Hivi jamani pammoja na juhudi na hatua zinazochukuliwa bado kuna uzembe hivi wa hali ya juu. Na kwa nini hassa??? Mbunge kwanza ulikua wapi hadi mradi wa mabioloni unachezewa? Mkuu wa mkoa na hadi wa wilaya? Hadi waziri aje ndio haya madudu ya shughulikiwe?
Binafsi natoa maoni ADHABU ya watu kama hawa wazembe na wezi inabidi ipandishwe, watu hawaogopi, wanajua wakitumbuliwa tayari wameshajiwekezea huko mahela chungu nzima kwahiyo maisha yao yataendelea kunyooka, na akiletwa mwingine nae ataendelea na uzembe na wizi huohuo, hadi atakaposhtukiwa tiari kashakula mabilioni. watu hawa ni kuwaweka ndani si chini ya miaka 10 na hakuna kununua kifungo. Wallahi bada ya hapo hakuna atakaye thubutu kuleta madudu hayo.