Morogoro: Lori la Mafuta lapata ajali na kulipuka, watu 104 Wapoteza maisha na wengine kujeruhiwa...(Picha zinaogofya)

Morogoro: Lori la Mafuta lapata ajali na kulipuka, watu 104 Wapoteza maisha na wengine kujeruhiwa...(Picha zinaogofya)

Aisee janga kubwa hili. Watu hawana elimu ya kutosha juu ya majanga
 
Hapo kuna mjinga mmoja aliwawashia maana inaonesha baada ya kudondoka watu walienda chota.
Wengi inaonesha ni wa pikipiki
 
Hizi ajali za watu kuungua mafuta wakichota kwenye malori yaliyoanguka nazisikia mara nyingi sana nikiwa tangu mdogo,
sasa unajiuliza hivi watu hawajifunzi?
unajiuliza hata kama watu ni masikini kiasi gani, utaendaje kubet maisha yako kwenye mafuta ya 10,000 au 20,000?

Matatizo, umaskini na shida huwa zinapumbaza uwezo wa mtu kufikiri sawa sawa
 
Duuh hapa kuwa na askari wa kuwazuia?
Wamesahau ile ajali ya Iringa miaka kadhaa nyuma. Karibu kijiji kizima kiliteketea sababu ya kusombelea mafuta ya bure. Moto ukishika unafata mtiririko wa matone ya mafuta yalipoenda, hivo hadi nyumba ziliungua.
May their soul Rest In Peace.
Siyo Iringa, ni Mbeya milima ya Uporoto kuelekea Tukuyu ambapo mtanashati John alisababisha moto ulipuke baada ya kujaribu kuiba betri, wenye sufuria hata, wenye vijiko nao wamo, wenye madumu twende, kaburi lao la pamoja lipo kando ya barabara.
 
Duuh hapa kuwa na askari wa kuwazuia?

Wamesahau ile ajali ya Iringa miaka kadhaa nyuma. Karibu kijiji kizima kiliteketea sababu ya kusombelea mafuta ya bure. Moto ukishika unafata mtiririko wa matone ya mafuta yalipoenda, hivo hadi nyumba ziliungua.

May their soul Rest In Peace.
Kila siku watu wanapigiwa kelele waache huu upuuzi hawaelewi.

Ni tabia za kipumbavu kabisa, mwenzako anapata ajali wewe unafurahia kwenda kufaidika na ajali.
​
 
Aisee hatari sana. Katika vitu ambavyo watu hawana uelewa navyo kwa kiasi kikubwa ni malori ya mafuta. wengi huwa tunayachukulia kama magari mengine tuu ila ni hatari sana.
Sio malori ya mafuta tu mara kadhaa pia tumelalamikia tabia ya mabasi ya abiria kuingia sheli na abiria lakini mamlaka husika zimekaa kimya ipo siku tutapata majanga makubwa sana Mungu atuepudshe.
 
Ni jambo la kusikitisha sana.
Tumepoteza nguvu kazi ya Taifa na pia familia zimepoteza wapendwa wao waliokuwa wanawategemea.

MUHIMU:
Tujifunze na tufuate maelekezo tunayopewa kuhusu kujikinga na ajali.
 
Kuna Lori Moja la mafuta lilipinduka mbele ya mto ruvu nikakuta watu na madumu nikaandika humu jamii forums kuwa polisi nendeni mkawapige virungu na mabomu nikatukanwa Sana humu jamii forums kuwa Nina roho ya shetani nk kwa tamko langu Hilo ona sasa maafa hayo
Yawezekan shetw kweli
 
MAANDISHI YAMEANDIKWA KWA HERUFI KUBWA INFLAMABLE,,DANGER, LAKINI HAWAELEWI AU YAANDIKWE KISWAHILI,TENA UNAKUTA HAPA DAR KWENYE FOLENI LORI LIPO MBELE HALAFU UNAMKUTA GARI YA NYUMA LIMTU LINA VUTA SIGARA HUWA NACHUKIA SANA 🙄 🙄ONA SASA WAMEGEUKA NDAFU
 
Back
Top Bottom