Mtoto wa Monalisa aliwahi kuhojiwa mwaka jana alipomaliza form 6 na akasema chuo hawezi kusoma bongo na hakuna chuo cha hadhi yake na hata havijui vyuo vya bongo Ila anasikiasikia tu sijui Kuna UD, IFM na sijui nini.
Naweza kusema ni akili za kitoto hivyo hapaswi kuchukuliwa sana serious, japo kwa mwanafunzi aliyemaliza form 6 kibongobongo huyo ni mtu mzima maana wanakua over 18. Lakini sio issue sana bado hajakua vizuri.
Tatizo lipo kwa mama mzazi ambae ni monalisa, yeye alikuja na kusema haoni kosa na akamtetea. Ni kosa hilo, alipaswa kumsahihisha mtoto kwa Yale aliyozungumza.
Sasa baada ya muda monalisa akarudi tena public akimsindikiza mtoto airport ili aende chuo ulaya, hivyo ametimiza shauku ya mtoto wake. Bila yeye mama kujua kuwa elimu ya Ulaya mashariki haina thamani kivile. Na hata ada yao ni ndogo sana haina tofauti sana na vyuo vya hapa. Hadi hapa alipaswa kuona kitu.
Ulaya mashariki nchi za Ukraine, Bulgaria, Romanja, Czech, Poland, Slovakia, Belarus n.k ni nchi maskini na hata wananchi wa hizo nchi huzamia nao nchi za ulaya magharibi.
Unataka mtoto asome ulaya? Mpeleke nchi za ulaya magharibi Kama UK, Germany, France, Iraland, Norway, Sweden, Belgium, Spain n.k
Hivyo ni Kama alitaka kuonyesha ana huo uwezo kwa watu wa mitandaoni(wengi nao hawaelewi kitu) ndio maana alifanya yote haya in public ili watu waone. Na bahati mbaya pia aliingia contract kwa kulipa kwa installment via Glo.......e....lin...(wale madalali wa kupeleka watoto vyuo vya India na huko ulaya mashariki) nimeficha Hilo jina la hao watu ili kutoharibu biashara yao. Unaenda kuingia mkopo wa kumsomesha mtoto kwenye nchi za ulaya mashariki ili kuonekana unaweza kumsomesha Ulaya?
Ni mfano wa mzazi mbaya, Sasa unasema watu Wana chuki. Ni Nani aliwaambia muende public kwa mambo yenu binafsi? Ulionyesha kujitutumua sana bila kujua mkija kukwama mnakimbilia kuomba watu wawachangie na kutia huruma. Mnapswa kufahamu internet haisahau
Tusikubali kila ambacho watoto wanataka alafu tunawatimizia huku tukibaki na maumivu makubwa. Mtoto anapaswa kupewa kile ambacho una uwezo nacho tu.