Morogoro: Fumanizi la Wapenzi lasababisha kifo

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Polisi mkoani Morogoro inamshikilia Salipina Thomas (21) mkazi wa kijiji cha Kiroka kwa tuhuma za mauaji ya Rashid Maharangande (20) aliyefumaniwa akiwa ndani ya chumba cha mwanamke huyo, huku anayedaiwa kuwafumania akitoweka kusikojulikana.

Akizungumza mjini Morogoro leo Jumamosi Septemba 17, Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Fortunatus Musilimu amesema mauaji hayo yametokea saa 8 usiku wa kuamkia Septemba 16, 2022 katika kitongoji cha Temekero tarafa ya Mkuyuni wilayani Morogoro.

Amesema mauaji hayo yanahusishwa na wivu wa kimapenzi ambapo kijana aitwaye Richard Stephen Chanzila (23) mkazi wa Kitongoji cha Maembe, Kijiji cha Kiloka ndiye anatuhumiwa kutekeleza mauaji hayo, baada ya kumkuta Maharagande akiwa amelala kwa Salpina ambaye ni mzazi mwenzake.

Kamanda Musilimu amesema, mtuhumiwa huyo inadaiwa alimkata na kitu chenye ncha kali shingoni kijana Mahalagande (20), mkazi wa Sultan Area, aliyekuwa dereva wa bodaboda.

Kamanda Musilimu amesema baada ya Maharagande kukatwa na kitu chenye ncha kali, mwanamke huyo alifanikiwa kukimbia na kwenda kuomba msaada.

Musilimu amesema, Chanzila baada ya kufanya mauaji hayo aliubeba mwili wa marehemu na kwenda kuutupa porini umbali wa mita 100 kutoka eneo alilofanyika mauaji.

Amesema mtuhumiwa huyo alikimbia kijijini hapo kwenda kusikojulikana baada ya mauaji hayo na Polisi inaendelea kumtafuta ili kumtia mbaroni na kufikishwa katika vyombo vya sheria ili kuchukua mkondo wake.

“Nawasihi wananchi ya kwamba kufanya mauaji ya aina mbalimbali kutokana na mapenzi, ushirikina au migogoro mbalimbali sio maamuzi sahihi, ni kinyume cha sheria, zipo njia ambazo zinaweza kutumika kupata suluhu ya mambo yanayojitokeza badala ya kuchukua maamuzi ya kuua mtu,” amesema Kamanda Musilimu.

Mwananchi
 
Na mwanamke anayezini na mwanaume yeye akili yake vipi!?
Maana naona lawama zote analundikiwa mwanaume 😣

Mwanamke akizini unatakiwa umwache tena kwa talaka kabisa. Na huyo hatakiwi kuolewa tena! Mungu mkaliiiiiii

Mathayo 5:32​

"Lakini mimi nawaambieni, anayempa mkewe talaka, isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, anamfanya azini; na mwanamume akimwoa mwanamke aliyepewa talaka, anazini."​

Polisi mkoani Morogoro inamshikilia Salipina Thomas (21) mkazi wa kijiji cha Kiroka kwa tuhuma za mauaji ya Rashid Maharangande (20) aliyefumaniwa akiwa ndani ya chumba cha mwanamke huyo, huku anayedaiwa kuwafumania akitoweka kusikojulikana.

Akizungumza mjini Morogoro leo Jumamosi Septemba 17, Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Fortunatus Musilimu amesema mauaji hayo yametokea saa 8 usiku wa kuamkia Septemba 16, 2022 katika kitongoji cha Temekero tarafa ya Mkuyuni wilayani Morogoro.

Amesema mauaji hayo yanahusishwa na wivu wa kimapenzi ambapo kijana aitwaye Richard Stephen Chanzila (23) mkazi wa Kitongoji cha Maembe, Kijiji cha Kiloka ndiye anatuhumiwa kutekeleza mauaji hayo, baada ya kumkuta Maharagande akiwa amelala kwa Salpina ambaye ni mzazi mwenzake.

Kamanda Musilimu amesema, mtuhumiwa huyo inadaiwa alimkata na kitu chenye ncha kali shingoni kijana Mahalagande (20), mkazi wa Sultan Area, aliyekuwa dereva wa bodaboda.

Kamanda Musilimu amesema baada ya Maharagande kukatwa na kitu chenye ncha kali, mwanamke huyo alifanikiwa kukimbia na kwenda kuomba msaada.

Musilimu amesema, Chanzila baada ya kufanya mauaji hayo aliubeba mwili wa marehemu na kwenda kuutupa porini umbali wa mita 100 kutoka eneo alilofanyika mauaji.

Amesema mtuhumiwa huyo alikimbia kijijini hapo kwenda kusikojulikana baada ya mauaji hayo na Polisi inaendelea kumtafuta ili kumtia mbaroni na kufikishwa katika vyombo vya sheria ili kuchukua mkondo wake.

“Nawasihi wananchi ya kwamba kufanya mauaji ya aina mbalimbali kutokana na mapenzi, ushirikina au migogoro mbalimbali sio maamuzi sahihi, ni kinyume cha sheria, zipo njia ambazo zinaweza kutumika kupata suluhu ya mambo yanayojitokeza badala ya kuchukua maamuzi ya kuua mtu,” amesema Kamanda Musilimu.

Mwananchi
Huyo ameibiwa mpenzi wake na hakuna SHERIA ya kumkamata na kumuadhibu mgoni wake zaidi ya madai .Hasira yake nani anaibeba.?
Kazi ya Dola ni kulipiza kisasi badala ya mwadhirika /Malamikaji na pia kutoa adhabu Kali Inayokomesha vitendo vinavyoleta madhara .

Serikali hili suala la SHERIA ya Ndoa inalichukulia kirahisi lakini vifo havitakoma mana ni dhambi inayogusa hisia za watu. Hakuna Mwanaume anayefurahi kuona mwanaume Mwenzake anaingilia mapenzi yake na kufarakanisha familia yake.
Hayupo hapa Duniani na hata Mbinguni.
Watauawa sana wasipobadikika na serikali isipobakaa na kutafakari suala la mauaji ya wanandoa itakuja kutengeneza kizazi kibaya zaidi ya hiki Cha Panya Road ambacho ni kizazi kilichotokana na serikali kushindwa kuweka SHERIA za kuzia uhalifu unaoyotokana na mipango mizuri ya ajira na mipango miji na kuachia kundi la watu wachache kuwa na maisha ya anasa huku wengine wakiwa kama watazamaji wa mpira.
 
Back
Top Bottom