Kapeace
JF-Expert Member
- May 26, 2017
- 24,514
- 65,521
Tulilipanga wote hilo akili moja yaniSafi sana, wabongo tuko tayari kuchangia harusi ila matibabu hapanaš but vipi upande wa shemeji pia alikubaliana na hilo?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tulilipanga wote hilo akili moja yaniSafi sana, wabongo tuko tayari kuchangia harusi ila matibabu hapanaš but vipi upande wa shemeji pia alikubaliana na hilo?
Ndugu wa nini ?, marafiki wa nini ? Na majirani wa nini ?
Hebu ngoja, Millard Ayo alifunga ndoa lini?Hizo ni harusi za jamii yenye akili sana
Harusi ya majizo mmiliki wa EFM na Lulu ilikuwa kama hizo. Jiulize Je lulu na majizo hawana watu wa kuwachangisha ?, ama hawana network ?
Harusi ya Millard Ayo ilikuwa kama hizo, je millard Ayo hana watu wa kuwachangisha ?
Jibu ni hapana. Bali ni ushahidi wa wazi kwamba ni mfano wa vijana wenye akili kubwa Tanzania
Akili zao ndizo zimewafanya watajirike wakiwa wadogo
Priest si unamuona hapo, mahakama gani hiyo inayoendeshwa na priest?Bila shaka hii ni ndoa ya mahakamani?
But shughuli huwa wanawake ndio wanaotaka sana sio wanaume. Mara nyingi wanaume wanajua hapa kuna mzigo wa gharama ila wanawake wanataka ile shughuli wafurahie.Mnaweza kujikana? Tatizo lililopo...Mob pressure...nyie wanaume mnapenda sana hizi harusi, lakin mnashindwa kuwa na misimamo. Mkishawaambia mashangazi zenu na wajomba wenu wakapinga basi na msimamo unadissolve.
Sawa mara nyingi wanawake tunakuwa vikwazo lakin sio spouse tu, hadi huko kwenu mkisema hili mnapingwa. Ila kufanya such things lazima ujikane na uwe tayar kugombana na ndugu zako wengi.
Ulafi tu wanakuwa wanaza ubwabwa.Ila kufanya such things lazima ujikane na uwe tayar kugombana na ndugu zako wengi
Hapo kwenye ndg ni kama ulikuwepo lawama kama zote hadi kufikia kutamkiana maneno magumu ugomvi km mtu umenyima kupumua- ndoa ni ya wawili ndg ni kitu kidogo sana katika maisha ya ndoa
Ndio ni ya watu wawili, siku hizi macho ya wengi yanaharibu ndoa za watu. Unafunga ndoa watu wanabet lini mtaachana, utasikia "hawa kwa jinsi alivyo yule mwanamke na mdomo wake hawatamaliza miaka 3".Sio kweli ni ya watu wapumbavu wabinafsi na wasiokuwa watu wa watu iwe majirani ,ndugu,marafiki,wanaofanya nao kazi au biashara nk
Ndoa kama hixo ni watu ambao hata ndugu hawataki wanajioza wenyewe.Wakati kawaida jamii ndio inatakiwa ikuoze .Watu wanaofurika ndio waozaji ukiona wachache jua hao sio wati wa watu kaa nao mbali ni watu wa maisha self-contained hao.
Hii ndio shida mnafunga ndoa ili kuwaprove wrong mashost zenu badala ya kuwa na mtu ambaye unapenda kufanya nae lifeMashoga zangu waliosema sitaolewa watanionajeee???
Sawa sawaNdoa ni yako maamuzi ni yako
Mimi napenda sana hii kwenye harusi kama mwanaume nina shughulikia hili ila vipi kuhusu sendoff ambayo ni mwanamke ndiyo ana shughulikia anaweza fanya hivi na yeye hiyo siku ?!Yeah unaita watu unaowafahamu.
Upande wa mke na upande wako shughuli kwisha.
Kufanya nini, kufanya sherehe simple kama hivyo ama ?!Mnaweza kujikana? Tatizo lililopo...Mob pressure...nyie wanaume mnapenda sana hizi harusi, lakin mnashindwa kuwa na misimamo. Mkishawaambia mashangazi zenu na wajomba wenu wakapinga basi na msimamo unadissolve.
Sawa mara nyingi wanawake tunakuwa vikwazo lakin sio spouse tu, hadi huko kwenu mkisema hili mnapingwa. Ila kufanya such things lazima ujikane na uwe tayar kugombana na ndugu zako wengi.
Na ndo maana nasemaje braza, ukisema wanawake basi jumuisha wanawake wa upande wa kiumeni na wa kikeni plus huyo mke mtarajiwa. Hapa anaweza kulaumiwa mtarajiwa tu huku ukisahau huko kwenu pia kuna wanawake wanaotaka shughuli hasa kina mama. Anakuwa anaona amechangia watoto wa wenzake kwann yeye wa kwake asichangiwe na yeye ajishebedue mtaa wa pili ujue.But shughuli huwa wanawake ndio wanaotaka sana sio wanaume. Mara nyingi wanaume wanajua hapa kuna mzigo wa gharama ila wanawake wanataka ile shughuli wafurahie.
Ndugu wengi hawatakagi hizi simple...amini kwamba.Kufanya nini, kufanya sherehe simple kama hivyo ama ?!
Naomba nijibu hapa...sendoff ni shughuli ya wazazi wa mwanamke. Wao ndo wanaamua watamuaga binti yao kwa style gani. So kile kitakachoamuliwa ni mzazi kaamua. Sasakwa sabbu ya usasa na mabinti wanaoagwa wanajiweza anakuwa anaamua yeye afanyeje ndo mara designer annacollectionz, mara mckatokisha, etc.... Lakin laiti kwamba ingekuwa ni wazazi wenyewe basi mambo yangekuaga muswano, ni familia chache sana zingemudu sherehe kubwa. Nweiz maisha ni mafupi sana so kila anayeamua lake na afanye tu.....Mimi napenda sana hii kwenye harusi kama mwanaume nina shughulikia hili ila vipi kuhusu sendoff ambayo ni mwanamke ndiyo ana shughulikia anaweza fanya hivi na yeye hiyo siku ?!
Kumbe....sasa hata kama nikifanya simple kama hii alafu sitaki mchango wa mtu still watakataaa ?!Ndugu wengi hawatakagi hizi simple...amini kwamba.
Mimi mwanaume naweza amua sherehe simple kama hivyo ila kama mwanamke anataka mambo makubwa aisee sasa haita pendeza, maana Sendoff mambo mengi sherehe kubwa alafu harusi simple kama hivyo, wabongo wata anza maneno tuu, aah upande wa mume wame tuangusha sana tunajuta kumpeleka mtoto wetu kule, wabahili sana mara wachoyo wale sherehe hivi je tukienda salimia watatupa hata maji kweli ?! Nafikiri sherehe simple kama hizi ni nyie wote muamue kuanzia Sendoff mpaka harusi ila shida Wanawake nyie ndiyo hamuelewi mnataka mashindano all the time.Naomba nijibu hapa...sendoff ni shughuli ya wazazi wa mwanamke. Wao ndo wanaamua watamuaga binti yao kwa style gani. So kile kitakachoamuliwa ni mzazi kaamua. Sasakwa sabbu ya usasa na mabinti wanaoagwa wanajiweza anakuwa anaamua yeye afanyeje ndo mara designer annacollectionz, mara mckatokisha, etc.... Lakin laiti kwamba ingekuwa ni wazazi wenyewe basi mambo yangekuaga muswano, ni familia chache sana zingemudu sherehe kubwa. Nweiz maisha ni mafupi sana so kila anayeamua lake na afanye tu.....
Anayejitenga na wenziwe ni mchawiNdugu wa nini ?, marafiki wa nini ? Na majirani wa nini ?
Utanuniwa mkuu.....unavyohisi harusi ndogo ni shingapi??all things inclusiveKumbe....sasa hata kama nikifanya simple kama hii alafu sitaki mchango wa mtu still watakataaa ?!