Morogoro Kusini, Wilaya masikini kuliko zote Tanzania

Morogoro Kusini, Wilaya masikini kuliko zote Tanzania

.....kuna mtu alisema mluguru ukimpa kofia ya fisiem au kanga halafu ukamwambia anywe sumu ili uone kama inaua anakunywa........(mtu akikunyima elimu kakunyima vitu vingi sana .....hawa watu wawapendi ndugu zetu waelimike kwa sababu wakielimika hawawachagui)........pole zenu njooni huku kasikazini kuna unafuu...
Ujinga unatutafuna sisi waluguru na utaendelea kututafuna
 
Cha ajabu huenda una degree ila upeo wako uko chini sana hebu niambie barabara ina uhusiano gani na kujituma kwa wananchi.Wapeni wananchi yale mliyowaahidi MUNGU anawaona mlivyo wanafiki

Mjinga huyo. Ten barabara mbovu na miundombinu mingine mibovu ndiyo inafanya watu wakose moyo wa uwajibikaji.
 
Wilaya kama hizi ni nyingi sana. Na, binafsi wala siwashangai Wananchi hao kwa kuipigia kura CCM; maana ndiyo ufahamu wao umeishia hapo.

Lakini, si wakati wote ufumbuzi wa matatizo yetu ni kuchagua Upinzani; Vyama vya Upinzani havipati Wanachama toka Germany, Viongozi wao na Wanachama wanatoka miongoni mwetu sisi hawa hawa. Halmashauri Manispaa ya Musoma ilikuwa ya CHADEMA, nini cha maana sana kilichofanyika kule? UKAWA watasingizia waliibiwa kura.

Lakni wana musoma ni watu wenye upeo mpana kuliko maeneo ambayo ccm wameyakalia kwa miaka yote
 
Lakni wana musoma ni watu wenye upeo mpana kuliko maeneo ambayo ccm wameyakalia kwa miaka yote

Ishu ni kwamba je kuna maendeleo? Upeo mpana peke yake hautoshi. Hata utumbo upo utumbo mpana
 
Ishu ni kwamba je kuna maendeleo? Upeo mpana peke yake hautoshi. Hata utumbo upo utumbo mpana

Maendeleo ya aina gani na yaletwe na nani? Mf.barabara au hospital au maji nani anatakiwa awpelekee wananchi kama sio nyie mnao kusanya kodi msikwepe wajibu wenu hivyo nilivyo vitaja hapo juu sio kazi ya mbunge
 
Maendeleo ya aina gani na yaletwe na nani? Mf.barabara au hospital au maji nani anatakiwa awpelekee wananchi kama sio nyie mnao kusanya kodi msikwepe wajibu wenu hivyo nilivyo vitaja hapo juu sio kazi ya mbunge

Kodi inalipwa ila shida kwa hao wanaokusanya kodi
 
Waache waendelee kuisoma... wameipenda wenyewe
 
Watu wa morogoro mjini,vijijini,kilosa,mvomero na gairo wote ------- sana.
 
Wanakera sana watu wa morogoro yaani hawajiamini wao kwa wao. Usishangae wakimuona mwarabu hata mtoto wanamwakia. Ni mkoa wangu ila kuna baadhi ya maeneo wananichukiza sana. Bora kilombero iwe mkoa tuhamie mkoa mpya wa kilombero maana kule wameamka
 
Nchi hii ni hovyo sana watu tunaongelea maendeleo kwa wananchi jitu linakuja na habari za Mbowe hivi mbowe ndy mkusanya kodi au yeye ndy amesababisha tufike hapa tulipo
 
Wilaya hii makao makuu yake yapo moro mjini kwa kuwa watendaji wengi wa wilaya hii wanakwepa maisha ya dhiki yasiyo stahili kuishi binadamu ndani ya wilaya.

ELIMU:
-Wilaya ya Morogoro hakuna hata shule moja ya Advance level (kidato cha tano na sita).
-Shule za msingi zilizopo ni duni chakavu tena zilizochoka.
-Hakuna walimu wa kutosha. Kuna shule kama shile ya msingi kitengu, lumba chini na lumba juu kuna mwalimu mmoja mmoja kila shule.
Mbunge ni wa ccm.

AFYA:

Wilaya hii hakuna hospital yenye hadhi ya kuwa hospital ya wilaya. Kuna kituo cha afya cha tawa eti ndo wanataka kuifanya hospital ya wilaya. Kiukweli haina hadhi, kama ingekuwa Dar hii ingekuwa zahanati.
Mbunge ni wa ccm.

BARABARA:
Unaweza ukafikiri kama nafanya uchochezi au masihara ila ukweli ni kwamba HAKUNA HATA MITA MOJA ya kipande cha lami. Barabara huku kwetu ni za vumbi zilizojaa makorongo zinazohatarisha safari.
Mbunge ni wa ccm.

UONEVU:
wananchi wanaonewa kwa kulipishwa michango na faini zisizo na tija. Kuna mpango wa kila kata kuchangia shilingi elfu moja kulipia vyanzo vya maji mpango huu unaratibiwa na shirika na CARE INTERNATIONAL. Wakati mito Mungu mwenyewe ndiyo kaiumba na ipo tu siku zote toka utotoni kwa bibi na babu zetu na tulikuwa tunatumia bure.
Mbunge ni wa CCM.

Lakini pamoja na yote hayo wananchi wameridhika na ccm huwaambii kitu juu ya CCM yao.
Huku mgombea akishapitishwa na CCM basi yeye ndiye mshindi kwa asilimia 90. Haijawahi pata kiongozi wa upinzani ingawa mwaka 2005 - 2010 tulikuwa na diwani mmoja tu wa chadema kata ya kibungo juu.

Wananchi tumeamua kujisemea wenyewebkwa kuwa masikini wachache na wajinga wachache wanatuumiza sisi kwa kuendelea kuichagua ccm.

Acha kudangaya watu wewe. hakuna wilaya ya Morogoro kusini. kimazingira nimeelewa unaongelea wapi. Huko barabara ni nzuri na inapitika mwaka mzima tokea Morogoro mjini mpaka Kisaki. na watu wana maisha ya kawaida kama watanzania wengine.
Mimi kama mtanzania ninajua maisha yetu ni magumu yamezungukwa na fursa nyingi ila tumetiwa upofu na watawala tusione. wanajamvi msinielewe vibaya. najua maisha ya watz yanafananafanana.
 
Wanakera sana watu wa morogoro yaani hawajiamini wao kwa wao. Usishangae wakimuona mwarabu hata mtoto wanamwakia. Ni mkoa wangu ila kuna baadhi ya maeneo wananichukiza sana. Bora kilombero iwe mkoa tuhamie mkoa mpya wa kilombero maana kule wameamka

Kama ukiwa mkoa, tukutane IFAKARA
 
Back
Top Bottom