Moja wapo ya Fungu kwenye Biblia linalotafsiriwa vibaya: Matendo ya Mitume 10:15

Nik
Tafadhali mwache mkuu wa meza
 
Hayo mengine ni maagizo na ni Mungu mwenye alizungumza na Musa, Amri ni msisitizo ndio maana Mungu aliziandika kwa kidole chake.
2 Wakorintho 3:7
Basi, ikiwa huduma ya mauti, iliyoandikwa na kuchorwa katika mawe, ilikuja katika utukufu, hata Waisraeli hawakuweza kuukazia macho uso wa Musa, kwa sababu ya utukufu wa uso wake; nao ni utukufu uliokuwa ukibatilika;

2 Wakorintho 3:8
je! Huduma ya roho haitazidi kuwa katika utukufu?

2 Wakorintho 3:15
ila hata leo, torati ya Musa isomwapo, utaji huikalia mioyo yao.

2 Wakorintho 3:16
Lakini wakati wo wote watakapomgeukia Bwana, ule utaji huondolewa.

2 Wakorintho 3:17
Basi “Bwana” ndiye Roho; walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru.
 
Nioneshe Yesu aliposema Tusitunze sabato ilihali hata akina Maria Magdalene tuliowaona wakipumzika siku ya sabato masaa machache baada ya Yesu Kufa, Na hawa ni watu waliomfuata Yesu maeneo mbalimbali.
Siyo lazima aseme direct kwamba tusitunze sabato, ila baadhi ya mazungumzo yake yanathibitisha kuwa kwake yeye hakuna kutunza sabato.

Mfano:
Kwa mujibu wa torati haipaswi kufanya kazi yoyote siku ya sabato lakini Yesu alisema hivi:
Yohana 5:16
Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwudhi Yesu, kwa kuwa alitenda hayo siku ya sabato.

Yohana 5:17
Akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi.
[Yesu alikuwa anayafanya yote haya katika siku ya Sabato. Hivyo Wayahudi hao wakaanza kumsumbua asiendelee. Lakini yeye akawaambia, “Baba yangu hajawahi kuacha kufanya kazi, hivyo nami pia nafanya kazi.”
Yohana 5:16‭-‬17 TKU]

Mfano 2: Soma kisa marko 2 : 23-27
Marko 2:27
Akawaambia, Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato.

Marko 2:28
Basi Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato pia.
[Ndipo Yesu akawaambia mafarisayo, “Siku ya Sabato ilifanywa kwa faida ya watu. Watu hawakuumbwa ili watawaliwe na Sabato. Kwa hiyo Mwana wa Adamu ambaye ni Bwana juu ya kila kitu, pia ni Bwana juu ya siku ya Sabato.”
Marko 2:27‭-‬28 TKU]

Yesu kama mwanadamu mwenye roho wa Mungu alikuwa juu ya sabato (yaani anaweza kufanya chochote na asipate/asihesabiwe hatia) nasi pia wanadamu wa Leo wenye roho wa Mungu(yaani kristo anakaa ndani yetu) tupo juu yaani ni Mabwana wa Sabato tunaweza kufanya lolote na hakuna wa kukuhesabia hatia.

Nikisema hakuna wa kukuhesabia hatia inategemeana na unaemtumaini nafsini mwako, kama unamtumaini Yesu yeye mwenyewe alisema hatakushtaki.
Yohana 5:45
Msidhani kwamba mimi nitawashitaki kwa Baba; yuko anayewashitaki, ndiye Musa, mnayemtumaini ninyi.

Hii mifano michache inathibitisha kuwa hiyo sabato unayoipigania iko chini yako yaani hupaswi kuwa na wasiwasi nayo
 
NB: tunamuabudu Mungu katika roho na KWELI. Hakuna madhara wala dhambi kumla nguruwe.
Exactly, maana chakula hupita mdomoni, tumboni kisha hutupwa chooni. Ila yamtokayo mtu mdomoni hutoka moyoni hayo ndio humtia mtu unajisi.
 
Takbirrrr.
 
Barikiwa sana pastor
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…