Moodys wamekuja nchini kutathmini cha kuuza endapo tutashindwa kulipa mikopo?

Moodys wamekuja nchini kutathmini cha kuuza endapo tutashindwa kulipa mikopo?

Tumeisha! Tunageuzwa geuzwa kama chapati tu sshv hatuna lakusema!
 
Tunaambiwa hawa Moodys wamekuja kutathmini hali yetu ya kukopesheka, hii maana yake ni nini? Mtu ambae hakopesheki ni yupi na mtu anaekopesheka yukoje?

Kwa uelewa wangu, mtu anaekopesheka ni yule anaeweza kuulipa mkopo tarajiwa, lakini pia anacho cha kuweka ‘Collateral’ endapo atashindwa kurudisha mkopo, sasa kwa hapa Tz kuna vitu kadhaa nahisi vinatolewa macho

1.) Gesi - Japo tunaambiwa kwamba JK alishaiuza yote, lakini nadhani bado kuna nyingine iliyogunduliwa huko deepshore inaweza kufanyiwa tathmini na Moodys kuona jinsi Inavyoweza kuwekwa dhamana na kupigwa mnada endapo tutashindwa kulipa deni, hivyo wanaweza kusema tunakopesheka bado.

2.) Bwawa la Nyerere - Hii pia ni asset kubwa sana inayoweza kutumika kama ‘collateral’, Moodys wanaweza kufanya tathmini juu ya thamani ya zile Megawati 2100 zitakazozalishwa na mapato yanayoweza kuingizwa, hapa wanaweza kutupa maksi kwamba bado tunakopesheka, maana tukishindwa kulipa deni, basi wanajimilikisha bwawa na kutuuzia umeme kwa bei mbaya

3.) Watu milioni 60 - Watu ni asset, hata kama ajira, bado wanaweza kutumika kama dhamana, ukiwa na watu wengi unakuwa na nafsi ya kuwakamua na kuwaminya kwenye kodi kwa kutumia mbinu mbali mbali, mfano Tozo za miamala, Tozo za mazao, VAT na kadhalika, hivyo tukishindwa kulipa deni, tunaweza kuoandishiwa tozo na kodi muda wowote ili kulipa deni

4.) SGR., mengine tuongezee

-----
Wataalamu kutoka Taasisi ya kimataifa ya Moody's inayojihusisha kuzifanyia tathimini Nchi mbalimbali dunia ili kujua uwezo wao wa kukopesheka katika masoko ya fedha ya Kimataifa, wamewasili Nchini kwa ajili ya kuifanya tathimini Nchi ya Tanzania.

Akizungumza wakati akiikaribisha Timu ya Wataalamu kutoka Taasisi hiyo Jijini Dodoma, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema tathimini hiyo ni fursa kwa Tanzania kuweza kuyafikia Masoko ya fedha ya Kimataifa yatakayoiwezesha Nchi kupata rasilimali fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya Wananchi.

Dkt. Mchemba amesema kuwa tathimini huru inayofanywa na Taasisi hiyo itaiwezesha Tanzania kuaminiwa na Taasisi za fedha za kimataifa hivyo kuchochea uwekezaji ambao utakuza uchumi wa Nchi pamoja na ajira kwa Vijana na kwamba ujio wa Wataalamu hao unajibu kiu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyeagiza Nchi ifanyiwe tathimini ili kubaini uwezo wake wa kuyafikia masoko ya fedha ya kimataifa katika kuharakisha maendeleo ya Watu.
.Nchi zipo kwenye verge ya ku-collapse kwa sababu ya mikopo,halafu sisi bado tunang'atng'ania mikopo,ni upimbi wa hali ya juu sana.Angalia👇 nchi zenye uwezekano wa ku-collapse 2023 kwa sababu ya mikopo.


Ndugai was right, sisi wananchi tunajukumu la kumuunga mkono.
 
Hapa inapigwa akili kuporwa vyote vilivyowekezwa wakati wa magufuli kuanzia ndege, meli ziwa victoria gesi etc etc. Wameshaona mtazamo wa samia kukopa ovyo na kumlaghai bado madeni ni madogo akope zaidi. Hila na ujanja wa mabeberu tutajikuta kila kilichowekezwa na umma kiko kwenye mikono ya watu binafsi tena wageni.
Tujifunze kutoka argentina. Wao toka miaka ya 80 kwa kumbukumbu yangu wanakopa na mikopa haijaweza kuwakomboa toka umaskini. Nchi imeishia kua na migogoro mikubwa ya kiuchumi hadi kuanguka serikali zao mara kwa mara. Juzi tu hapa wametangaza mfumuko wa bei ni zaidi ya asilimia 100. Wanaoneemeka ni viongozi ambao wanapokezana kutoka mume kwenda mke wake, na sasa kuna kigogo mmoja rais ila aliyekua mke wa rais ndio makamu wake. Wana kesi za kula rushwa hdi hukumu zipo ila hang'atuki mtu wala hafungwi mtu. Naona kama tukiendelea na mama tunaelekea huko.
Bandari washalamba
 
Kama hujui acha kuiidharirisha utaumbuliwa Bure
 
Back
Top Bottom