Taasisi ya Mifupa-MOI
Senior Member
- Apr 15, 2025
- 118
- 214
Wauguzi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) washiriki Maadhimisho ya Siku ya Mkunga Duniani kwa kutoa elimu kwa wazazi jinsi ya kijikinga na watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi.
Maadhimisho hayo yanafanyika katika viwanja vya Fire mkoani Shinyanga, yenye kauli mbiu “Wakunga nguzo muhimu katika kila janga”.
Afisa Muuguzi wa MOI Catherine Rwegasila amesema katika maadhimisho hayo wametoa elimu kwa wazazi ya umuhimu wa kunywa dawa ya folic acid mapema kabla ya ujauzito na baada ya ujauzito ili kujikinga na watoto wanaozaliwa na kichwa kikubwa.
“ Tumeshiriki kwenye maashimisho ya siku ya mkunga duniani yalioanza tarehe 03 Mei na kilele chake ni 05, Mei 2025 ambapo tumetoa elimu kwa wazazi wa mkoani wa Shinyanga jinsi ya kutumia madini ya folic acid ili kujikinga wasipate watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi” amesema Rwegasila.
Aidha, Bi. Rwegasila amesema kupitia maadhimisho hayo wauguzi wa MOI wameongeza ujuzi wa kutoa huduma bora kwa mama mjamzito aliyepata ajali na jinsi ya kupatiwa matibabu bora ya mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu katika Taasisi ya MOI.