Nikuulize swali, hivi lile daraja la Nyerere, na mabarabara mengine, hata stendi ya mkoa Morogoro nk, yasingeweza kujengwa na watz wenyewe, kwakuwa taaluma hatuna au mitaji hatuna?
Hapo ndo ninapouona ujinga huu, haswa kuona jengo tu limejengwa na wageni, linavutia, nasi kuona kwa hilo tumeendelea, mi siamini kama hayo nayo ni maendeleo.
Mfano, mi maskini, Bakresa amenipa bilioni moja, akanijengea nyumba nzuri na mengineyo,yote ndani ya wiki 2 tu. Je nami naweza pita mtaani na kujinadi kuwa nimeendelea?
Na wenye akili nao wanaweza kumsifia huyu mtu kuwa jamaa ameendelea? Najua uko vizuri, utakuwa umenielewa nini namaanisha hapo.