Morogoro: Fumanizi la Wapenzi lasababisha kifo

Sehemu za siri bhana.
Acha kabisa we ziskiage hvy hvy.
Wala sio ishu.Tatizo ni SHERIA ya Ndoa ni inambeba Mwizi na haijali maumivu ya mwanye mke . Kama pangekua hakuna SHERIA Kali ya Kubaka mwanafunzi unategemea nani angewaacha wanafunzi wa sekondari walivyonona. Kwa hiyo watu wanavamia ndoa za watu na kuzivuruga wanavyotaka Kwa sababu hawana woga. Hivi nani atakubali kufungwa Kwa sababu ya kuiba mke wa mtu.? Yani ukikaa kwenye maofisi ,mitaani ,kwenye vijiwe watu wanazungumzia ngono TU na kuwalenga wake na waume za watu.
Wake za watu wamekua rahisi na waume za watu ndio ATM ya Wanawake mchanganyiko walioolewa wasioolewa wanaobinua makalio.
Vijana hawana Tena mademu Wazuri.
Pisi Kali zote ziko na wanaume wa watu.
Taifa na kizazi kinaelekea wapi?

Serikali iliangalie suala hili Kwa jicho la tatu.
Viongozi wa dini nao hawana Tena msaada wa kukemea dhambi mana nao ni sehemu ya uharibifu huo. Kilichobaki ni serikali kutunga SHERIA Kali ya Ndoa.

Tutakua na serikali na Bunge la ajabu kama litaacha jambo linalosababisha mauaji na mayatima kila kukicha bila kukitungia SHERIA Kali ya kudhibiti wanaosababisha . Kama Kuna SHERIA ya kuzuia Bangi na Gongo ambayo Haina madhara ya vifo makubwa kama ugoni inashindiakana Nini kutunga SHERIA ya kudhibiti wachepuka.Tumebeba masheria ya hovyo ya Kizungu .
 
Wao wenyewe wanashiriki hiyo michezo Leo waje kutunga Sheria sidhani. Acha tuuwane labda wataona na kuskia.
 
Huyo ameibiwa mpenzi wake na hakuna SHERIA ya kumkamata na kumuadhibu mgoni wake zaidi ya madai .Hasira yake nani anaibeba.?
Kazi ya Dola ni kulipiza kisasi badala ya mwadhirika /Malamikaji na pia kutoa adhabu Kali Inayokomesha vitendo vinavyoleta madhara .

Serikali hili suala la SHERIA ya Ndoa inalichukulia kirahisi lakini vifo havitakoma mana ni dhambi inayogusa hisia za watu. Hakuna Mwanaume anayefurahi kuona mwanaume Mwenzake anaingilia mapenzi yake na kufarakanisha familia yake.
Hayupo hapa Duniani na hata Mbinguni.
Watauawa sana wasipobadikika na serikali isipobakaa na kutafakari suala la mauaji ya wanandoa itakuja kutengeneza kizazi kibaya zaidi ya hiki Cha Panya Road ambacho ni kizazi kilichotokana na serikali kushindwa kuweka SHERIA za kuzia uhalifu unaoyotokana na mipango mizuri ya ajira na mipango miji na kuachia kundi la watu wachache kuwa na maisha ya anasa huku wengine wakiwa kama watazamaji wa mpira.
Ndio ukweli hata mimi ikitokea ntafanya kama alivyofanywa huyo tuendelee tu kusubiri matukio mengine mengi.
 
Polisi mkoani Morogoro inamshikilia Salipina Thomas (21) mkazi wa kijiji cha Kiroka kwa tuhuma za mauaji ya Rashid Maharangande (20) aliyefumaniwa akiwa ndani ya chumba cha mwanamke huyo, huku anayedaiwa kuwafumania akitoweka kusikojulikana.

Akizungumza mjini Morogoro leo Jumamosi Septemba 17, Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Fortunatus Musilimu amesema mauaji hayo yametokea saa 8 usiku wa kuamkia Septemba 16, 2022 katika kitongoji cha Temekero tarafa ya Mkuyuni wilayani Morogoro.

Amesema mauaji hayo yanahusishwa na wivu wa kimapenzi ambapo kijana aitwaye Richard Stephen Chanzila (23) mkazi wa Kitongoji cha Maembe, Kijiji cha Kiloka ndiye anatuhumiwa kutekeleza mauaji hayo, baada ya kumkuta Maharagande akiwa amelala kwa Salpina ambaye ni mzazi mwenzake.

Kamanda Musilimu amesema, mtuhumiwa huyo inadaiwa alimkata na kitu chenye ncha kali shingoni kijana Mahalagande (20), mkazi wa Sultan Area, aliyekuwa dereva wa bodaboda.

Kamanda Musilimu amesema baada ya Maharagande kukatwa na kitu chenye ncha kali, mwanamke huyo alifanikiwa kukimbia na kwenda kuomba msaada.

Musilimu amesema, Chanzila baada ya kufanya mauaji hayo aliubeba mwili wa marehemu na kwenda kuutupa porini umbali wa mita 100 kutoka eneo alilofanyika mauaji.

Amesema mtuhumiwa huyo alikimbia kijijini hapo kwenda kusikojulikana baada ya mauaji hayo na Polisi inaendelea kumtafuta ili kumtia mbaroni na kufikishwa katika vyombo vya sheria ili kuchukua mkondo wake.

“Nawasihi wananchi ya kwamba kufanya mauaji ya aina mbalimbali kutokana na mapenzi, ushirikina au migogoro mbalimbali sio maamuzi sahihi, ni kinyume cha sheria, zipo njia ambazo zinaweza kutumika kupata suluhu ya mambo yanayojitokeza badala ya kuchukua maamuzi ya kuua mtu,” amesema Kamanda Musilimu.

Mwananchi
duh,hiyo familia ya marehemu Kama nawafahamu, Kuna ndugu yao alikuwa diwani nadhani
 
Mwanamke akizini unatakiwa umwache tena kwa talaka kabisa. Na huyo hatakiwi kuolewa tena! Mungu mkaliiiiiii

Mathayo 5:32​

"Lakini mimi nawaambieni, anayempa mkewe talaka, isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, anamfanya azini; na mwanamume akimwoa mwanamke aliyepewa talaka, anazini."​

Talaka huko zinaruhusiwa?
 
Musilimu amesema, Chanzila baada ya kufanya mauaji hayo aliubeba mwili wa marehemu na kwenda kuutupa porini umbali wa mita 100 kutoka eneo alilofanyika mauaji.
 
Shetani hana maana anakupeleka kufanya zinaa halafu anahakikisha umefia kwenye hiyohiyo zinaa

MITHALI 6:32​

Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.​

Na mtu anayezini na mbwa?

Au ili mtu awe na akili anapaswa kuzini na nani?
 
Polisi mkoani Morogoro inamshikilia Salipina Thomas (21) mkazi wa kijiji cha Kiroka kwa tuhuma za mauaji ya Rashid Maharangande (20) aliyefumaniwa akiwa ndani ya chumba cha mwanamke huyo, huku anayedaiwa kuwafumania akitoweka kusikojulikana.

Akizungumza mjini Morogoro leo Jumamosi Septemba 17, Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Fortunatus Musilimu amesema mauaji hayo yametokea saa 8 usiku wa kuamkia Septemba 16, 2022 katika kitongoji cha Temekero tarafa ya Mkuyuni wilayani Morogoro.

Amesema mauaji hayo yanahusishwa na wivu wa kimapenzi ambapo kijana aitwaye Richard Stephen Chanzila (23) mkazi wa Kitongoji cha Maembe, Kijiji cha Kiloka ndiye anatuhumiwa kutekeleza mauaji hayo, baada ya kumkuta Maharagande akiwa amelala kwa Salpina ambaye ni mzazi mwenzake.

Kamanda Musilimu amesema, mtuhumiwa huyo inadaiwa alimkata na kitu chenye ncha kali shingoni kijana Mahalagande (20), mkazi wa Sultan Area, aliyekuwa dereva wa bodaboda.

Kamanda Musilimu amesema baada ya Maharagande kukatwa na kitu chenye ncha kali, mwanamke huyo alifanikiwa kukimbia na kwenda kuomba msaada.

Musilimu amesema, Chanzila baada ya kufanya mauaji hayo aliubeba mwili wa marehemu na kwenda kuutupa porini umbali wa mita 100 kutoka eneo alilofanyika mauaji.

Amesema mtuhumiwa huyo alikimbia kijijini hapo kwenda kusikojulikana baada ya mauaji hayo na Polisi inaendelea kumtafuta ili kumtia mbaroni na kufikishwa katika vyombo vya sheria ili kuchukua mkondo wake.

“Nawasihi wananchi ya kwamba kufanya mauaji ya aina mbalimbali kutokana na mapenzi, ushirikina au migogoro mbalimbali sio maamuzi sahihi, ni kinyume cha sheria, zipo njia ambazo zinaweza kutumika kupata suluhu ya mambo yanayojitokeza badala ya kuchukua maamuzi ya kuua mtu,” amesema Kamanda Musilimu.

Mwananchi
Haya ni mauaji ya pili kutokea huko Kiloka kwa style hiyohiyo mwaka huu
 
Shetani hana maana anakupeleka kufanya zinaa halafu anahakikisha umefia kwenye hiyohiyo zinaa

MITHALI 6:32​

Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.​

Shetani kasingiziwa, labda ni hii hapa

280686486_113455474696652_5428223777758762508_n.jpg
 
Na mtu anayezini na mbwa?

Au ili mtu awe na akili anapaswa kuzini na nani?

TORATI 27:21​

Na alaaniwe alalaye na mnyama wa aina yo yote. Na watu wote waseme, Amina.​

TORATI 28:15;21-28
15 Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata.
21 Bwana atakuambatanisha na tauni, hata atakapokwisha kukuondoa katika nchi uingiayo kwa kuimiliki.
22 Bwana atakupiga kwa kifua kikuu, na kwa homa, na kwa kuwashwa, na kwa hari ya moto, na kwa upanga, na kwa ukaufu, na kwa koga; navyo vitakufukuza hata uangamie.
23 Na mbingu zako zilizo juu ya kichwa chako zitakuwa shaba, na nchi iliyo chini yako itakuwa chuma.
24 Bwana atafanya mvua ya nchi yako iwe vumbi na mchanga; itakujilia juu yako kutoka mbinguni hata uangamie.
25 Bwana atakufanya upigwe mbele ya adui zako; utawatokea juu yao kwa njia moja, lakini utakimbia mbele yao kwa njia saba; nawe utatupwa huko na huko katika falme zote za duniani.
26 Na mzoga wako utakuwa chakula cha ndege wote wa angani, na wanyama wote wa duniani, pasiwe na mtu wa kuwafukuza.
27 Bwana atakupiga kwa majipu ya Misri, na kwa bawasiri, na kwa pele, na kwa kujikuna, ambayo hupati kupoa.
28 Bwana atakupiga kwa wazimu, na kwa upofu, na kwa bumbuazi la moyoni;
29 utakwenda kwa kupapasa-papasa mchana, kama apapasavyo kipofu gizani, wala hufanikiwi katika njia zako; nawe sikuzote utaonewa na kutekwa nyara, wala hapatakuwa na mtu wa kukuokoa.
30 Utaposa mke na mume mwingine atalala naye; utajenga nyumba usiikae; utapanda mizabibu usitumie matunda yake.
 
Back
Top Bottom