Mohammed Said na Mapinduzi ya Zanzibar

kmbwembwe

Mambo kadhaa mapya yalisababisha kuongezeka mahitaji ya watumwa kutoka Afrika ya Mashariki wakati wa karne ya kumi na tisa. Katika eneo la mamlaka la pwani ya Ureno, palikuwepo na ongezeko la juu sana katika biashara ya utumwa kwenda Brazil. Hii ilisababishwa na kuondolewa kwa familia ya kifalme ya Kireno kutoka Lisbon kupelekwa Brazil wakati wa Vita za Napoleon. Ruhusa maalum zilitolewa kwa Wabrazil na mara biashara inayoshamiri katika watumwa ikawa inaendeshwa kupitia Rasi ya Tumaini Jema huko Afrika ya kusini.


“Sasa ni ukweli unaokubalika miongoni mwa wataalam wa historia makini wa Afrika ya Mashariki kwamba njia ndefu za biashara kati ya bara na pwani zilianzishwa hasa zaidi kwa kutumia ujasiri na moyo wa kujituma wa Waafrika. Kwa maneno mengine njia za biashara zilibuniwa na Waafrika kutoka bara kwenda pwani, wala si Waarabu, au Waswahili, ambao walisafiri kutoka pwani kwenda bara kupitia sehemu zisizojulikana.


Wafanya biashara wa Kiswahili walianza tu kutelekeza usalama wa pwani mnamo nusu ya pili ya karne ya kumi na nane, na walisafiri kufuata njia safi ambazo ziliendelezwa kwa miongo mingi kabla yake. Ni baada tu kuanza karne ya kumi na tisa ndipo wafanya biashara wa Kiarabu walijasiri kufuata njia hiyo.”


Wayao ambao walikuja kuwa wafanya biashara makini sana wa Kiafrika wa biashara ya watumwa katika Afrika ya Mashariki, hivyo walikuwa na desturi ya muda mrefu ya kubeba pembe za ndovu na bidhaa zingine halali kwenda pwani miongo mingi kabla ya mahitaji ya pamoja ya Wafaransa na Waarabu kutaka watumwa yalipoeleweka.”


“Katika Afrika Magharibi njia hizi ziliendeshwa kwenda bara kutoka pwani na Waafrika ambao kazi yao hasa ilikuwa kutafuta watumwa. Watumwa walitawala biashara ya Afrika ya Magharibi tangu mwanzo. Katika Afrika ya Mashariki wala hapakuwepo na hali zilizolingana na hiyo. Biashara ya watumwa lazima ionekane kuwepo katika mazingira ya mapema zaidi, iliyokwishajengeka kwa umakini, na biashara yenye faida ya masafa marefu ambayo chimbuko lake ilikuwa ubebaji wa pembe za ndovu. Hii ni muhimu kukumbuka hasa kwa mikoa ya kusini ambalo kila mara ilikuwa hazina kuu ya “Biashara ya Utumwa katika Afrikamashariki.”
 
kmbwembwe


Bwana Alpers anahitimisha, “lazima iwe wazi sasa kwamba fikira ya zamani inayotamkwa kiholela kwamba wengi wa watumwa walikamatwa na wafanya biashara wanyang’anyi wa Kiarabu na Kiswahili ni moja wapo ya mambo ya kubuniwa na ngano tu ambazo zimekuzwa kuhusu biashara ya watumwa ya Afrika mashariki. Lakini lazima tuwe waangalifu tusifanye kosa la kutoa tathmini potofu kuhusu mchango waliotoa watu hawa kwenye biashara hii.”


Kwa mara nyingine, lazima nisisitize kwamba lengo langu si kudhihaki juhudi za kundi dogo la waadilifu ambao walikuwa wanashughulika na propaganda dhidi ya utumwa. Ninachotaka kuonyesha ni kwamba juhudi zao hazikufaulu (na hazingefaulu) hadi pale shinikizo la kiuchumi lilipoilaz- imisha kwanza Uingereza ilipolazimika kufuatana na matatizo ya kiuchumi kuanza kuzuia utumwa, biashara ya utumwa na halafu kukomesha utumwa.


Kwa kweli, Uingereza ilipojitokeza kwa ajili ya kutaka kukomesha utumwa haikusimama kwenye mapaa ya nyumba na kutangaza kwamba ilikuwa inakomesha utumwa kushindana dhidi ya wenye viwanda wa Kifaransa. Uingereza ililigeuza jambo hili kuwa suala la kimaadili na kiunyofu kabla haijatumainia kushinikiza serikali zingine kufuata mpango wake. Na ilifanya hivyo. Tunatambua jinsi Uingereza ilivyoanzisha vita si kwa lengo la kulinda maslahi ya himaya yake kiuchumi na kisiasa, lakini ilifanya hivyo ili “kulinda Uhuru wa Watu.”


Ndivyo ilivyokuwa kuhusu vita yake dhidi ya utumwa. Murua na maadili mema lilikuwa suala la waadilifu wachache tu ambao hawakuwa na uwezo. Suala halisi, kama serikali mbali mbali na walowezi na wakoloni walivyohusika, lilikuwa kuhusu uchumi.


Ref.


  • Alpers, op. cit., uk. 5-6
  • 2. Ibid uk. 7-8.
  • 3. Ibid, uk. 13.
  • 4. Bid, uk. 14.
  • 5. Ibid uk. 15.
  • 6. Ibid uk. 24.
 
kmbwembwe



Wakristo Wanapanga Biashara Ya Utumwa​


Watumwa walikuwa wanachukuliwa kutoka hata katika wakati wa Ufalme wa Kirumi, lakini “biashara halisi ya Utumwa” ilianza mnamo karne ya 16 baada ya ujio wa mataifa ya Kikristo ya Ulaya.

Edward A. Alpers wa Chuo Kikuu cha Dar-es Salaam, anaandika kwamba; “kama tunavyoleta utofautisho baina ya biashara inayoambatana katika watumwa ambayo ilichuruzika katika sahara kutoka magharibi mpaka kaskazini ya Afrika kuanzia siku za nyuma sana za wakati wa utawala wa Ufalme wa Kirumi, kwa upande mmoja, na kioja tunacho kiita The West African Slave Trade kwa upande mwingine, kwa hiyo lazima tulete tofauti hiyo hiyo kwa Afrika ya Mashariki.”

Walter Rodney pia wa Chuo, Kikuu cha Dar es Salaam, anaanza kuandika kijitabu chake “West Africa and the Atlantic Slave-Trade kwa maneno yafuatayo: - Wakati wote lazima ikumbukwe kwamba biashara ya utumwa iliyo;fanyi- ka katika bahari ya Atlantiki” lilikuwa ni tukio katika histo- ria ya dunia, iliyo husisha mabara matatu – Ulaya, Afrika na Marekani.

Watu walio toka kwa dhamira ya kutafuta watumwa walikuwa Wazungu waliotoka katika kila nchi kati ya Sweeden kwa upande wa Kaskazini na Ureno kwa upande wa magharibi. Wareno walifika Afrika ya Magharibi muda mfupi kabla ya kuingia nusu karne ya kumi na tano. Mara moja na kwa haraka sana walianza kukamata (watumwa) Waafrika na kuwapeleka kufanya kazi Ulaya kama watumwa, hususan katika Ureno na Hispania.

Lakini maendeleo muhimu sana kwa biashara hii ya utumwa yalikuwa katika karne ya kumi na sita, ambapo mabepari wa Kizungu walitambua kwamba wangepata faida kubwa sana kwa kutumia nguvukazi ya Waafrika kuujenga na kuuendeleza utajiri wa nchi zote za Amerika.

Matokeo yake, Waafrika walipelekwa Amerika ya kaskazini, Amerika ya kati, Amerika ya kusini na Visiwa vya Caribbean kwa ajili ya kukidhi haja ya nguvukazi ya watumwa kwenye machimbo ya dhahabu na shaba, na kwenye mashamba ya kilimo cha mazao ya miwa, pamba na tumbaku. Biashara hii mbaya ya kununua na kuuza binadamu ilidumu kwa kipindi cha miaka (400) mia nne, kwani Atlantic slave-Trade (Biashara ya Utumwa wa kupitia bahari ya Atlantiki) ilikoma mwishoni mwa miaka ya 1870.

“Mambo mengi yanaweza kusemwa kuhusu jinsi Biashara ya Utumwa katika bahari ya Atlantiki ilivyopangwa huko Ulaya, na kuhusu faida kubwa iliyokusanywa na nchi kama Uingereza na Ufaransa. Mambo mengi yanaweza kusemwa kuhusu safari za kutisha kutoka Afrika hadi Marekani kuvu- ka bahari ya Atlantic. Waafrika walipangwa kama dagaa kwenye meli za kubeba watumwa, na matokeo yake walikufa wengi sana.”

Na dagaa walioje! Kwa maelezo zaidi kuhusu upakiaji huu wa watumwa kwenye meli, soma taarifa ifuatayo: - Moja ya hati yenye kuuvunja moyo sana katika nyaraka zote zinazotisha ni “Plan of the Brookes,” mpango mbaya sana wa karne ya kumi na nane wa kupanga watumwa kwenye meli ya kubeba watumwa ‘Brookes’… Kwa mahesabu sahi- hi, teknolojia ya kushtua ilitengenezwa - futi na inchi, chumba cha kusimama na nafasi ya kupumua iliwekwa kwa matumaini ya faida kubwa. Mtu mmoja Bwana Jones anapendekeza kwamba wanawake watano wahesabiwe kama wanaume wanne, na wavulana watatu au wasichana watatu wafanywe kuwa sawa na watu wazima wawili … kila mtumwa mwanaume aruhusiwe futi sita kwa futi moja na inchi nne (1’4”x6’) kama nafasi ya chumba chake, kila mwanamke alipewa nafasi ya upana wa futi tano na inchi kumi na futi moja na inchi nne…. (5’10”x1’4”); na inaendelea hivyo mpaka kila mtu anapata nafasi – watumwa 451.

Lakini Muswada wa Bunge unaruhusu watumwa 454. Kwa hiyo hati hiyo inahitimisha kwamba kama watumwa watatu zaidi wangeweza kuwekwa kwa kubanwa katikati ya wale waliotamkwa kwenye mpango, mpango huu ungeweza kuchukua idadi ile ile ambayo imeelekezwa kwenye muswada.3
Mara Waafrika walipofikishwa upande mwingine wa bahari ya Atlantic, kwa hakika walikuwa katika “Dunia Mpya”, iliyojaa ukandamizaji na ukatili. Taarifa ifuatayo inaweza kusaidia kuelewa hali ilivyokuwa wakati huo. Rodney anaandika:

“Kuanzia wakati walipofika (Wakristo) Wazungu hadi 1600, takriban Waafrika milioni moja (1, 000,000) walichukuliwa kwenye meli za kubeba watumwa. Wakati wa kipindi hicho, Wareno walikuwa ndio wafanya biashara wakuu wa biashara ya watumwa huko Afrika ya Magharibi. Ama wali- wapeleka Waafrika huko Brazil, ambayo nchi hiyo ilikuwa koloni lao, au vinginevyo waliwauza kwa waloezi wa Kihispania huko Mexico, Amerika ya kati, Amerika ya Kusini na visiwa vya Caribbean. Mnamo karne ya kumi na saba, kiasi cha Waafrika wapatao milioni saba hadi nane kutoka Afrika ya magharibi walivushwa bahari ya Atlantic.

Wadachi walijumuika na Wareno kama wafanya biashara wakuu wa biashara ya utumwa mnamo karne ya kumi na saba, na karne iliyofuata Waingereza wakawa wafanya biashara wakubwa kushinda wote wa biashara ya utumwa. Wakati biashara ya Utumwa katika bahari ya Atlantiki ilipofikia kileleni mnamo karne ya kumi na nane, meli za Kiingereza zilikuwa zinachukua zaidi ya nusu ya jumla yote ya watumwa na idadi iliyobaki iligawanywa baina ya Wadachi, Wafaransa, Wareno na Wadane (Danish).

“Ilipofika karne ya kumi na tisa, palikuwepo na mabadiliko mengine ya watu ambao walishika nafasi mbele katika kuinyonya Afrika. Nchi za Ulaya zenyewe hazikushiriki kikamilifu kwenye biashara ya utumwa, lakini badala yake Wazungu ambao waliloea Brazil, Cuba, na Amerika ya Kaskazini ndio ambao walipanga sehemu kubwa ya biashara. Waamerika (U.S.A) ndiyo katika kipindi hicho hicho tu walipata uhuru kutoka kwa Waingereza, hili lilikuwa taifa jipya (U.S.A.) ambalo lilikuwa na mgawo mkubwa kabisa kuliko wote katika biashara ya watumwa katika biashara ya Atlantiki katika kipindi cha miaka hamsi- ni ya mwisho, kwa kuchukua kiwango kikubwa zaidi cha watumwa kuliko ambavyo imewahi kufanya huko nyuma.

“Ilipoanza “biashara ya watumwa ya Atlantiki kwenye pwani ya Afrika ya Magharibi, ilichukua utaratibu wa kutu- mia nguvu moja kwa moja wa Wazungu kuwashambulia Waafrika waliokuwa wanaishi karibu na pwani. Mabaharia wa kwanza wa Kireno walipofika kwenye pwani inayoju- likana leo kama Mauritania, waliacha meli zao na kuanza kuwawinda watu waitwao, Moors watu walioishi katika jimbo hilo. Kwa kweli, hii haikuwa biashara hata kidogo – ilikuwa uvamizi wa nguvu. Hata hivyo, baada ya mashambulizi kadhaa ya kushtukizwa, Waafrika wa pwani wakawa na kawaida ya kulinda kwa zamu na walijilinda kwa nguvu dhidi ya washambuliaji wao Wazungu.

Katika kipindi kifupi tu, Wareno walitambua kwamba uvamizi haikuwa mbinu inayofaa na iliyo salama katika kujaribu kuwapata watumwa. Zaidi ya hayo, pia walitaka dhahabu na bidhaa zingine za Kiafrika, ambazo wangeweza tu kuzipata kwa njia ya kununuliana na kuuziana kwa amani. Kwa hiyo badala ya kuvamia, Wareno waliona afadhali kutumia bidhaa zilizo tengenezwa kiwandani ili kuwatia moyo Waafrika kubadilishana na bidhaa zao na hata kuweza kuwafikisha mateka wa Kiafrika kwenye meli za Wazungu kwa urahisi. Mpango huu haukufanywa na Wareno pekee, lakini hata wazungu wengine wote walitambua na kukubali kwamba huo ulikuwa mpango mzuri zaidi wa kupata bidhaa hapa Afrika; na ilikuwa kwa njia hii waliweza kupata mamilioni ya watumwa
 
Mzee wangu ila unyama walioufanya walowezi wa kiarabu kwa karne nyingi haukuacha makovu kwa mababu zetu wa kibantu????
Nelson...
Una hakika na hayo au unafanya rejea za propaganda za wamishionari?

Hadithi za kuzika watu hai nguzo za Beit Al Ajaib?
 
Nelson...
Una hakika na hayo au unafanya rejea za propaganda za wamishionari?

Hadithi za kuzika watu hai nguzo za Beit Al Ajaib?
Kwahiyo mzee wangu ni walowezi wa kizungu na wamishionari tu ndio walikua na propaganda ila walowezi wa kiarabu na vizazi vyao vya machotara hawakua na propaganda mzee wangu????
 
Ni kama vile vile makhalifa wa kiislamu walivyoeneza utumwa bara asia!!!Au wewe hujui hilo kaka???
 
Jemshid ni mlowezi tu na alizaliwa na walowezi!!!!!Kuhusu watu waliodhulumiwa na walowezi wabaguzi wa zanzbar unazungumzia wakati wa jemshid au hao maslutani walowezi wa kabla yake?????Unataka tuanzie wapi kufahamishana kaka
Nelson...
Hakuna Sultan alyeua raia au kuweka kundi la watesaji katika utawala wa Zanzibar.

Hakuna historia hii.
 
Kwahiyo mzee wangu ni walowezi wa kizungu na wamishionari tu ndio walikua na propaganda ila walowezi wa kiarabu na vizazi vyao vya machotara hawakua na propaganda mzee wangu????
Nelson...
Kama unao ushahidi wa dhulma ya watu kupigwa na kuteswa tuwekee.
 
Nelson...
Hakuna Sultan alyeua raia au kuweka kundi la watesaji katika utawala wa Zanzibar.

Hakuna historia hii.
Naona unajitahidi kuwatetea walowezi wa kiarabu!!!Basi mzee wangu hao walowezi walikua watu bora kabisa nasikia walikua wanawagawia mababu zetu tende na kaniki na kuwafundisha waache ubantu ni ushenzi!!!!!Sawa mzee wangu sultana na vizazi vyao vya machotara walikua watu wa haki kabisa!!!!!!Upo sahii mzee wangu na mapinduzi 1964 ni haramu kabisa kwa kua akina okelo walikua makafir
 
Gavana,
Ndugu zetu wamejaa chuki dhidi ya Uislam inayotisha sana.

Angalia walivyojaribu kufuta historia ya Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Hawa ni wa kuandika historia ya Julius Nyerere ndani ya TANU wasimtaje Abdu Sykes?

Hajafanya utafiti wowote wala hana hata makala fupi aliyoandika.

Hana ajuacho masikini ya Mungu si yeye wala wengine.

Leo mimi nawasomesha historia ya Tanganyika upya na kila niandikalo kwao ni geni hawakupata kusoma wala kusikia.

Ila tusiwaache wakaeneza uongo kama ule wa historia ya TANU.

Tuwajibu mpaka siku ya kiama.
 
Nelson...
Kama unao ushahidi wa dhulma ya watu kupigwa na kuteswa tuwekee.
Dhuluma za waarabu ushahidi hauna ila dhuluma za ASP ushahidi unao!!!!Sawa mzee wangu walowezi wa kiarabu walikua watu bora zaidi kuliko babi zetu akina mzee karume
 
Mbona wewe historia ya kupigania uhuru wa tanganyika kwa wakristo unajitahidi kuifuta????Wewe mzee wangu una chuki binafsi na mzee wetu karume na nyerere na chama chetu cha ASP na TANU!!!!Kwa kua wazee wenu wa kariakoo walikosa nafasi za madaraka
 
Dhuluma za waarabu ushahidi hauna ila dhuluma za ASP ushahidi unao!!!!Sawa mzee wangu walowezi wa kiarabu walikua watu bora zaidi kuliko babi zetu akina mzee karume
Lete ushahidi wa Sultan Jemshid kumuuwa mtu au kumnajisi mtu au kumtia kilens mtu
 
Lete ushahidi watu wapate elimu , usipaparike na chuki zako
 
Dhuluma za waarabu ushahidi hauna ila dhuluma za ASP ushahidi unao!!!!Sawa mzee wangu walowezi wa kiarabu walikua watu bora zaidi kuliko babi zetu akina mzee karume
Wewe mwenye ushahidi mbona unazidi kuumia maoni, huuweki
 
Jibu swali langu kwanza huyo jamshid alikaa mda gani kwenye throne
Nilikujibu alikaa miaka 100

Huna isipokuwa chuki mara Waarabu ,mara Sultani mara machotara hamna chochote nyinyi vibaraka wa mkoloni muingereza . Nchi yote mumeichafua na watu kuwatia umasikini uliokithiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…