Monday Morning Special!!

Monday Morning Special!!

Nilivyojiunga JF nilijua ni sehemu nitasoma niburudike na nijifunze. Sikua najua hata members huwa wanaonana nje ya hapa. Kumbe watu huwa wanaonana huko nje halafu yakiwabumia wanarudi kutuelezea humu.

Inatosha kuwa mtu mzima kujua kipi niweke wazi kwenye mtandao kipi nisikiweke wazi. Kwa mimi naona ni jambo baya kuweka ugomvi wa matusi na mahusiano kwenye mtandao ambao hujui nani utakutana nae kesho.

Ukiwa kwenye ugomvi unaoweza kuuepuka uepuke. Heri nusu shari kuliko shari kamili. Hutaonekana mnyonge kwa kumdharau mtu anaekukosea. Hata huyo mtu akiandika mara mbili tatu akiona humjibu ataacha tu.

Umetengeneza marafiki kaa nao kwa amani. Kupishana ni jambo la kawaida kwa binadamu. Usitake kupishana kwako kidogo na mtu kuwe ndo bifu ulibebe mgongoni.

Tuifanye JF kuwa sehemu salama. Tukumbuke kuna maisha baada ya mitandao. Maisha hayaishii leo hapa JF. Kuna kazi kuna watoto kuna ndugu. Usijiangalie wewe unaendika ujinga humu. Angalia na wengine walio nyuma yako.

Hakuna mtu aliepewa medal kwa kupenda kutukanana mtandaoni sana sana watu wanakudharau.

Nashangaa JF niliyoingia kwa mapenzi yangu watu wanachaguliana wa kuongea nae wa kucheka nae. Guys huku uliingia mwenyewe. Usifanye jambo kumfurahisha mtu ulomkuta humu ambae hakuchangii hata bundle. Mtu anakwambia kamtukane mzigua na wewe kwa kuwa akili yako haijui kuchanganua mambo unakuja unanitukana kweli.

Huku ni home of GT embu tuishi basi kama GT.

Nimesema haya baada ya kuona watu wanajisahau sana na hii mitandao hasa humu.
Ndiyo mpunguze kudanga, mnaomba pesa mno mpaka wachunwaji wanahisi uchungu.
 
Ktk maisha yetu ya kila siku kuna kupata na kukosa, namaanisha kuna faida na hasara. Tunafurahia sana faida kwakuwa inamanufaa kwetu na familia zetu na jamii kwa ujumla, tunaichukia sana hasara kwakuwa inaudhi/inakwaza/inabomoa.
Binadamu pia tupo hivyo kama hivyo vitu viwili, yani faida na hasara. Kuna watu ni faida na kuna watu ni hasara ktk jamii yetu, hatuwezi kuwa timilifu wote ni faida tupu pasipo hasara, Mungu mwenyewe alipata hasara pale malaika wake walipoasi na kumgeuka.
Kuna watu ktk mitandao ya kijamii ni makwazo kwa wengine kila wakati na kuna wengine ni wajenzi wa jamii pana kwa kadri Mungu aluvyowajalia, kama wewe hapa unajenga lakini kuna watakaojaribu kubomoa, ndivyo tulivyo binadamu hatukuanza sisi walianza watu wa mwanzo wa ulimwengu huu. NB: Sihalalishi unachokitetea.
 
Back
Top Bottom