Morogoro: Fumanizi la Wapenzi lasababisha kifo

Polisi mkoani Morogoro inamshikilia Salipina Thomas (21) mkazi wa kijiji cha Kiroka kwa tuhuma za mauaji ya Rashid Maharangande (20) aliyefumaniwa akiwa ndani ya chumba cha mwanamke huyo, huku anayedaiwa kuwafumania akitoweka kusikojulikana.

Akizungumza mjini Morogoro leo Jumamosi Septemba 17, Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Fortunatus Musilimu amesema mauaji hayo yametokea saa 8 usiku wa kuamkia Septemba 16, 2022 katika kitongoji cha Temekero tarafa ya Mkuyuni wilayani Morogoro.

Amesema mauaji hayo yanahusishwa na wivu wa kimapenzi ambapo kijana aitwaye Richard Stephen Chanzila (23) mkazi wa Kitongoji cha Maembe, Kijiji cha Kiloka ndiye anatuhumiwa kutekeleza mauaji hayo, baada ya kumkuta Maharagande akiwa amelala kwa Salpina ambaye ni mzazi mwenzake.

Kamanda Musilimu amesema, mtuhumiwa huyo inadaiwa alimkata na kitu chenye ncha kali shingoni kijana Mahalagande (20), mkazi wa Sultan Area, aliyekuwa dereva wa bodaboda.

Kamanda Musilimu amesema baada ya Maharagande kukatwa na kitu chenye ncha kali, mwanamke huyo alifanikiwa kukimbia na kwenda kuomba msaada.

Musilimu amesema, Chanzila baada ya kufanya mauaji hayo aliubeba mwili wa marehemu na kwenda kuutupa porini umbali wa mita 100 kutoka eneo alilofanyika mauaji.

Amesema mtuhumiwa huyo alikimbia kijijini hapo kwenda kusikojulikana baada ya mauaji hayo na Polisi inaendelea kumtafuta ili kumtia mbaroni na kufikishwa katika vyombo vya sheria ili kuchukua mkondo wake.

“Nawasihi wananchi ya kwamba kufanya mauaji ya aina mbalimbali kutokana na mapenzi, ushirikina au migogoro mbalimbali sio maamuzi sahihi, ni kinyume cha sheria, zipo njia ambazo zinaweza kutumika kupata suluhu ya mambo yanayojitokeza badala ya kuchukua maamuzi ya kuua mtu,” amesema Kamanda Musilimu.

Mwananchi
Hasira na stress za tozo zinaibua maroho ya mauaji yaliyotokomea kitambo

Inauma haya mauaji
 
Huyo ameibiwa mpenzi wake na hakuna SHERIA ya kumkamata na kumuadhibu mgoni wake zaidi ya madai .Hasira yake nani anaibeba.?
Kazi ya Dola ni kulipiza kisasi badala ya mwadhirika /Malamikaji na pia kutoa adhabu Kali Inayokomesha vitendo vinavyoleta madhara .

Serikali hili suala la SHERIA ya Ndoa inalichukulia kirahisi lakini vifo havitakoma mana ni dhambi inayogusa hisia za watu. Hakuna Mwanaume anayefurahi kuona mwanaume Mwenzake anaingilia mapenzi yake na kufarakanisha familia yake.
Hayupo hapa Duniani na hata Mbinguni.
Watauawa sana wasipobadikika na serikali isipobakaa na kutafakari suala la mauaji ya wanandoa itakuja kutengeneza kizazi kibaya zaidi ya hiki Cha Panya Road ambacho ni kizazi kilichotokana na serikali kushindwa kuweka SHERIA za kuzia uhalifu unaoyotokana na mipango mizuri ya ajira na mipango miji na kuachia kundi la watu wachache kuwa na maisha ya anasa huku wengine wakiwa kama watazamaji wa mpira.
🤣🤣🤣Hapo kwanza nicheke!! Hao wote unaweza Kuta ni vibaka unakamata vip mgoni wako kama mke haujamuoa?

Fuatilia hapo huyo jamaa kazaa na demu tu inawezekana hajamuoa vyote vichalii sasa hapo aliyemaliza mwenzie ni jela moja kwa moja.
 
Ohooo, wazee naomba tushirikiane kumtafta na kumtag mzabzab kwa sababu zifuatazo
1. Ni boda boda
2. Yuko morogoro
3. Anapenda mbususu kuliko hata maisha yake.
4. Hatujui jina lake halisi
This is serious aisee usikute mzee wa mbususu tayari kala nchale
 
Polisi mkoani Morogoro inamshikilia Salipina Thomas (21) mkazi wa kijiji cha Kiroka kwa tuhuma za mauaji ya Rashid Maharangande (20) aliyefumaniwa akiwa ndani ya chumba cha mwanamke huyo, huku anayedaiwa kuwafumania akitoweka kusikojulikana.

Akizungumza mjini Morogoro leo Jumamosi Septemba 17, Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Fortunatus Musilimu amesema mauaji hayo yametokea saa 8 usiku wa kuamkia Septemba 16, 2022 katika kitongoji cha Temekero tarafa ya Mkuyuni wilayani Morogoro.

Amesema mauaji hayo yanahusishwa na wivu wa kimapenzi ambapo kijana aitwaye Richard Stephen Chanzila (23) mkazi wa Kitongoji cha Maembe, Kijiji cha Kiloka ndiye anatuhumiwa kutekeleza mauaji hayo, baada ya kumkuta Maharagande akiwa amelala kwa Salpina ambaye ni mzazi mwenzake.

Kamanda Musilimu amesema, mtuhumiwa huyo inadaiwa alimkata na kitu chenye ncha kali shingoni kijana Mahalagande (20), mkazi wa Sultan Area, aliyekuwa dereva wa bodaboda.

Kamanda Musilimu amesema baada ya Maharagande kukatwa na kitu chenye ncha kali, mwanamke huyo alifanikiwa kukimbia na kwenda kuomba msaada.

Musilimu amesema, Chanzila baada ya kufanya mauaji hayo aliubeba mwili wa marehemu na kwenda kuutupa porini umbali wa mita 100 kutoka eneo alilofanyika mauaji.

Amesema mtuhumiwa huyo alikimbia kijijini hapo kwenda kusikojulikana baada ya mauaji hayo na Polisi inaendelea kumtafuta ili kumtia mbaroni na kufikishwa katika vyombo vya sheria ili kuchukua mkondo wake.

“Nawasihi wananchi ya kwamba kufanya mauaji ya aina mbalimbali kutokana na mapenzi, ushirikina au migogoro mbalimbali sio maamuzi sahihi, ni kinyume cha sheria, zipo njia ambazo zinaweza kutumika kupata suluhu ya mambo yanayojitokeza badala ya kuchukua maamuzi ya kuua mtu,” amesema Kamanda Musilimu.

Mwananchi
Jamaa kafa kisa mbususu, bodaboda wanazngua sana kaifungia safari mbususu😀😀
 
Ohooo, wazee naomba tushirikiane kumtafta na kumtag mzabzab kwa sababu zifuatazo
1. Ni boda boda
2. Yuko morogoro
3. Anapenda mbususu kuliko hata maisha yake.
4. Hatujui jina lake halisi
This is serious aisee usikute mzee wa mbususu tayari kala nchale
Aise nashukuru kwa kunijulia hali....bwana huyu bodaboda mwezetu tulimkanya mara kibao mambo ya kulala gheto la mwanamke sio...bora utuombe wana tukuoe gheto hakusikia...sasa tupo hapa tunafarijiana tuu.
Ila napiga mkakati na mie nikaonje utamu aliokuwa anapata maharagande
 
Niliwahi andika hapa, juu ya vijana wa bodaboda kutokana na kuwa na mzunguko mkubwa wa fedha (kipato chake sio mpaka mwisho wa mwezi).
Wengi wana mahusiano na wanawake wengi,wengine ni wake za wenyewe.Anaweza kutenga 4000 ya kununua nusu kilo ya nyama kila siku kwa ajili ya mke wa mtu. Au anaweza kulipia fedha ya vikoba ya wanawake kadha kila siku. Au kuwa na mahusiano na mwanafunzi wa kike, binti akiamini uhakika wa usafiri kila siku anao.

Ukiisha mgundua kama ni mume mwenza, unachofanya ni kutafuta wadau wamkodishe muda mbaya na kwenda naye sehemu mbaya. Huko unachapa mtu na kuondoka na pikipiki, ambayo una kuja kuuza kama spare au chuma chakavu.
Uwezo wao wa kuweka AKIBA, wakafanya makubwa hawana.na kazi ile ina chanagamoto nyingi barabarani, leo una chombo kesho huna. leo umepata ajali na kuvunja mguu au mkono na kulala kwa miezi kadha hospital.
VYEMA KUWEKA AKIBA, NI VYEMA KUHESHIMU MAHUSIANO YA WENGINE
 
Aise nashukuru kwa kunijulia hali....bwana huyu bodaboda mwezetu tulimkanya mara kibao mambo ya kulala gheto la mwanamke sio...bora utuombe wana tukuoe gheto hakusikia...sasa tupo hapa tunafarijiana tuu.
Ila napiga mkakati na mie nikaonje utamu aliokuwa anapata maharagande
🤣🤣🤣🤣🤣 kwaio alichopata mwamba hakijatosha na we unataka ukatest zali?
 
Aise nashukuru kwa kunijulia hali....bwana huyu bodaboda mwezetu tulimkanya mara kibao mambo ya kulala gheto la mwanamke sio...bora utuombe wana tukuoe gheto hakusikia...sasa tupo hapa tunafarijiana tuu.
Ila napiga mkakati na mie nikaonje utamu aliokuwa anapata maharagande
Wee jamaa chizi Sana[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Na bado watauana sana, si wanajifanya wao ni malijari na mapenzi wanayajua, watakwisha mnooo.

Vijana wadogo wanakimbilia mapenziii. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom