Moment: Benki ya Finca ilivotunyoosha mimi na familia yetu kisawa sawa

Moment: Benki ya Finca ilivotunyoosha mimi na familia yetu kisawa sawa

Binafsi hakuna kitu naogopa kama mikopo
Kwa story hii, kitu cha kuogopa siyo mikopo, ila cha kuogopa ni tabia za uasherati. Kiuchumi ni afadhali ya ulevi wa pombe kuliko uasherati.

Ulevi wa pombe huwa na kikomo cha matumizi, ukishalewa vya kutosha huwezi kuendelea kununua pombe, so ulevi una kikomo cha matumizi.

Lakini, tunaona kwenye story hii huyu mwasherati amehonga kwa hawara biashara nzima ya pato la familia na kiwanja chenye msingi. Inasikitisha.

Ova
 
Hakuna benki inatoa mkopo kwa mume bila mke kusaini,mama yako angeweka injuction kisingeuzwa kitu,elewa maana ya court injuction
Msiwe wabishi, hayo mambo ya spouse concert, affidavit, yameanza miaka ya karibuni baada ya familia nyingi kupata matatizo na ikagundulika baba ndo chanzo.
Zamani hata kuuza ilikuwa ni foreclouser sio market value
 
Daah maisha yanatupitisha kwenye moments ambazo ni ngumu kusahaulika. Moja ya moment ambayo sitakuja kuisahau ni jinsi Bank ya Finca ilivotufanyia somba somba alooo.

Nakumbuka mwaka 2010 tumekaa ofisini na mama (ofisi ya kushona nguo maana wazazi wangu wote ni mafundi kushona na kipindi hicho walikuwa wanatumia ofisi moja ambapo mama ni mavazi ya ke na mzee mavazi ya me).Tukashangaa kuna gari imeandikwa finca imefika pamoja Canter size ya kati hivi,wale jamaa walijitambulisha kisha wakatuonyesha makaratasi yalikuwa na majina ya mzee na sahihi zake kisha wakaomba tuwapishe wafanye kazi yao.

Aisee hatukuamini wale jama walianza kupikia mashine za mle ofisini,walipakia meza,tundua vitambaa,vitenge,wax na kanga zote.Walichukua kabati la kuuzia nyuzi,zipu,ruksi na vidude vingne kama lilivyo. Walivyotoka hapo wakaomba mama aingie kwenye gari na mimi nikachoma ndani wakatueleza tunaenda kwenye kiwanja chenu.

Daah tulivofika kule kiwanja kilikuwa na msingi tayari kikapigwa mnada mbele ya macho yetu. Daah siku ile mama machozi talimtoka ikabidi ampigie mzee kumuuliza vipi ndo mzee akamjibu kuwa alikopa na hela amemfungulia duka la vipodozi mchepu kashindwa kuliendesha kala mtaji af kasepa.

Mama ikabidi amuulize ko ukowapi saa hivi,mzee bila aibu akajibu nipo nakodi gari inakuja kupakia vitu vya ndani tunarudi nyumba ya kijijini kulima.

Aisee siku ile ilikuwa mpalangano yaani hadi tunakuja kusettle mimi na dogo tushahamishwa na shule ilitumia mda sana.

Bank ya kwanza kuijua ilikuwa Finca kisa hii issue

ILA MZEE ALIJUA KUTUUZA AISEE
Poleni sana Mkuu

Ndiyo maana binafsi hupenda kuwashauri Wazee wenzangu akina ERoni na Glenn tukiwa tunacheza Bao kwamba, Kwa uzee huu tulionao tusijaribu kutafuta michepuko hasa mabinti vigoli

Hawachelewi kutuibia Pension zetu kutokana na wao kuwa na mbinu Kali za Kisasa ambazo wakizitumia tukiwa Kwa bed utajikuta unaandika Will kwamba Mali na fedha zote za kwenye akaunti ni Mali ya Mchepuko huku tukiwaacha watoto na wake zetu wa ujanani katika wakati mgumu 🙌
 
Back
Top Bottom