Uchaguzi 2020 Morogoro: Devotha Minja amewasilisha fomu bila picha kitendo kinachomnyima sifa ya kuwa Mgombea

Ukisoma vizuri maelekezo ya ujazaji form no.4 wameainisha kabisa..picha 4 ziambatanishwe

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuambatanisha picha maana yake unapokabidhi form zako unawapa na picha zako, hujaambiwa ubandike kwenye form. unaweza hata ukazibana na pini kwenye Bahasha ndogo.
 
Picha ziambatanishwe na siyo zibandikwe kwenye fomu.

Abood Kama alibandika ni kosa.

Minja apite bila kupingwa.
Mpaka anakua disqualified means hata hakuambatanisha..achilia mbali kubandika..
Hakuweka picha kabisa.
 
Kwa Devotha mzoefu kusahau picha hainiingii akilini labda kama kavuta "FUNGU" ajitoe kama Nassari alivyofanya Kimya Kimya.
 
Inawezekana kabisa kuwa amewasilisha form zote 4 pamoja na picha 4 kama kifungu cha 4 kinavyosema. Inawezekana kabisa kuwa hizo picha hakuzibandika, kwani kipengele hicho hakisemi kuwa hizo picha zibandikwe.
 
Hata bwana yule hajaweka picha zake
 
Sasa anaepokea fomu alipokeaje hajaona picha....fukuzaa kazii hao mabwege wanaoshindwaa ata kuangalia picha wakati kuna vijana mtaani tupo tunaona mpakaa keshoo mamaye
 
Mbona sehemu ya kuweka picha haipo. Kila mmoja anaweza amua kuweka au kutoiweka
 
Wasimamizi wa uchaguzi hawatakiwi kufanya kazi Kama robot.Kosa la kusahau picha Ni kwa Nini mgombea asiruhusiwe kuziwazilisha Hata baada ya kuzisahau? Mambo mengine Ni ukosefu tu wa kutumia busara.Sio kosa linalomzuia Mbunge Bora kugombea ubunge.
 
Vyama vyote wanatakiwa wawe na watu maalum wa kukagua forms kama zimekamilika. Ni upuuzi kuwekeza uanachama kwa mapenzi mema kwenye vyama vyenu tukidhani mnajielewa kumbe mapunguwani tu . Imagine kikundi cha watu kinamsindikiza kurejesha form na kelele na shangwe kumbe hajakamilisha vipengele muhimu

Mtu kama huyu ni hata kubeba form ya mkopo wa kikoba chake huko mtaani akaacha kubeba form ya kugombea jimbo . Upuuzi huu ndio unanifanya nibakie mtazamaji tu . πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…