Moodys wamekuja nchini kutathmini cha kuuza endapo tutashindwa kulipa mikopo?

Moodys wamekuja nchini kutathmini cha kuuza endapo tutashindwa kulipa mikopo?

Nilidhani Dkt. Mwigulu Nchemba atakuwa amewaalika WEF au WTO team kuja kutathmini uwezo wa nchi kufanya exports... kumbe ameleta watu wa benki kutathmini dhamana ya mikopo endapo tutashindwa kulipa..

Jamani mwaka 2024 na 2025 tusirudie kosa la kuipa kura CCM. Haya yanayofanyika ni kuipiga nchi mnada. Hawa hawajali hata kidogo.

Hali ya kipato ni duni. Wanaongeza mikopo ambapo sehemu kubwa ya mikopo hiyo inaenda matumboni mwao
Kwani mhe Ndugai anasemaje ?!! Tuwape kura au tusiwape ?!! Naona yupo kimya sana anakula vyake taratiiiibu !!
 
Hapa inapigwa akili kuporwa vyote vilivyowekezwa wakati wa magufuli kuanzia ndege, meli ziwa victoria gesi etc etc. Wameshaona mtazamo wa samia kukopa ovyo na kumlaghai bado madeni ni madogo akope zaidi. Hila na ujanja wa mabeberu tutajikuta kila kilichowekezwa na umma kiko kwenye mikono ya watu binafsi tena wageni.
Tujifunze kutoka argentina. Wao toka miaka ya 80 kwa kumbukumbu yangu wanakopa na mikopa haijaweza kuwakomboa toka umaskini. Nchi imeishia kua na migogoro mikubwa ya kiuchumi hadi kuanguka serikali zao mara kwa mara. Juzi tu hapa wametangaza mfumuko wa bei ni zaidi ya asilimia 100. Wanaoneemeka ni viongozi ambao wanapokezana kutoka mume kwenda mke wake, na sasa kuna kigogo mmoja rais ila aliyekua mke wa rais ndio makamu wake. Wana kesi za kula rushwa hdi hukumu zipo ila hang'atuki mtu wala hafungwi mtu. Naona kama tukiendelea na mama tunaelekea huko.
Yaani hili bwawa litachukuliwa kama lile la Zambia lilivyochukuliwa ili kulipa madeni, SGR, ndege zote na gesi vitakuja kubebwa kufidia deni...
 
Kuwatumia WEE KULA kuweka bei za mchongo za mafuta na kuendelea kutoa bei elekezi za mchongo kwenye mafuta pale kitita kikubwa kinapohitajika.
 
Ataicha nchi yetu ikiwa kwenye madenu mpaka mjukuu yupo tumboni anadaiwa.
Yaani PhD hii kweli haikuriri kweli ama ilipata ya kuandikiwa. Mana jamaa hajabuni kitega uchumi japo uchumi ukue ama mapato yaongezeka Bali yeye anawaza kuwakamua wachunga ng'ombe wenzake.
 
Tunaambiwa hawa Moodys wamekuja kutathmini hali yetu ya kukopesheka, hii maana yake ni nini? Mtu ambae hakopesheki ni yupi na mtu anaekopesheka yukoje?

Kwa uelewa wangu, mtu anaekopesheka ni yule anaeweza kuulipa mkopo tarajiwa, lakini pia anacho cha kuweka ‘Collateral’ endapo atashindwa kurudisha mkopo, sasa kwa hapa Tz kuna vitu kadhaa nahisi vinatolewa macho

1.) Gesi - Japo tunaambiwa kwamba JK alishaiuza yote, lakini nadhani bado kuna nyingine iliyogunduliwa huko deepshore inaweza kufanyiwa tathmini na Moodys kuona jinsi Inavyoweza kuwekwa dhamana na kupigwa mnada endapo tutashindwa kulipa deni, hivyo wanaweza kusema tunakopesheka bado.

2.) Bwawa la Nyerere - Hii pia ni asset kubwa sana inayoweza kutumika kama ‘collateral’, Moodys wanaweza kufanya tathmini juu ya thamani ya zile Megawati 2100 zitakazozalishwa na mapato yanayoweza kuingizwa, hapa wanaweza kutupa maksi kwamba bado tunakopesheka, maana tukishindwa kulipa deni, basi wanajimilikisha bwawa na kutuuzia umeme kwa bei mbaya

3.) Watu milioni 60 - Watu ni asset, hata kama ajira, bado wanaweza kutumika kama dhamana, ukiwa na watu wengi unakuwa na nafsi ya kuwakamua na kuwaminya kwenye kodi kwa kutumia mbinu mbali mbali, mfano Tozo za miamala, Tozo za mazao, VAT na kadhalika, hivyo tukishindwa kulipa deni, tunaweza kuoandishiwa tozo na kodi muda wowote ili kulipa deni

4.) SGR., mengine tuongezee

-----
Wataalamu kutoka Taasisi ya kimataifa ya Moody's inayojihusisha kuzifanyia tathimini Nchi mbalimbali dunia ili kujua uwezo wao wa kukopesheka katika masoko ya fedha ya Kimataifa, wamewasili Nchini kwa ajili ya kuifanya tathimini Nchi ya Tanzania.

Akizungumza wakati akiikaribisha Timu ya Wataalamu kutoka Taasisi hiyo Jijini Dodoma, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema tathimini hiyo ni fursa kwa Tanzania kuweza kuyafikia Masoko ya fedha ya Kimataifa yatakayoiwezesha Nchi kupata rasilimali fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya Wananchi.

Dkt. Mchemba amesema kuwa tathimini huru inayofanywa na Taasisi hiyo itaiwezesha Tanzania kuaminiwa na Taasisi za fedha za kimataifa hivyo kuchochea uwekezaji ambao utakuza uchumi wa Nchi pamoja na ajira kwa Vijana na kwamba ujio wa Wataalamu hao unajibu kiu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyeagiza Nchi ifanyiwe tathimini ili kubaini uwezo wake wa kuyafikia masoko ya fedha ya kimataifa katika kuharakisha maendeleo ya Watu.
Ukakasi mtupu.Naona hatimaye tutanyang'anywa mkoa mmoja maarufu sana wenye Tanzanite na utalii.Ole wetu.
 
Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu kila kinyozi anajifunzia kunyoa. Utasikia mikopo ya masharti nafuu, tunakopesheka, kula kwa urefu wa kamba. Baadae tunalipishwa sisi raia

Ukiwa mjinga usitoe mawazo hadharani namna hii
 
Wa Tanzania wasomi hasa wa Uchumi huwa mnasoma nini? Huwezi kuamini, siku moja miaka kama mitano iliyopota nilimuuliza waziri mmoja kuhusu Standard & Poor, Fitch na Mood, kwake ilikuwa misamiati na yule mwingine kwenye ofisi ya CAG alikuwa gizani hapo ndiyo niligundua Kwa mara nyingine nani wanatutawala very uninformed na ignorant people.

Rating ya Tanzania tangu 2008 imekuwa ikifanywa na Moody, wakati ule ilikuwa B, sijafuatilia miaka ya hivi karibuni.

wewe mwandishI usipotoshe, this is just a rating agency usilete porojo, nchi yako ikiwa rated unakuwa na nafasi ya kupata investors, financiNg etc etc

Kama hujafuatilia miaka ya hivi karibuni unapata wapi ujasiri wa kupinga usichokijua
 
Nilidhani Dkt. Mwigulu Nchemba atakuwa amewaalika WEF au WTO team kuja kutathmini uwezo wa nchi kufanya exports... kumbe ameleta watu wa benki kutathmini dhamana ya mikopo endapo tutashindwa kulipa..

Jamani mwaka 2024 na 2025 tusirudie kosa la kuipa kura CCM. Haya yanayofanyika ni kuipiga nchi mnada. Hawa hawajali hata kidogo.

Hali ya kipato ni duni. Wanaongeza mikopo ambapo sehemu kubwa ya mikopo hiyo inaenda matumboni mwao

Kumbe shida ni kuwa CCM hatuwezi kukuzingatia sababu umeonesha upo upande gani
 
Back
Top Bottom