Morogoro: Bodaboda wawili wafariki dunia kwa kugongwa na Lori

Morogoro: Bodaboda wawili wafariki dunia kwa kugongwa na Lori

Mwezi jana kupita Kibaigwa usiku nilikuta gari zimesimama na mimi nikaenda kushuhudia.

nikakuta vidume viko bize kumchomoa dereva wa boda na boda yake kanasia katikati ya akseli za nyuma ya tela.
boda waliowengi hawazingatii kabisa usalama kwasababu hawapatiwi mafunzo ya udereva.
 
Aisee maisha ni mafupi nimepita bwawani -moro mida hii ya saa 1 jioni kuna bodaboda wawili wamekanyagwa vibaya sana na lorry , kiufupi wamekufa , yaani vichwa havieleweki

Msinidai picha nimeshindwa kupiga
Inamaana pikipiki mbili zimehusika kwenye ajali?
 
Boda boda haziruhusiwi kutumia highways, hii ni sheria isipokua politicians wanaangalia kura tu, ukubwa wa pikipiki hizi ni mdogo kuruhusiwa kutumia freeways, pia hawavai hermits za kujikinga na ajali ,ondoa bodaboda zote kwenye barabara kuu,Mbeya kwenye ile T1 ndio uchafu zaidi maana kuna bajaji ndani ya highway kibao
 
Hawa watu sijui wapoje Jana asubuhi nilikuwa naingia zangu Kanisani nikiwa kwenye usafiri wa Umma(coaster), ilikuwa tumefika kwenye zebra(sinai) huku nikiwa nasoma zangu lesoni kwenye simu.

Ghafla naona mdada yupo juu ya boneti ya gari(land cruser-hard-top), huku pikipiki ipo chini huku bodaboda akirukaruka ile ya maumivu, kwa kifupi hata mimi nilibaki nimetahamaki kitendo cha boda boda kuigonga ile hard'-top na abiria wake wa kike karushwa toka kwenye siti ya nyuma hadi juu ya boneti.

Muda wa taa kusimama ukaisha lakini yule dada awali ni kama alidata pale juu ya gari na dalili zilionyesha yupo salama kabisa, sijui nini kiliendelea baada ya pale japo ni ajali lakini abiria kwenye gari ilibidi tucheke tuu kitendo cha yule dada kurushwa juu ya boneti " Wewe dada na bodaboda mlopta ajali pale sinai, asubuhi, sijui utamfanyia nini Mungu"

Jioni yake nikiwa narudi nyumbani mitaa ya nundu -meko, naona pikipiki ipo chini na kijana-dogo hivi yupo chali amezima haswa fahamu hana, kulia naona kijana mwingine analia-maumivu akiwa chini, mbele ya bajaji, sijui bodaboda aligonga bajaji au vipi, niombe alokuwa pale meko, yule kijana alokuwa amezima pale chini ile ajali ilitokeaje, je yule dogo alokuwa amezima pale chini alikuwa amedanja?

Kiufupi nazidi kuamini Uwepo wa Mungu kulingana na hayo matukio mawili ya jana kuhusiana na bodaboda kutotii sheria za barabarani.
 
Leo nlipita Kituo cha Mwendokasi Pale Kinondoni mkwajuni nkakuta Damu nyingi sana imetapakaa chini kwenye barabara ya mwendokasi inaonekana jana usiku kuna Ajali kubwa ilitokea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom