Kwa mantiki haya Wapinzani hawakufanya kazi nzuri ya kuwaelimisha wananchi wa kule juu ya ubaya wa CCM. Katika maeneo amabayo wapinzani wanakubalika ni yale yenye maendeleo yaliyoletwa na CCM.Elimu imepelekwa kwenye maeneo hayo na CCM, miundo mbinu mingine kama vile barabara reli, maji na umeme katika maeneo wanayopendwa wapinzani imepelekwa na serikali ya CCM ila ndiyo kawaida usimwamshe aliyelala utalala wewe. Rasilmali zilizoendeleza maeneo mnayosema ni ya wapinzani ni za watanzania wote zingeweza kupelekwa kuendeleza Morogoro kusini lakini zikapelekwa maeneo mengine kwa kuwa watendaji wa serikali walikuwa wa maeneo yale. Maendeleo hayo hayakuletwa na wabunge wao.
Wapinzani hawajawahi kushika serikali hivyo siyo kweli kwamba penye maendeleo maendeleo pana wapinzani wapinzani. Maendeleo yana sababu nyingi ikiwemo miundo mbinu ambayo hujengwa na serikali, utamaduni wa wananchi kupenda kazi na mambo mengine mengi.