Hawa watu sijui wapoje Jana asubuhi nilikuwa naingia zangu Kanisani nikiwa kwenye usafiri wa Umma(coaster), ilikuwa tumefika kwenye zebra(sinai) huku nikiwa nasoma zangu lesoni kwenye simu.
Ghafla naona mdada yupo juu ya boneti ya gari(land cruser-hard-top), huku pikipiki ipo chini huku bodaboda akirukaruka ile ya maumivu, kwa kifupi hata mimi nilibaki nimetahamaki kitendo cha boda boda kuigonga ile hard'-top na abiria wake wa kike karushwa toka kwenye siti ya nyuma hadi juu ya boneti.
Muda wa taa kusimama ukaisha lakini yule dada awali ni kama alidata pale juu ya gari na dalili zilionyesha yupo salama kabisa, sijui nini kiliendelea baada ya pale japo ni ajali lakini abiria kwenye gari ilibidi tucheke tuu kitendo cha yule dada kurushwa juu ya boneti " Wewe dada na bodaboda mlopta ajali pale sinai, asubuhi, sijui utamfanyia nini Mungu"
Jioni yake nikiwa narudi nyumbani mitaa ya nundu -meko, naona pikipiki ipo chini na kijana-dogo hivi yupo chali amezima haswa fahamu hana, kulia naona kijana mwingine analia-maumivu akiwa chini, mbele ya bajaji, sijui bodaboda aligonga bajaji au vipi, niombe alokuwa pale meko, yule kijana alokuwa amezima pale chini ile ajali ilitokeaje, je yule dogo alokuwa amezima pale chini alikuwa amedanja?
Kiufupi nazidi kuamini Uwepo wa Mungu kulingana na hayo matukio mawili ya jana kuhusiana na bodaboda kutotii sheria za barabarani.