Moja ya dalili kuwa hujitambui na hujiamini ni kutuma nauli kwa mwanamke ambaye ndio kwanza mnaanza mahusiano

Moja ya dalili kuwa hujitambui na hujiamini ni kutuma nauli kwa mwanamke ambaye ndio kwanza mnaanza mahusiano

Nawaunga mkono wanawake wanaokula nauli ila mwanamke anayetumia nauli ya mwanaume mwingine kuenda kwa mwanaume mwingine huyo ni mpumbavu

Kama umeshindwa kuenda kwa huyo mtoto wa mwanamke mwenzio aliyekutumia hiyo nauli ni heri uile tu kuliko kuendea kwa mwanaume mwingine

Na mianaume ya hivi inayopenda vitonga kula hela za wanaume wenzao kupitia mademu zao nayo inatakiwa ichapwe viboko hadharani na idhalilishwe tu
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Dah!!!
 
Mimi nataka K, lazima nihakikishe mzigo unanifikia kwa kugharamia usafiri wa 'package'...

Mbona tunaagiza vitu online na nauli tunalipia tunakuna pumbu kusubiria delivery..!??
Are women some kind products!!!? Ooh wow.
 
Hakika vijana tujifunze kwa mtibeli na tumtumikie MUNGU Katika haki na kweli maana yeye ndo hutupa yaliyo mema.
 
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Lazima uliwe nauli wewe si lijinga. Na mimi nawasisitiza kina dada endeleeni kuwachangamsha ubongo wanaume wasiojitambua na wasiojiamini.

Wewe umemtongoza Binti au mwanamke labda kwenye Daladala, au mtandaoni,au umekutana naye mtaani au Kanisani au popote. Ni sawa kabisa. Wewe ni mwanaume lazima utongoze.

Katika mawasiliano ya hapa na pale, ukiwa unamseti Mwanamke kwenye angle unayoitaka ajae. Naye pia anakuseti kwenye Log10 yake ujae akupasue. Hivyo ni mchezo fulani wa kuzidiana akili na mbinu.
Kila mmoja akimvizia mwenzake.

Mwanamke yeyote anayetumia kigezo cha kukupima kama unampenda kwa Kukutaka fedha au umhudumie ujue huyo ni tapeli, hakupendi, na anachotaka ni kukupasua.

Elewa kuwa Mwanamke anayekupenda hakosi NAULI ya kuja kukuona mpenzi wake. Mwanamke hawezi kukosa nauli kwa Mwanaume anayempenda au mtoto wake aliyemzaa. Na Mzazi wake.

Sisi Watibeli tunatongoza Mwanamke na anakuja kwa nauli yake. Kama hataki tunapita kushoto. Hatulazimishi na hatutaki kulazimishwa.

Uzoefu wangu katika Mahusiano unaonyesha wazi kuwa Mwanamke akikupenda lazima ajitoe kwako kama wewe utakavyojitoa.

Achana na wale wanaume Washamba ambao wanatuma nauli alafu nauli hizohizo wanawake wanazitumia kwenda kwa wanaume wanaowapenda.

Mwanaume yoyote mjinga huona kujiumiza ndio uanaume wakati ni ubwege. Huwezi ukajiumiza kwa mtu ambaye hakupendi au kujiumiza kijinga ukasema huo ndio uanaume. Uanaume sio kuwa Bwege au Lofa.
Uanaume sio kujidharau na kukubali mtu mwingine akudharau.

Ni sawa na wale Mabwege yanayohudumia wake au Wanawake zao alafu bado hayapewi heshima, na tendo wanapimiwa au wanaomba. Wanaume hawapo hivyo.

Mwanaume lazima ujue kuwa jasho lako pia lazima liheshimiwe. Mtu anayedharau jasho lako amekudharau.

Kijana ukianza mahusiano usitume nauli, huko ni kutojitambua na kutojiamini.
Ni bora hiyo nauli utafute Kahaba au mwanamke mcheza vikoba hapo mtaa wa tatu umpe uende ukamalizane naye kama shida ni uzinzi, ngono.

Kama shida ni Mahusiano ya kweli, usitume Nauli. Mwache Aje kwa pesa yake mwenyewe. Naye lazima ajitoe kwaajili yako.

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam


Wakati mwingine tunatuma tukijua wana asilimia 6% kuja, 94% hawaji, na hata wasipokuja, tunajua pengine tumesaidia single Mama na wanae kununua mchele.

Tatizo ni kukosa hela tu, sio kutuma hela..... Kama unajielewa huwezi nunua mwili wa mwanamke kwa nauli, naelewa unaweza usinielewe.
 
Wakati mwingine tunatuma tukijua wana asilimia 6% kuja, 94% hawaji, na hata wasipokuja, tunajua pengine tumesaidia single Mama na wanae kununua mchele.

Tatizo ni kukosa hela tu, sio kutuma hela..... Kama unajielewa huwezi nunua mwili wa mwanamke kwa nauli, naelewa unaweza usinielewe.

Kununua ni kununua tuu
 
Wanadai ni heri zaidi kutoa kuliko kupokea, mambo mengine kama nauli ni utu zaidi sio kupigwa, kuna wadada kweli kakupenda na uhalisia wa maisha, na maisha yetu haya kila mtu ana yajua , na kweli uhalisia hana pesa, sioni kama ni dhambi au kosa kumsaidia nauli, sisi wanaume ni walezi wa hawa wenzetu, ndio maana wana sema wanaume watakula kwa jasho, hilo ndo jasho lenyewe.
 
Waache!
Alafu kuna mijinga ikipigwa matukio inajfanya inahasira za kijinga😂😂 yaani kama Wendawazimu hivi. Ukiyasikia yanavyoongea ni kama nati zimelegea. Ooh! Nimetumia gharama kubwa sijui nimelipa blahblahblah!
Alafu Mpumbavu hanaga aibu. Hataki kama kujieleza hivyo ni kujidhalilisha kuwa yalikuwa majinga yenyewe yanaona yalikuwa yanawajibika😄
hahah its true.
 
Back
Top Bottom