Monduli: Waziri Jumaa Awezo akuta maji hayatoki kisa Sh. elfu 50, amtumbua Meneja mbele ya Wananchi

Waziri Aweso tafadhali njoo Morogoro uongee na wananchi kuna ubadhilifu mkubwa Kihonda Kilimanjaro na maeneo yanayolizunguka eneo hilo, Mkandarasi aliyekabidhiwa mradi hakukamilisha kazi akalipwa, baadhi ya mabomba yakaondolewa kwenye eneo la mradi, usambazaji wa mabomba haukukamilika wananchi hawapati maji, ubabaishaji ni mkubwa haijapata kutokea.
 
Wimbo wa Sisi ni maskini, chanzo chake ni haya mambo!!
Kuna ufisadi mkubwa kampuni ya kwanza iliomba tenda ikashinda halafu ikaipa tenda kampuni ingine ya kiongozi wa halmashauri ndio ifanye!!!

Msikilize msemaji wa pili kwenye hii CLIP akimwaga mboga!!


 
Yaani hawa dawa yao ni adhabu kali, jela au wawekwe mahali hata ndugu zao wasiwaone kwa miaka 10. Hapo ndio watu wataogopa
 
Juhudi zinachukuliwa kwenye makaratasi na kwenye vyombo vya habari, field ni tofauti kwani pesa hazifiki kwa wakati na zikifika hazitoshi
Sasa kibaya hawa wamepeleka report kwamba mradi umeisha na watu wanapata maji. Yaani hawa wamwdanganya taasiai kubwa pammoja na wamwdanganya raisi na waziri wake. Hawa ni watu wa hatari sana
 
kuna watu ugoi goi ni tatizo la kuzaliwa nalo.

yaani kama hapo kasimamishwa ndio akili zinarudi sasa.
😆😆😆 kweli kabisa, kama ndio akili imemrudi. Lakini bahati mbaya kashavuta sana chakwake. Na tusishangae tukasikia kwamba kasamehewa na karudishwa kwenye post. Napenda sana juhudi ya raisi lakini bado kuna mambo mengi yanatakiwa yawekwe sawa.
 
Aweso Njoo na hapa manispaa ya Morogoro, mradi wa maji wa kihonda mkundi una zaidi ya miaka 4 haujakamilika, tuko mjini sehemu yenye vyanzo vingi vya maji lakini wananchi wanakosa huduma ya msingi ya maji, mbunge wetu tajiri abood kalala usingizi as if kapigwa general anaesthesia (full kaputi),mi naona hawa wabunge wenye asili ya kiarabu wako kimaslahi yao binafsi,let them give us break,
 
Bila kuwapiga risasi hawa watu hatuwezi kuendelea mbele. China wamefanikiwa kwa sababu ya kutowaonea huruma watu kama hawa.
 
Nashindwa kuelewa hili somo,DC yupo, RC yupo,iweje hadi aje Waziri ilhali wao wapo na wananchi?

Nasema sielewi sielewi nini kinachoendelea
 
Tulikuambia Waziri Aweso , ubabaishaji wa mirad ya Maji upo kwa watendaji Wizarani, Mkoani na Wiayani.
Weledi hakuna!
 
kuna uzembe hapa kwakweli. mpaka kiongozi aje ndio waruke ruke. wanashindwaje ku solve tatizo dogo kama hilo
Ukweli kuna watu sijui tuseme ni dharau,au kuridhika!!! tusiseme mengi,anastahili kupata alicho pata.yaani ni zaidi ya uzembe na uvivu.
 
Wimbo wa Sisi ni maskini, chanzo chake ni haya mambo!!
kuna watu wanaleta ubosi bosi,yaani yy ni kutoa maagizo akiwa ofisini ametulia,sasa subili uje mradi wa kaposho fulani,atakuwa bize huyo mpaka basi,sasa ngoja mradi ukishakwsha humuoni tena atoke ofisini.hawa dawa yao ni kuwa weka pending Kama hivyo.good job waziri aweso.
 
Aje huku kwetu Wami Dakawa,Wilaya ya Mvomero.Maji hayatoki eti kwa sababu ya seed money ya 2m,na Mkurugenzi wa Halimashauri yupo.
 
Jinsi inavyoonekana ni kwamba ukiwa kiongozi chini mwetu hutakiwi kuamini wasaidizi wako na haitakiwi kuamini ripoti yoyote unayoletewa ofisini! Ni aibu kubwa sana, fedheha wasomi wanaitwa wataalamu kuwa na tabia za unafsi kiasi hicho. NINI KIMEUA UZALENDO NCHINI MWETU? Inasikitisha kweli kweli. Nadhani ziwekwe sheria za kuwafunga miaka isiyopungua 7 na kuwafilisi. Tena aliyetoa hiyo ripoti na aliyeifikisha kwa Waziri pia anatakiwa kuwajibishwa.
 
Kuna kazi kubwa sana. Mheshimiwa Rais anahaki ya kuwa mkali. Mijitu ya ajabu kumbe bado yamejaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…