Moja wapo ya Fungu kwenye Biblia linalotafsiriwa vibaya: Matendo ya Mitume 10:15

Moja wapo ya Fungu kwenye Biblia linalotafsiriwa vibaya: Matendo ya Mitume 10:15

Kuna watu wanajuta kwa nini hawali hivyo vyakula lkn tu mifumo ya maisha inawakataa na makanisa yao na watatamani siku ya kiama wao wajiweke mbele kuwahukumu wengine waliomla mdudu.. ngoja tu tafsiri ya Mungu siku ya mwisho.. utashangaa vice versa is true
 
Najisi always ni neno ambalo lili-imply kitu ambacho kinaharibu uhusiano kati ya wana wa Israel na Mungu kufuatana na Torati.Hata hivyo Sheria za Torati ambzo ni 613 zilikuwa za muda tu,na Biblia inasema ziliingizwa kwa sababu ya makosa(Wagalatia 3:19),ili aje mkombozi Bwana Yesu,ambaye yeyote atakaye mwamini atahesabiwa haki kwa imani katika Yeye.This was God's original plan,lakini Shetani kwa kumdanganya Hawa akaharibu God's original plan.
Kwamba Torati haikuwa kitu cha kudumu is proved by the following verses.
i.Mwanzo 9:3
3 Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani, kadhalika nawapeni hivi vyote.
Mwanzo 9:3
ii.Wagalatia 3:17
17 Nisemalo ni hili; agano lililothibitishwa kwanza na Mungu, torati iliyotokea miaka mia nne na thelathini baadaye hailitangui, hata kuibatilisha ile ahadi.
iii)Marko 7:18-21
18 Akawaambia, Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia
19 kwa sababu hakimwingii moyoni, ila tumboni tu; kisha chatoka kwenda chooni? Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote.
20 Akasema, Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi.
21 Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati,

Kwa hiyo kufuatana na maandiko hayo,kwa Wakristo sasa hakuna kitu najisi,if you want to eat anything it is okay,ili mradi tu kisikwaze a new convert ambaye imani yake haijajengeka vizuri.Waislamu pia wànatumia neno hili,na maana yake ni ile ya kwenye Torati,isipokuwa kwenye Torati they go farther.Waislamu wao mahiri ni nguruwe tu,vingine ruksa.

Na haramu?Hili ni neno ambalo sisi wana wa Mungu hatulitumii,linatumika sana kwa Waislamu na vyombo vya Sheria.Kote kote lina maana ya kitu kinachokatazwa au kisichokubalika kidini na kisheria.
Kwa hiyo nyie kila mnyama mnakula? Vyura, Nyoka, konokono. n.k?

Swali langu kwako, Petro alikuwa ni Mwanafunzi wa Yesu na bila shaka hilo mnalolitaja la Marko 7 kwamba Yesu alihalalisha Vyakula vyote alikuwa analijua, na tukubaliane katika yale maono wanyama wote alioshushiwa walikuwa ni najisi[wangekuwepo wasafi, angechinja na kula] mbona alimkatalia Mungu ilhali akiwa anajua Yesu alihalalisha hivyo vyakula?
 
Yesu aliwaambia wayahudi waache unafiki
*Wa kunawa hadi kwenye viwiko kabla ya kula ilhali mioyo yao michafu
*Kuishi kwa sheria ,Sabato, vyakula n. K ndiyo maana wanafunzi wake walionekana shambani siku ya sabato.

ENYI WANAFIKI HAMJUI KUWA KIMUINGIACHO MTU CHATOKA KWENDA CHOONI?? BALI KIMTOKACHO MTU (MAWAZO AU MANENO) NDIYO KINAWEZA KUMKOSESHA MTU
Nioneshe Yesu aliposema Tusitunze sabato ilihali hata akina Maria Magdalene tuliowaona wakipumzika siku ya sabato masaa machache baada ya Yesu Kufa, Na hawa ni watu waliomfuata Yesu maeneo mbalimbali.
 
Angetuumba jinsi anavyotaka yeye, tusiwe na mawazo ya uzinzi wala dhambi nyingine.

Katuwekea miili yenye tamaa ili tu aje atuadhibu.

Doesnt make sense.
Kama ambavyo tunachagua wake na waume wa kuoa au kuolewa vivyo hivyo Mungu naye anahitaji watu walio loyal kwake.

Angeweza kutuumba hivyo ikiwa Shetani asingeasi
 
Petro alimkana Yesu X3 kabla jogoo hajawika,na alikua mfuasi wa Yesu,unaweza kutufafanulia kuwa Petro alipata wapi mafundisho ya kumnakana Yesu ?
Kumkana Yesu ilikuwa anaogopa na Yeye kukamatwa lakini kumgomea Mungu hiyo iko Beyond.

Yaliyowapata wengine waliomgomea Mungu tunayajua.
 
Kama ambavyo tunachagua wake na waume wa kuoa au kuolewa vivyo hivyo Mungu naye anahitaji watu walio loyal kwake.

Angeweza kutuumba hivyo ikiwa Shetani asingeasi
Angeweza kumuondoa huyo shetani asiwepo kuisumbua dunia. Lakini kashindwa...sisi ni nani tuweze?
 
Umenena vema sana kuwa kuzishika amri za Mungu na imani ya Yesu. Sasa naomba unitajie ni amri ipi kati ya zile 10 inaongelea habari za wanyama najisi/Amri ipi inazuia wanyama flani waliwe na wengine wasiliwe.
Hayo mengine ni maagizo na ni Mungu mwenye alizungumza na Musa, Amri ni msisitizo ndio maana Mungu aliziandika kwa kidole chake.
 
Angeweza kumuondoa huyo shetani asiwepo kuisumbua dunia. Lakini kashindwa...sisi ni nani tuweze?
Kama alivyompa uhuru wa kuchagua Shetani hata sisi wanadamu ametupa uhuru wa kuchagua pia.
 
Mkuu inaonekna hujajua Sabato ni nini na aina za Sabato, ukijua ndipo utajua kwamba Kuishi kwa kufuata Sheria hakuwezi kutufanya wakamilifu!! Musa na wana wa Israeli walishindwa, kumbuka Yule mtu aliyemfuata Yesu akamwambia NIMEFUATA AMRI ZOTE ZA MUNGU TANGU NIKIWA MTOTO!! Yesu alimjibuje??

Kwa kujua kuwa hatuwezi kuokolewa kwa Sheria kwa upendo wake Mungu akamtoa mwanaye wa pekee ili tuokolewe!! Kama ingekuwa kutunza sabato kunatuokoa kusingekuwa na haja ya YESU kuja duniani
 
Hukumu ipokwa sababu alikuumba yeye, ingekuwa haina maana kama ungekuwa ulijiumba
ndo maana nasema alifanya makusudi kutuumba watenda dhambi na kuweka sheria tusitende dhambi huku akijua fika hatuwezi kuacha dhambi.

Hukumu ni justification ili aje kutuadhibu kwa kutuchoma moto.

Sisi ni wake, dhambi ni zake na hukumu ni yake.
 
Watu wanalitumia fungu hili kuhalalisha kula wanyama ambao wamekatazwa katika kitabu cha Mambo ya walawi. Na kwa kuweka mambo sawa fungu hili halizungumzii vyakula, na kudhihirisha hili ukisoma hiyo matendo ya mitume 10 yote utaelewa.

Fungu lenyewe linasema "Sauti ikamjia mara ya pili, ikimwambia, vituvilivyotakaswa na Mungu usiviite wewe najisi." Mwisho wa kunukuu.

Kwa kifupi labda nisimulie hiki kisa kilivyokuwa,

Ukisoma Matendo ya Mitume 10 kuanzia fungu la 9 Petro alikuwa na njaa sana wakati msosi unaandaliwa alizimia na alioneshwa maono na katika maono hayo Kilishushwa Chombo chenye pembe nne kutoka mbinguni ambamo ndani yake kulikuwa na wanyama mbalimbali, kisha sauti ikasema Ondoka Petro uchinje ule, Petro akajibu akisema Hasha Bwana, kwa maana sijakula kamwe kitu kilicho kichafu wala najisi.

Na tendo hilo la kumuambia kwamba achinje ale lilifanyika mara tatu na zote Petro alikataa, ndio ile sauti ikamwambia vitu alivyovitakasa Bwana usiviite najisi. Na mwisho alipozidi kugoma kile chombo kikarudishwa juu.

Kabla sijaendelea hapa kuna mambo mawili ya kujiuliza,

1. Bila shaka wanyama walikuwepo mle ndani wote walikuwa ni Najisi ndio maana Petro aliwakataa, Na hakuwa anamkatalia Binadamu mwenzake, Bali alikuwa anaikataa sauti ya Mungu.

2. Kama sheria ile ya mambo ya walawi ilifutwa, kama watu wanavyodai kwenye Marko 7 na Mathayo 15(Hili nitaletea uzi nalo maana nalo watu wanadanganywa sana). Ni kwanini Petro alikuwa anakataa na aliwaita wale wanyama najisi na wachafu? Zingatia huyu alikuwa mmoja kati ya wanafunzi wa Yesu.

Na mwisho kabisa yale yalikuwa ni maono tu na wakati anaendelea kuyafikiria kwamba yana maana gani, Roho mtakatifu akamuambia kuna watu watatu kawatuma kuja kwake hivyo aongozane nao.

Tafsiri ya Maono yale inakuja kupatikana katika Matendo ya Mitume 10:28 ambayo inasema "Akawaambia, Ninyi mnajua kuwa si halali mtu aliye Myahudi ashikamane na mtu aliye wa taifa lingine wala kumwendea, Lakini Mungu amenionya, nisimuite mtu awaye yote mchafu wala Najisi."

Watu wanachukua vifungu kidogo ambavyo vinafavor vitu vyao ambavyo kwa macho yao vinawavutia ila hawasemu ukweli.

Jina la Bwana Libarikiwe.

Muwe na Usiku mwema.
Kumbuka kuwa mwanzo MUNGU aliongea Kwa mifano ili watu wajue ni Nini maana yake

Bado awaambia wanafunzi wake walipomuuliza mbona waongea nao Kwa mifano !!!!

Ujue hata agano la kale halikumaanisha haswa wanyama ilimaanisha wanaadamu wenye tabia fanana na wanyama hao usiambatane nao huu ndiyo mfano Sasa unaomtokea Petro , yaani hujui kuwa hata wanyama wanatazamia kufunuliwa Kwa mwana wa adamu?

Na hata sadaka ya wanyama haikupedeza ilipaswa mwanadamu ndiyo afe kama sadaka , ndiyo maana YESU akajitoa mhanga .

Wanyama wazungumzwao kwenye biblia sijui usile huyu au yule ilikuwa ni mfano ambao ungefunuliwa baadaye ambao ndiyo Sasa umefunuliwa

Kumbuka wanajimu wanamgawa mwanadamu na tabia za wanyama utasikia ng'ombe, mbuzi, nk na nk
 
Kwa hiyo nyie kila mnyama mnakula? Vyura, Nyoka, konokono. n.k?

Swali langu kwako, Petro alikuwa ni Mwanafunzi wa Yesu na bila shaka hilo mnalolitaja la Marko 7 kwamba Yesu alihalalisha Vyakula vyote alikuwa analijua, na tukubaliane katika yale maono wanyama wote alioshushiwa walikuwa ni najisi[wangekuwepo wasafi, angechinja na kula] mbona alimkatalia Mungu ilhali akiwa anajua Yesu alihalalisha hivyo vyakula?
Haya ndio matatizo ya kusoma Biblia bila kuwa na Roho Mtakatifu.Najua Petro alishushiwa nguo yenye wanyama wote akaambiwa achinje ale-Matendo ya Mitume 10:13.Najua pia kwamba Petro alisema sijakula kamwe kitu kilicho najisi.But notice this, Mungu alimuambia "vilivyotakaswe na Mungu usiviite najisi."

Sasa who has higher authority,obviously ni Mungu,so obviously Mungu ameruhusu kula kila kitu!I hope this is clear.

Lakini mazungumzo haya kati ya Mungu na Petro hayahusiani na vyakula kabisa,yanahusu Waisraeli kuwaona wasio Waisraeli wachafu au najisi.
Soma Matendo ya Mitume 10:23-29.Notice mstari wa 28.Petro hapa ana-refer maongezi yake ya awali kuhusu ile nguo,anasema,"Ninyi mnajua ya kuwa si halali mtu aliye Myahudi ashikamane na mtu aliye wa taifa lingine,wala kumwendea,lakini Mungu amenionya nisimuite mtu awaye yote mchafu au najisi.

Kwa hiyo ni wazi mazungumzo kati ya Mungu na Petro yalimhusu Kornelio na nyumba yake ambao hawakuwa Wayahudi.Notice pia Matendo ya Mitume 10:34-35,it proves that point.
 
Usile nguruwe.(Israeli ya kimwili)
Usile nguruwe (usipokee mafundisho wa wachungaji wasaliti/mbwa mwitu, rejea Mathayo. Hii ni kwa sisi Waisrael kiroho)

NB: tunamuabudu Mungu katika roho na KWELI. Hakuna madhara wala dhambi kumla nguruwe.

Sent from my SM-G800F using JamiiForums mobile app
swali moja la kujiuliza ni hili, je? kula nguruwe, samaki wasio na magamba n.k kuwa dhambi, ilikuwa ni sheria? ikiwa jibu ni ndio, basi, kuanzia Yesu Kristo alipokuja alikuja na agano jipya ndani ya Damu yake, agano ambalo hatuhesabiwi haki kwa matendo ya sheria bali kwa sheria ya Roho mtakatifu. hatuongozwi na Sheria tena, tunaongozwa na Roho Mtakatifu.

ndio maana katika Matendo 15:20, wakristo wa kwanza ambao ni mitume, waliingiwa kwenye mgogoro wao kwa wao kwasababu awali hawakutakiwa kabisa kuchangamana hata na wamataifa, ilikuwa najisi, sasa wamataifa wakaanza kuokoka, na ilijulikana wazi kwamba sheria ya dini ya kiyahudi haikuwahusu wamataifa, walichanganyikiwa kweli pia hasa baada ya kuona hata wamataifa wamejazwa hadi Roho Mtakatifu kama vile wao wenyewe walivyojazwa, tena wamataifa wenyewe hawajatahiriwa hata kutahiriwa tu. wakashindana wao kwa wao wakiamini hadi watahiriwe, au hadi wafuate sheria zote za dini ya kiyahudi ndio watakuwa wameokoka. baada ya mabishano, wakaweka kikao, kwa uongozo wa Roho Mtakatifu wakafikia muafaka kwamba sheria za kiyahudi haziwahusu wamataifa, yaani mimi na wewe, isipokuwa wakatoa angalizo ambalo walisema wamataifa wakifuata hilo watakuwa wamefanya yanayompasa mtu aliyeokoka.

Watu fulani walishuka kutoka Uyahudi na kuwafundisha ndugu, wakisema, “msipotahiriwa kama desturi ya Musa, hamwezi kuokolewa.”

4 Walipokuja Yerusalem, walikaribishwa na Kanisa na mitume na wazee, na waliwasilisha taarifa ya mambo yote ambayo Mungu amefanya pamoja nao.

5 Lakini watu fulani walioamini, waliokuwa katika kundi la Mafarisayo, walisimama nakusema, “ni muhimu kuwatahiri na kuwaamuru waishike sheria ya Musa.”

7 Baada ya majadiliano marefu, Petro alisimama na kusema kwao, “Ndugu mwatambua kwamba kitambo kizuri kilichopita Mungu alifanya chaguo kati yenu, kwamba kwa mdomo wangu Mataifa wasikie neno la injili, na kuamini.
8Mungu, anayefahamu mioyo, anashuhudia kwao, anawapa Roho mtakatifu, kama alivyofanya kwetu;
9na hakutengeneza utofauti kati yetu na wao, akiifanya mioyo yao safi kwa imani.

10Kwa hiyo, kwa nini mnamjaribu Mungu kwamba muweke nira juu ya shingo za wanafunzi ambayo hata baba zetu wala sisi hatukuweza kustahimili? Lakini twaamini kwamba tutaokolewa kwa neema ya Bwana Yesu, kama walivyokuwa.”

21 Kutoka vizazi vya wazee kuna watu katika kila mji wahubirio na kumsoma Musa katika masinagogi kila Sabato.”
22Kwa hiyo ikaonekana kuwa imewapendeza mitume na wazee, pamoja na kanisa lote, kumchagua Yuda aliyeitwa Barsaba, na Silas, waliokuwa viongozi wa kanisa, na kuwatuma Antiokia pamoja na Paulo na Barnaba.
23 Waliandika hivi, “Mitume, wazee na ndugu, kwa ndugu wa Mataifa walioko Antiokia, Shamu na Kilikia, salamu.

28 Kwa kuwa ilionekana vyema kwa Roho Mtakatifu na kwetu, kutoweka juu yenu mzigo mkubwa kuliko mambo haya yaliyo ya lazima: kwamba mgeuke kutoka kwenye vitu vitolewavyo sadaka kwa sanamu, damu, nyama iliyosongolewa (iliyonyongwa), na uasherati. Kama mtajiweka mbali na hivi, itakuwa vyema kwenu. Wasalam.”
 
Watu wanalitumia fungu hili kuhalalisha kula wanyama ambao wamekatazwa katika kitabu cha Mambo ya walawi. Na kwa kuweka mambo sawa fungu hili halizungumzii vyakula, na kudhihirisha hili ukisoma hiyo matendo ya mitume 10 yote utaelewa.

Fungu lenyewe linasema "Sauti ikamjia mara ya pili, ikimwambia, vituvilivyotakaswa na Mungu usiviite wewe najisi." Mwisho wa kunukuu.

Kwa kifupi labda nisimulie hiki kisa kilivyokuwa,

Ukisoma Matendo ya Mitume 10 kuanzia fungu la 9 Petro alikuwa na njaa sana wakati msosi unaandaliwa alizimia na alioneshwa maono na katika maono hayo Kilishushwa Chombo chenye pembe nne kutoka mbinguni ambamo ndani yake kulikuwa na wanyama mbalimbali, kisha sauti ikasema Ondoka Petro uchinje ule, Petro akajibu akisema Hasha Bwana, kwa maana sijakula kamwe kitu kilicho kichafu wala najisi.

Na tendo hilo la kumuambia kwamba achinje ale lilifanyika mara tatu na zote Petro alikataa, ndio ile sauti ikamwambia vitu alivyovitakasa Bwana usiviite najisi. Na mwisho alipozidi kugoma kile chombo kikarudishwa juu.

Kabla sijaendelea hapa kuna mambo mawili ya kujiuliza,

1. Bila shaka wanyama walikuwepo mle ndani wote walikuwa ni Najisi ndio maana Petro aliwakataa, Na hakuwa anamkatalia Binadamu mwenzake, Bali alikuwa anaikataa sauti ya Mungu.

2. Kama sheria ile ya mambo ya walawi ilifutwa, kama watu wanavyodai kwenye Marko 7 na Mathayo 15(Hili nitaletea uzi nalo maana nalo watu wanadanganywa sana). Ni kwanini Petro alikuwa anakataa na aliwaita wale wanyama najisi na wachafu? Zingatia huyu alikuwa mmoja kati ya wanafunzi wa Yesu.

Na mwisho kabisa yale yalikuwa ni maono tu na wakati anaendelea kuyafikiria kwamba yana maana gani, Roho mtakatifu akamuambia kuna watu watatu kawatuma kuja kwake hivyo aongozane nao.

Tafsiri ya Maono yale inakuja kupatikana katika Matendo ya Mitume 10:28 ambayo inasema "Akawaambia, Ninyi mnajua kuwa si halali mtu aliye Myahudi ashikamane na mtu aliye wa taifa lingine wala kumwendea, Lakini Mungu amenionya, nisimuite mtu awaye yote mchafu wala Najisi."

Watu wanachukua vifungu kidogo ambavyo vinafavor vitu vyao ambavyo kwa macho yao vinawavutia ila hawasemu ukweli.

Jina la Bwana Libarikiwe.

Muwe na Usiku mwema.
Umeongea Sana...niambie why Mungu muumba ulimwengu wenye nyota na sayari zaidi ya billion aumie kima mmoja sayari moja ndani ya system ya nyota moja akila mnyama mmoja...hizi ni sheria ni za watu tumieni akili za kuzaliwa...
 
wanaokula damu (kama masai na wachaga wanavyokunywa kisusio), wanaokula nyama ya mnyama ambaye hajachinjwa shingoni damu ikamwagika (kibudu), wanaofanya uasherati, ndivyo vilikatazwa. ila sheria zile za kidini hasa kwenye rituals za vyakula ambazo ni sheria za kiyahudi (za Musa) waliona ni mzigo kuwatwisha watu ambao sio wayahudi, hivyo sio dhambi kula nguruwe, kambare, pweza, kaa na vingine kwa mujibu wa maandiko hayo, au la, tuyaondoe kwenye Biblia. hata hivyo chakula ni kwa tumbo, kimtokacho mtu ndicho kibaya, kiingiacho huishia chooni Yesu alisema hivyo au mmdsahau? matendo ya mwili hayawezi kumpendeza Mungu hata siku moja. na matendo yote ya sheria ni ya mwili.
 
Watu wanalitumia fungu hili kuhalalisha kula wanyama ambao wamekatazwa katika kitabu cha Mambo ya walawi. Na kwa kuweka mambo sawa fungu hili halizungumzii vyakula, na kudhihirisha hili ukisoma hiyo matendo ya mitume 10 yote utaelewa.

Fungu lenyewe linasema "Sauti ikamjia mara ya pili, ikimwambia, vituvilivyotakaswa na Mungu usiviite wewe najisi." Mwisho wa kunukuu.

Kwa kifupi labda nisimulie hiki kisa kilivyokuwa,

Ukisoma Matendo ya Mitume 10 kuanzia fungu la 9 Petro alikuwa na njaa sana wakati msosi unaandaliwa alizimia na alioneshwa maono na katika maono hayo Kilishushwa Chombo chenye pembe nne kutoka mbinguni ambamo ndani yake kulikuwa na wanyama mbalimbali, kisha sauti ikasema Ondoka Petro uchinje ule, Petro akajibu akisema Hasha Bwana, kwa maana sijakula kamwe kitu kilicho kichafu wala najisi.

Na tendo hilo la kumuambia kwamba achinje ale lilifanyika mara tatu na zote Petro alikataa, ndio ile sauti ikamwambia vitu alivyovitakasa Bwana usiviite najisi. Na mwisho alipozidi kugoma kile chombo kikarudishwa juu.

Kabla sijaendelea hapa kuna mambo mawili ya kujiuliza,

1. Bila shaka wanyama walikuwepo mle ndani wote walikuwa ni Najisi ndio maana Petro aliwakataa, Na hakuwa anamkatalia Binadamu mwenzake, Bali alikuwa anaikataa sauti ya Mungu.

2. Kama sheria ile ya mambo ya walawi ilifutwa, kama watu wanavyodai kwenye Marko 7 na Mathayo 15(Hili nitaletea uzi nalo maana nalo watu wanadanganywa sana). Ni kwanini Petro alikuwa anakataa na aliwaita wale wanyama najisi na wachafu? Zingatia huyu alikuwa mmoja kati ya wanafunzi wa Yesu.

Na mwisho kabisa yale yalikuwa ni maono tu na wakati anaendelea kuyafikiria kwamba yana maana gani, Roho mtakatifu akamuambia kuna watu watatu kawatuma kuja kwake hivyo aongozane nao.

Tafsiri ya Maono yale inakuja kupatikana katika Matendo ya Mitume 10:28 ambayo inasema "Akawaambia, Ninyi mnajua kuwa si halali mtu aliye Myahudi ashikamane na mtu aliye wa taifa lingine wala kumwendea, Lakini Mungu amenionya, nisimuite mtu awaye yote mchafu wala Najisi."

Watu wanachukua vifungu kidogo ambavyo vinafavor vitu vyao ambavyo kwa macho yao vinawavutia ila hawasemu ukweli.

Jina la Bwana Libarikiwe.

Muwe na Usiku mwema.
Kwani siye tukila nguruwe we unapungukiwa nini?
 
Back
Top Bottom