivyo amesema anaendelea kuwa mwekezaji katika klabu ya SImba huku akiahidi kushirikiana vizuri na viongozi watakaoendelea kuwepo

Kwa sasa Kaimu Mwenyekiti ni Said Abdallah Muhene A.K.A Try Again ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Simba
Simba inaelekea pabayaaaa
 
Aisee kwa hii comment sijui una umri gani! Simba imetambulika kimataifa zaidi wakati wa mwamedi!! My ribs....
Doh inavyoonekana hata darasan ktk mtihan ulikua husomi maswali ukayaelewa.
Nakusihi acha kukurupuka.
πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ KWAHERI.
 
Back
Top Bottom