Mondi platinumuz anaelekea kuwa level ya Michael Jackson

Mondi platinumuz anaelekea kuwa level ya Michael Jackson

Mkuu the cigarette that you are smoking is not good for you healthwise, just LEAVE IT ALONE before it is too late.

Jamaa no mbunifu sana. Wimbo japo kuna watu wanajaribu kuudis but tayari ni gumzo kila kona ya hii nchi. Vibanda vyote vinavyoingiza nyimbo kwenye simu, memori card, na hata flash siku mbili hizi wamepiga pesa sana. Unaambiwa kuna foleni KUBWA kila mtu anataka kuupata huu wimbo.

Mondi kwenye video yake mpya ya wimbo wa kanyaga kagongesha watu kwata kama Michael jackson. Video ni nzuri, kwa kweli Mondi ni noumar.
 
Nilibahatika kumuona karibu kama hatua tano alivyokuja Bongo 90"s..ukimtazama jamaa alikuwa anatisha (sio ubaya)bali jamaa alikuwa na power fulani watu wanazimia..alafu ananukia kama jini
Yaani una maanisha kwamba akimuona unasisimka yaani sijui unakuwa unajisijikiaje ...yeah iko hivyo hiyo hata diamond platnum anayo ....Ila power ya MJ imeshindikana. .. yaani imepitiliza viwango vya ushirikina .... Kuna clip niliiona akiwa Moscow yaani raia wanapata tabu wanamkimbilia tu nyomi la watu kibao kama 500 yao hiyo sio show .ni wamemuona mtaani tu ...basi bwana Kuna sehemu sijui Walikuwa location akatokea binti 1 hivi akapewa nafasi ya kumsalimia Michael Daah yule dada akawa analia ..anasema I can't blv ..Ohhh my god huu sio muujiza au ninaota .Michael ni wewe kweli ..yaani yule dada hapo amepewa chance ya kumshika mkono tu Michael akiwa ndani ya gari dada wawatu analia aise. ........ Daah yule jamaa sijui freemason walimpaka pika vipi sio kwa ule mvuto

Mkuu hebu ni hadithie jamaa ilikuwaje alipo Kuja tz maana sisi wengine tulikuwa bado sijui tuna mwaka 1
 
Mkuu the cigarette that you are smoking is not good for you healthwise, just LEAVE IT ALONE before it is too late.
Honestly niileta hapa kupima upepo watu mtareact vp. Najua kabisa MJ ni level ya mbali sana.

Mondi type yake ni kina Jose Chamelione n alike.
 
Jamaa Akili yako itakuwa imeganda. .Hivi una mjua MJ vizuri wewe ??

Yaani kabisaa una m-compare MJ binaadamu ambaye shughuli za mazishi yake ndio shughuli ambayo ina shika nafasi ya kwanza kwa kutazamwa na watu duniani nzima. ..Tangu technology ya TV na social network ilipoanzishwa. ...

Labda nikusaidie tu kukuelewesha kwamba Michael Jackson ndiye binaadamu maarufu kuliko binaadamu wote wanao ishi na walio wahi kuishi karne ya 21
Sawa lakini hamfikii Yesu na Wiliam sheckspear.
 
Basi tuna kuomba umtake radhi late MJ ...maana kazi aliyoifanya duniani ilikuwa ni kubwa mnooo MJ kaanza kuwa famous tangu akiwa na miaka 6..mpaka mauti yanamfika bado alikuwa ni mtu maarufu sana ijapokuwa katika umri wa utuuzima wake tangu mwaka 2000 hakutoa album yoyote ila mwaka 2009 alipotaka kufanya tour Uingereza miezi nyuma kabla ya tarehe ya siku ya event tayari tickets zilikuwa zineshaisha na kampuni iliyokuwa inasimamia show hiyo ikawa inajiandaa kuanza kuprint tickets nyingine. ..Kumbuka kwamba mtu tunaye muongelea hapa Alikuwa anafanya show kwenye viwanja vikubwa vya mpira kama wembley
Hapana mkuu. Nilikuwa napima upepo....
 
Tena apige magoti na kilio cha makamasi,

Daah MJ pamoja na umaarufu wote hakua na jeuri wala dharau wala majivuno, zaidi alinikosha vile alivyokua na aibu kali,

May his soul continue to rest in peace.
Aamen ...Jamaa nilikuwa na muhusudu sana. ..
 
Tena apige magoti na kilio cha makamasi,

Daah MJ pamoja na umaarufu wote hakua na jeuri wala dharau wala majivuno, zaidi alinikosha vile alivyokua na aibu kali,

May his soul continue to rest in peace.
Usisahau pia kumpa pale alivyoona kinyaa kukanyaga ardhi ya Afrika
 
Back
Top Bottom