Moja kati vitu vilivyonishinda

Moja kati vitu vilivyonishinda

Kijana weka aibu na woga pembeni. Kwa level yako, muite mdada tena kwa kujiamini(kama mbwai n mbwai), msalimie, muangalie alivyo vaa harafu tatufa cha kumsifia mf "sketi yako nzuri imekupendeza sana" kama unamjua, mwambie siku hizi mambo yako mazuri nini, maana umenenepa. Hapo mtapiga blah blah blah mkatishe huku unamuangalia usoni mwambie "harafu mwenzako nakupenda kweli yani huwezi amini"..... hapo atajistua na mengineyo lakin wewe jazia nyama neno hilo hilo. Popote utakapo muona kama inafaa mfuate au muite akija mueleze, usiogope hata kuua.

Kwa kuongea ni rahisi mno lakini kutekeleza baba achaaa! Yana wenyewe ndugu yangu
 
Ivi karne hii bado kunakutongozana? Kutongozana kulikua enzi za miaka ya 80, unavizia dem jioni akiwa anaenda kuchukua maziwa kwa jirani unaunga tela, huku unatafuna big G na mikanda ya video ya VHS umeishika, manake enzi hizo ndo ilikua ujiko. Unasomesha miezi sita ndo unakula denda, then mwezi wa tisa unapewa kamoja ka juu juu, unawehuka unaenda hadithia washkaji kijiweni wanakuona kidume!

Sasa hivi kanyaga twende, unatanguliza uongo mwingi na chipsi yai na savannah mbili, unakula mzigo, kwaulaini sana.

Bahati ilio nzuri habari za ngono sinazo tena vinginevyo ningekua mhanda
 
Umekariri kutongoza ni kumwambia mwanamke nakupenda
kutongoza hata kumtazama tu na kutabasam inatosha
hata kumsalimia tu na kumuuliza kitu nayo ni kutongoza....

Wenzio hawasemi tena nakupenda....ni kusalimia tu na kuongea chochote kilichopo hapo
hata mpira au diamond na wema au watangaza nia wa ccm....
halafu taratibu unajisogeza
Naamini mleta mada atakuwa amechukuwa hizi notes muhimu
 
Mbona rahisi tuu kama kumsukuma mlevi.wew muanze hivi " dada mambo" atakujibu poa then muulize "shemeji mzima?" Asilimia nyingi hucheka na kusema " shemeji hayupooo" thn muulize tena "je akija" utasikia ohh "akija nitamfikiria" mwambie okey "basi nenda kanifikirie mimi"

Kaaa! Sijui nikajaibu hii
Ila kumpata ngumu rahisi hivyo
 
Oya usiwe na pressure, utapata demu. Kuna watu wengine tunapitia the hard way hadi kujifunza kuwaingia hawa mademu, binafsi confidence ya kumweka sawa demu nimepata sekondari kabla ya hapo ungeniona ungenicheka. Halafu kuna mijitu mingine hapa itajifanya inajuwa kuwavua ch**p* hawa wanawake lakini ukicheki list yake ya wanawake aliyopitia hata Asha ngedere ana afadhali. JIAMINI.

Asante kwa kunipa moyo japo kwa mengine kama kazi,kuongea nk najiamini lakini kwa mwanamke pagumu aisee
 
Umekariri kutongoza ni kumwambia mwanamke nakupenda
kutongoza hata kumtazama tu na kutabasam inatosha
hata kumsalimia tu na kumuuliza kitu nayo ni kutongoza....

Wenzio hawasemi tena nakupenda....ni kusalimia tu na kuongea chochote kilichopo hapo
hata mpira au diamond na wema au watangaza nia wa ccm....
halafu taratibu unajisogeza

Kwa hivyo mbona tunaongea sana, kama kubadilshana mawazo kufunzishana Biblia na mengi tuu sema shida nimpende mmoja ile kumwanza ndio imekua ngumu kwangu
Sita sahau siku nilipompenda mdada mmoja mpaka nikalia chozi lakini kumwambia au kumwonyesha nilishindwa, nikajisemea si vyote viwezekanavyo kwa kweli.
 
Back
Top Bottom