Morogoro: Bodaboda wawili wafariki dunia kwa kugongwa na Lori

Morogoro: Bodaboda wawili wafariki dunia kwa kugongwa na Lori

Leo hii njia ya moro ajali kibao, mikese tena nimekutana na ajali ya roli la mafuta wamegongana na gari ndogo ipo nyanganyanga, na vijana wanachota wese
Yaani hatukomi kuhusu kuchota wese
 
Boda boda haziruhusiwi kutumia highways, hii ni sheria isipokua politicians wanaangalia kura tu, ukubwa wa pikipiki hizi ni mdogo kuruhusiwa kutumia freeways, pia hawavai hermits za kujikinga na ajali ,ondoa bodaboda zote kwenye barabara kuu,Mbeya kwenye ile T1 ndio uchafu zaidi maana kuna bajaji ndani ya highway kibao
Tanzania hatuna freeway ndugu.
 
Aisee maisha ni mafupi nimepita Bwawani -Moro mida hii ya saa 1 jioni kuna bodaboda wawili wamekanyagwa vibaya sana na lorry, kiufupi wamekufa, yaani vichwa havieleweki.

Msinidai picha nimeshindwa kupiga
ALIYEUFANYA USAFIRI WA BODABODA KUWA WA KIBISHARA hakika anawamaliza Vijana wetu
 
Boda huwa nawahurumia sana,,ila sometimes wanakera kwakweli. Mfano Highways/barabara kuu wamewekewa njia zao kwa pembeni wao na PACHA zao daladala za baiskeli lakini wengi wao hawatumii njia hizo,, aise wasipojirekebisha wataendelea kufa.

Waabheja sana
 
Back
Top Bottom