Monduli: Waziri Jumaa Awezo akuta maji hayatoki kisa Sh. elfu 50, amtumbua Meneja mbele ya Wananchi

Monduli: Waziri Jumaa Awezo akuta maji hayatoki kisa Sh. elfu 50, amtumbua Meneja mbele ya Wananchi

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso, amefanya ziara ya kikazi katika wilaya ya Monduli mkoani Arusha na kukuta wananchi hawapati maji kutokana na changamoto mbali mbali hali iliyopelekea kuchukua hatu ya kumsimamisha kazi Meneja wa mradi wa maji wa RUWASA Nevill D. Msaki.

View attachment 1704490
Waziri Aweso tafadhali njoo Morogoro uongee na wananchi kuna ubadhilifu mkubwa Kihonda Kilimanjaro na maeneo yanayolizunguka eneo hilo, Mkandarasi aliyekabidhiwa mradi hakukamilisha kazi akalipwa, baadhi ya mabomba yakaondolewa kwenye eneo la mradi, usambazaji wa mabomba haukukamilika wananchi hawapati maji, ubabaishaji ni mkubwa haijapata kutokea.
 
Wimbo wa Sisi ni maskini, chanzo chake ni haya mambo!!
Kuna ufisadi mkubwa kampuni ya kwanza iliomba tenda ikashinda halafu ikaipa tenda kampuni ingine ya kiongozi wa halmashauri ndio ifanye!!!

Msikilize msemaji wa pili kwenye hii CLIP akimwaga mboga!!


 
Yaani kuna watu vichwa ngumu acha kabisa.Raisi unamwona hadi anakonda .Ana delegate akiwaamini alio delegate madaraka chini lakini wapi!! upigaji pesa uko palepale na uongo pale pale!! Naibu waziri asingekuwa makini akaipokea hiyo ripoti ndio ilikuwa imetoka hiyo.

Mijizi imeshajua raisi anawaamini sana mawaziri kwa hiyo imehamia kwa mawaziri kuwa ukimudu kumdanganya waziri atampelekea ripoti raisi kuwa kila kitu kiko sawa itaishia hapo.Hao ndicho walitaka kufanya.Ila wamekwaa kisiki Naibu waziri yuko ngangari kagoma kudanganyika!!!

Hebu fikiria hawa watu kipindi kilichopita cha kutofuatiliwa walivyotupiga pesa ni hatari.Hivi sasa wanafuatiliwa kwa nguvu bado vichwa vigumu tu
Yaani hawa dawa yao ni adhabu kali, jela au wawekwe mahali hata ndugu zao wasiwaone kwa miaka 10. Hapo ndio watu wataogopa
 
Juhudi zinachukuliwa kwenye makaratasi na kwenye vyombo vya habari, field ni tofauti kwani pesa hazifiki kwa wakati na zikifika hazitoshi
Sasa kibaya hawa wamepeleka report kwamba mradi umeisha na watu wanapata maji. Yaani hawa wamwdanganya taasiai kubwa pammoja na wamwdanganya raisi na waziri wake. Hawa ni watu wa hatari sana
 
kuna watu ugoi goi ni tatizo la kuzaliwa nalo.

yaani kama hapo kasimamishwa ndio akili zinarudi sasa.
😆😆😆 kweli kabisa, kama ndio akili imemrudi. Lakini bahati mbaya kashavuta sana chakwake. Na tusishangae tukasikia kwamba kasamehewa na karudishwa kwenye post. Napenda sana juhudi ya raisi lakini bado kuna mambo mengi yanatakiwa yawekwe sawa.
 
Aweso Njoo na hapa manispaa ya Morogoro, mradi wa maji wa kihonda mkundi una zaidi ya miaka 4 haujakamilika, tuko mjini sehemu yenye vyanzo vingi vya maji lakini wananchi wanakosa huduma ya msingi ya maji, mbunge wetu tajiri abood kalala usingizi as if kapigwa general anaesthesia (full kaputi),mi naona hawa wabunge wenye asili ya kiarabu wako kimaslahi yao binafsi,let them give us break,
 
Yaani kuna watu vichwa ngumu acha kabisa.Raisi unamwona hadi anakonda. Ana delegate akiwaamini alio delegate madaraka chini lakini wapi!! upigaji pesa uko palepale na uongo pale pale!! Naibu waziri asingekuwa makini akaipokea hiyo ripoti ndio ilikuwa imetoka hiyo.

Mijizi imeshajua raisi anawaamini sana mawaziri kwa hiyo imehamia kwa mawaziri kuwa ukimudu kumdanganya waziri atampelekea ripoti raisi kuwa kila kitu kiko sawa itaishia hapo.Hao ndicho walitaka kufanya.Ila wamekwaa kisiki Naibu waziri yuko ngangari kagoma kudanganyika!

Hebu fikiria hawa watu kipindi kilichopita cha kutofuatiliwa walivyotupiga pesa ni hatari.Hivi sasa wanafuatiliwa kwa nguvu bado vichwa vigumu tu
Bila kuwapiga risasi hawa watu hatuwezi kuendelea mbele. China wamefanikiwa kwa sababu ya kutowaonea huruma watu kama hawa.
 
Nashindwa kuelewa hili somo,DC yupo, RC yupo,iweje hadi aje Waziri ilhali wao wapo na wananchi?

Nasema sielewi sielewi nini kinachoendelea
 
WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso, amefanya ziara ya kikazi katika wilaya ya Monduli mkoani Arusha na kukuta wananchi hawapati maji kutokana na changamoto mbali mbali hali iliyopelekea kuchukua hatu ya kumsimamisha kazi Meneja wa mradi wa maji wa RUWASA Nevill D. Msaki.

View attachment 1704490
Tulikuambia Waziri Aweso , ubabaishaji wa mirad ya Maji upo kwa watendaji Wizarani, Mkoani na Wiayani.
Weledi hakuna!
 
kuna uzembe hapa kwakweli. mpaka kiongozi aje ndio waruke ruke. wanashindwaje ku solve tatizo dogo kama hilo
Ukweli kuna watu sijui tuseme ni dharau,au kuridhika!!! tusiseme mengi,anastahili kupata alicho pata.yaani ni zaidi ya uzembe na uvivu.
 
Wimbo wa Sisi ni maskini, chanzo chake ni haya mambo!!
kuna watu wanaleta ubosi bosi,yaani yy ni kutoa maagizo akiwa ofisini ametulia,sasa subili uje mradi wa kaposho fulani,atakuwa bize huyo mpaka basi,sasa ngoja mradi ukishakwsha humuoni tena atoke ofisini.hawa dawa yao ni kuwa weka pending Kama hivyo.good job waziri aweso.
 
Aje huku kwetu Wami Dakawa,Wilaya ya Mvomero.Maji hayatoki eti kwa sababu ya seed money ya 2m,na Mkurugenzi wa Halimashauri yupo.
 
Jinsi inavyoonekana ni kwamba ukiwa kiongozi chini mwetu hutakiwi kuamini wasaidizi wako na haitakiwi kuamini ripoti yoyote unayoletewa ofisini! Ni aibu kubwa sana, fedheha wasomi wanaitwa wataalamu kuwa na tabia za unafsi kiasi hicho. NINI KIMEUA UZALENDO NCHINI MWETU? Inasikitisha kweli kweli. Nadhani ziwekwe sheria za kuwafunga miaka isiyopungua 7 na kuwafilisi. Tena aliyetoa hiyo ripoti na aliyeifikisha kwa Waziri pia anatakiwa kuwajibishwa.
 
Kuna kazi kubwa sana. Mheshimiwa Rais anahaki ya kuwa mkali. Mijitu ya ajabu kumbe bado yamejaa
 
Back
Top Bottom