Moja ya harusi bora kabisa hii

Moja ya harusi bora kabisa hii

Issue watu wa aina hiyo ni wabinafsi huwezi waona hata kwenye kuchangia harusi au misiba ya wengine.

Hivyo hujua wazi wakiwa na harusi zao hakuna watakaowachangia.Hivyo kujificha kwenye hilo chaka la harusii za watu wachache sijui.sita nk wanajua network kwenye za kuchangiana harusi wao hawamo hivyo wanakuwa hawana network kwenye eneo hilo.Waweza kuwa na network kwenye maeneo mengine lakini sio hilo
Usichanganye harusi na misiba, harusi imekuwa ni kero sana kwa baadhi ya watu. Unafika nyumbani unakuta kadi, yaani hata mtu huna mawasiliano naye yoyote yale. Baada ya hapo inakuwa ni kero kubwa, unakuwa kama anakudai, na hata hukuwahi kutoa ahadi ya kuchangia, kiufupi inakera sana.
Kuna harusi tulichangia, siku ya harusi, kamati ya harusi wanawapa wazazi zawadi ya Tsh milioni nne. Yaani michango yetu inagawiwa tena kwa wazazi, kuanzia hapo niliona ni ushenzi kabisa.
 
Moja ya harusi bora kabisa hiiView attachment 2949950
Watu wa hivi huwa hawataki mambo mengi kabisa, mara nyingi huwa sisi wanaume ndio tuna aamua iwe hivi.
View attachment 2949951View attachment 2949952

Nyingine ile mkimaliza kufunga ndoa shughuli zina endelea kama siku zingine tu za kawaida pale nyumbani.
Niliyoshuhudia ni ya mwamba ambapo kulikuwa na
1. Bwana na Bibi harusi
2. Mashahidi wawili
3. Padre
4. Sister ambaye Alisaidia kupiga picha
 
Hapahapa tz, nina maamuzi magumu sana kwenye vitu kama hizo.....ilizua zogo sana ila ndo sijali,,, wanafiq tu,
Wananiogopa vibaya mno jinsi nilivyo kauzu

Hapo ndo utajua watz wanapenda vitu visivyo vya msingi yani,
Safi sana, wabongo tuko tayari kuchangia harusi ila matibabu hapana😃 but vipi upande wa shemeji pia alikubaliana na hilo?
 
Huwa wengine wana matatizo yao

Mfano Magufuli aliwahi tamba waziwazi kuwa alifunga ndoa na Janet Magufuli akiwa anasoma chuo.kikuu na ndoa ilifungiwa pale kanisa la chuo kikuu ndoa hiyo ilishirikisha watu watano yeye na bi Janet Magufuli na wasimamizi wao wawili na Padre aiyefungisha ndoa

Baada ya kufungishwa ndoa walikunywa soda moja moja wote watano .Baada ya kunywa soda Magufuli akaendelea na masomo yake shughuli ya ndoa ikaishia hapo.

Hapo ukiangalia unaona kuna shida ndoa kama hiyo.Ndugu wa pande zote wapo ,marafiki wapi,majirani wapo nk why iwe hivyo?
Ndugu wa nini ?, marafiki wa nini ? Na majirani wa nini ?
 
Sio kweli ni ya watu wapumbavu wabinafsi na wasiokuwa watu wa watu iwe majirani ,ndugu,marafiki,wanaofanya nao kazi au biashara nk

Ndoa kama hixo ni watu ambao hata ndugu hawataki wanajioza wenyewe.Wakati kawaida jamii ndio inatakiwa ikuoze .Watu wanaofurika ndio waozaji ukiona wachache jua hao sio wati wa watu kaa nao mbali ni watu wa maisha self-contained hao.
Itoshe kusema huna akili nahuna exposure masikini ndio mnajaza watu kwenye maharusi namisiba hayo mambo huwez kuyakuta kwakina Beckham na ellon mask
 
Si lazima yes ila lawama sasa, inabidi kuwa na roho ngumu kiasi

Kama wewe ama nyumbani kwenu kwa wazazi sio vendors wa harusi

Yaani hamna ukumbi mnaomiliki

Pia Hampo kwenye mishe za u Mc

Jua Ukifanya sherehe kubwa jua wewe ni mjinga yaani wewe unaumia ila unatajirisha watu wanaofanya hizo kazi


Kina Mc garab wanatajirika. Ila wana ndoa wao ndoa zinavunjika sababu kuu financial reasons
 
Back
Top Bottom