Morogoro: Lori la Mafuta lapata ajali na kulipuka, watu 104 Wapoteza maisha na wengine kujeruhiwa...(Picha zinaogofya)

Morogoro: Lori la Mafuta lapata ajali na kulipuka, watu 104 Wapoteza maisha na wengine kujeruhiwa...(Picha zinaogofya)

wapumzike kwa amani,,hivi bado huwa hawajifunzi yale yalotokea mbeya na mbagala
 
Inasikitisha sana....

Kuna siku nilikua njian to tanga,lori la gesi likashika moto berti na mfumo wa mafuta....kila mtu alikimbia gari lake na kutokomea maporini

Wakabak wajeda 4,tingo na dereva wakambana na moto mpaka wakaudhibiti kabla ngoma haijalipuka...

Kwenye msafara alikuwepo NB waziri wakat huo alikimbia bila viatu
 
Hata kama huna ajira mkuu.ndo utafyte kipato kwa njia hatarishi na risky kama hizo?
Kwa kuiba?
Hili bomu la watu wasio na ajira wala uelewa ni kubwa mno hawa watu ni wengi vijana wadogo wengi sana wala hawana kazi ni hatari kweli.
 
Duuh hapa kuwa na askari wa kuwazuia?

Wamesahau ile ajali ya Iringa miaka kadhaa nyuma. Karibu kijiji kizima kiliteketea sababu ya kusombelea mafuta ya bure. Moto ukishika unafata mtiririko wa matone ya mafuta yalipoenda, hivo hadi nyumba ziliungua.

May their soul Rest In Peace.

ilikuwa mbeya nadhani,,kipindi hicho habari inasomwa na rainfredy masako wa itv
 
MAANDISHI YAMEANDIKWA KWA HERUFI KUBWA INFLAMABLE,,DANGER, LAKINI HAWAELEWI AU YAANDIKWE KISWAHILI,TENA UNAKUTA HAPA DAR KWENYE FOLENI LORI LIPO MBELE HALAFU UNAMKUTA GARI YA NYUMA LIMTU LINA VUTA SIGARA HUWA NACHUKIA SANA 🙄 🙄ONA SASA WAMEGEUKA NDAFU
na kweli hapo ni harufu ya mishkaki
 
Uzuri au ubaya tumembwa na kitu kinaitwa kusahau, baada ya miezi miwili kila mmoja atasahau hili na utakuta tukio kama hili litajirudia.

Pole kwa wote walio athirika na tukio hili.
 
Aiseee sio jambo dogo nina kila sababu ya kuilaumu serikali kwa kutowapa bodaboda na wakazi elimu ya majanga kama hayo
 
Back
Top Bottom