Abel Ndundulu
JF-Expert Member
- Sep 17, 2015
- 846
- 388
Nakubaliana na wewe ndugu, barabara zenu ni mbaya sana. Nimefika Mvuha mara ya kwanza mwaka huu, kwa kweli malalamiko yako ni genuine kabisa. Kesho pia naenda kijiji cha Kongwa, kule karibu na mbuga ya Selous, huko tunapita kwenye miti tu ili kufika kijijini, kwa sababu hakuna barabaya ya gari ya kueleweka ili kufika kijijini Kongwa. Kuna mradi nautekeleza kule, wa kuwapekelea umeme watu wa kijiji cha Kongwa. Ilituwia vigumu sana kupeleka mitambo wakati wa mvua, kwa kuwa njia hazipitiki kirahisi kabisa. Poleni sana
Sipati picha ya Wilaya mpya ya Malinyi huko Ulanga Magharibi.Hali ni tete kuliko hii Morogoro Kusini mnayoizungumzia.Mbaya zaidi CCM ni kama imeota mizizi maana asilimia kubwa ya Wananchi wa huko hawaoni kama CCM ndio kikwazo cha maendeleo yao.
Pole kwa watanzania wote. Ila vp kwa maeneo ya Iringa?
Hali ikoje...hiyo ya Ileje kuna rafiki yangu aliacha kazi ya serikali baada ya kukaa mwezi mmoja tu kule...
Walioenda Tandahimba , Simiyu wanakubali mazingira ni poa.
Kongwa ipo kata ya mvuha imepakana na kata ya selembala. Karibu moro (v) tusemayo yapo hatutanii
Hahaaa. Nilitembelea Malinyi mwanzoni mwa mwaka huu yaani ni shida. Barabara ni mbovu na matukio ya utekaji wa magari kwenye pori la Nambiga yalikuwa yameshamili. Ni eneo ambalo limeongozwa na kiongozi mzito wa serikali ndugu Ngasongwa kwa muda mrefu. Sasa hivi yupo ndugu Haji Mponda kwa awamu ya pili sasa. Ni eneo muhimu sana kwa uzalishaji wa mpunga na kwasasa kunafanyika tafiti za mafuta na gesi kwenye Bonde hilo lakini bado ni eneo lenye miundombinu mibovu kabisa.
Afadhali mkuyuni njiani je sisi kwetu kibungo juu, nyingwa huko.Mkuyuni kwetu, daaah ile barabara inakera Sana yani
hapa ndio mahali pa kuweka wazi kila kitu , usikae na donge moyoni .Msalieni mtume jamani, hivi mumeshawahi kufika vijiji vya wilaya ya Liwale ?????
wajomba naombeni niwafute machozi , cdm ishasogea karibu sana .Nyingwa hatari jombaaa
Hiyo chorus yako ya "mbunge wa ccm" mi hoi.Wilaya hii makao makuu yake yapo moro mjini kwa kuwa watendaji wengi wa wilaya hii wanakwepa maisha ya dhiki yasiyo stahili kuishi binadamu ndani ya wilaya.
ELIMU:
-Wilaya ya Morogoro hakuna hata shule moja ya Advance level (kidato cha tano na sita).
-Shule za msingi zilizopo ni duni chakavu tena zilizochoka.
-Hakuna walimu wa kutosha. Kuna shule kama shile ya msingi kitengu, lumba chini na lumba juu kuna mwalimu mmoja mmoja kila shule.
Mbunge ni wa ccm.
AFYA:
Wilaya hii hakuna hospital yenye hadhi ya kuwa hospital ya wilaya. Kuna kituo cha afya cha tawa eti ndo wanataka kuifanya hospital ya wilaya. Kiukweli haina hadhi, kama ingekuwa Dar hii ingekuwa zahanati.
Mbunge ni wa ccm.
BARABARA:
Unaweza ukafikiri kama nafanya uchochezi au masihara ila ukweli ni kwamba HAKUNA HATA MITA MOJA ya kipande cha lami. Barabara huku kwetu ni za vumbi zilizojaa makorongo zinazohatarisha safari.
Mbunge ni wa ccm.
UONEVU:
wananchi wanaonewa kwa kulipishwa michango na faini zisizo na tija. Kuna mpango wa kila kata kuchangia shilingi elfu moja kulipia vyanzo vya maji mpango huu unaratibiwa na shirika na CARE INTERNATIONAL. Wakati mito Mungu mwenyewe ndiyo kaiumba na ipo tu siku zote toka utotoni kwa bibi na babu zetu na tulikuwa tunatumia bure.
Mbunge ni wa CCM.
Lakini pamoja na yote hayo wananchi wameridhika na ccm huwaambii kitu juu ya CCM yao.
Huku mgombea akishapitishwa na CCM basi yeye ndiye mshindi kwa asilimia 90. Haijawahi pata kiongozi wa upinzani ingawa mwaka 2005 - 2010 tulikuwa na diwani mmoja tu wa chadema kata ya kibungo juu.
Wananchi tumeamua kujisemea wenyewebkwa kuwa masikini wachache na wajinga wachache wanatuumiza sisi kwa kuendelea kuichagua ccm.