A
Anonymous
Guest
Wananchi wa Morogoro Mjini, Kata ya Magadu, tunaomba kupaza sauti kuhusu hali mbaya ya barabara inayoelekea kwenye Kota za SUA zilizopo Kididimo.
Barabara hiyo imekuwa mbovu kwa muda mrefu, licha ya SUA kuwa na magari na uwezo wa kufanya matengenezo ili ipitike vizuri. Hali hii imekuwa kero kubwa kwa wananchi, hasa kipindi cha mvua ambapo barabara haipitiki vizuri.
Tumechoka na adha hii. Tunaomba uongozi wa SUA na mamlaka husika zichukue hatua kuhakikisha barabara hiyo inakarabatiwa na kuwa katika hali nzuri ya kupitika. Je, hadi Rais aje kulisemea ndipo hatua zichukuliwe?