Gavana
JF-Expert Member
- Jul 19, 2008
- 33,637
- 8,947
kmbwembwe
Mambo kadhaa mapya yalisababisha kuongezeka mahitaji ya watumwa kutoka Afrika ya Mashariki wakati wa karne ya kumi na tisa. Katika eneo la mamlaka la pwani ya Ureno, palikuwepo na ongezeko la juu sana katika biashara ya utumwa kwenda Brazil. Hii ilisababishwa na kuondolewa kwa familia ya kifalme ya Kireno kutoka Lisbon kupelekwa Brazil wakati wa Vita za Napoleon. Ruhusa maalum zilitolewa kwa Wabrazil na mara biashara inayoshamiri katika watumwa ikawa inaendeshwa kupitia Rasi ya Tumaini Jema huko Afrika ya kusini.
“Sasa ni ukweli unaokubalika miongoni mwa wataalam wa historia makini wa Afrika ya Mashariki kwamba njia ndefu za biashara kati ya bara na pwani zilianzishwa hasa zaidi kwa kutumia ujasiri na moyo wa kujituma wa Waafrika. Kwa maneno mengine njia za biashara zilibuniwa na Waafrika kutoka bara kwenda pwani, wala si Waarabu, au Waswahili, ambao walisafiri kutoka pwani kwenda bara kupitia sehemu zisizojulikana.
Wafanya biashara wa Kiswahili walianza tu kutelekeza usalama wa pwani mnamo nusu ya pili ya karne ya kumi na nane, na walisafiri kufuata njia safi ambazo ziliendelezwa kwa miongo mingi kabla yake. Ni baada tu kuanza karne ya kumi na tisa ndipo wafanya biashara wa Kiarabu walijasiri kufuata njia hiyo.”
Wayao ambao walikuja kuwa wafanya biashara makini sana wa Kiafrika wa biashara ya watumwa katika Afrika ya Mashariki, hivyo walikuwa na desturi ya muda mrefu ya kubeba pembe za ndovu na bidhaa zingine halali kwenda pwani miongo mingi kabla ya mahitaji ya pamoja ya Wafaransa na Waarabu kutaka watumwa yalipoeleweka.”
“Katika Afrika Magharibi njia hizi ziliendeshwa kwenda bara kutoka pwani na Waafrika ambao kazi yao hasa ilikuwa kutafuta watumwa. Watumwa walitawala biashara ya Afrika ya Magharibi tangu mwanzo. Katika Afrika ya Mashariki wala hapakuwepo na hali zilizolingana na hiyo. Biashara ya watumwa lazima ionekane kuwepo katika mazingira ya mapema zaidi, iliyokwishajengeka kwa umakini, na biashara yenye faida ya masafa marefu ambayo chimbuko lake ilikuwa ubebaji wa pembe za ndovu. Hii ni muhimu kukumbuka hasa kwa mikoa ya kusini ambalo kila mara ilikuwa hazina kuu ya “Biashara ya Utumwa katika Afrikamashariki.”